Ifike hatua Waafrika tuache ujinga. Hivi Nigeria maandamano yao yanataka Serikali ifanye nini ili waache?

unajua wanajeshi wanagapi wameuwawa mpaka leo nigeria!!!au ndio kauli za kishujaa tunazoziita!!!

hupendi uwepo wa kituo cha polisi,sawa maana ndio walalamikiwa wakuu.vipi kuhusu kituo cha kupaki mabasi ya BRT???
Na wana wa target mpaka viongozi na familia zao
Hatari ndomana wengine wamekula kona mapema

Ova
 

umeona video za raia waliouwawa!!!!siwezi post huku.

labda nawewe nitumie picha za hao polisi na wanajeshi waliouwawa.
 
Laana yetu kama ipo ni kukosa akili za kutosha na hata mada yako inaonyesha hilo, wananchi ndio mamlaka yote na viongozi waliochaguliwa hukasimishwa baadhi ya mamlaka hayo. Hawa viongozi wakishachaguliwa hujisahau na kuamini wao ndio mamlaka mpaka ya mbinguni. Wananchi wakichukizwa na uongozi uliopo wanaweza, leo kuandamana waziri mkuu atoke, kesho iwe zamu ya IGP na hata kutaka serikali nzima itoke madarakani.
 
Mi nasubiria mtiti wetu Tanzania.

sijui JF itakuwa hewani au ndio tutakuwa tunachapana kimya kimya.
 
Hahaha walioshiba huwa hawapendi nasi tupate haki.

Kila kitu kwao ni bugudha, sasa haki itapatikanaje bila maandamano?!

Walioko madarakani wana abuse power, eti nao hawataki tulalamike, yani watuibie tukee kimya, Police brutality tukae kimya.

Wafanye wafanyavyo kutuumiza, tukae kimya tu.

Angalau mgetuambia tutumie njia gani kulalamika, bunge mmelichukua wenyewe

Hakuna kukaa kimya, no justice no piece.
 
Wanachotaka ni mageuzi ya jeshi la polisi.

Hivi sasa, wengine wamekwenda mbali zaidi na kumtaka Buhari ajiuzulu.
Watapata wanacho taka, ngoja wakifikia point kama ya Libya, Syria, Iraq na sudani ndio watakaa vizuri.
 

Ni aibu kwa mtu mwenye ngozi nyeusi kuongea Huu Ujinga, haujielewi kabisa!

Ingekuwa mbaya zaidi kwa ngozi nyeupe! Usidharau kila kitu!

Mwanzo ni serikali ingeitikia vyema ni sawa, walichelewa, sasa wananchi hawarudi nyuma!

Ukimpiga mtu na kumwonea sana kuna namna ule uoga una kwisha, then inabaki chuki tu
 
Mambo haya ya kikatili tunayoendekeza ndiyo yanazidisha laana kwa waafrika. Belarus wana kama mwezi wanaandamana kila siku lakini hakuna mauaji ya binadamu.

Kwanini nyie waafrika mnaona solution ni kumwaga dam tu?
Mtu mweusi akiachwa pasipo kuguswa huhisi kudharauliwa hapo huanza kufanya uharifu mwingine kama kuchoma magari na kuvunja maduka ya raia wengine
Hapo ndo definition ya laana huanza kujionesha
 
Mtu mweusi akiachwa pasipo kuguswa huhisi kudharauliwa hapo huanza kufanya uharifu mwingine kama kuchoma magari na kuvunja maduka ya raia wengine
Hapo ndo definition ya laana huanza kujionesha
Mungu akusamehe kwa roho hiyo ya kikatili iliyo ndani mwako.
[emoji120]
 
ndio maana tunasema madai yoyote ya haki yakisukumwa kimihemko hayazai matunda yaliyokusudiwa.

hamtaki SARS,imetolewa.mnataka muipangie serikali namna ya kufanya sasa!!!mwisho mtataka na polisi wote watolewe maana hawafuati misingi ya haki.
YES"" Wanannchi ndio wanatakiwa kuipangia serikali nini cha kufanya.
Serikali inayokataa kufata matakwa ya wanannchi hiyo serikali inakosa uhalali wa kuongoza hao wanannchi.

Kiburi chako kinakuongoza kwenye hata kudharau matakwa ya wanannchi.
Mungu akusaidie kwa ulevi uliokulemea.
[emoji120]
 

mwananchi akitaka asilipe kodi serikali inatakiwa imsikilize si ndivyo???vipi akitaka asipangiwe miaka ya hukumu??

kuna sheria,na lengo la sheria ni kumchunga mwananchi katika mstari mnyoofu.ukitaka kuipangia serikali maana yake hauko katika mpango wa kuongozwa na sheria.
 
Nimekwambia wananchi, siyo mwananchi.
 
Conclusion tayari unayo, unauliza nini?
 
Ujinga mwingine uko hapa kwa CCM na Magufuli. Wanafikiri wanaweza kutawala kwa NEC na polisi. Ngoja tuone tarehe 27 na 28 Okt 2020.
 
Nimekwambia wananchi, siyo mwananchi.

wananchi kwa ujumla wao hawapendi kodi,hawapendi kunyinwa uhuru kwa kiasi chochote kile.

sasa uhuru wowote usio na kiasi hakuna utawala hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…