Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Mimi ni mwalimu Nina vipindi 72 Kwa wiki afu inasema demand ni ndogo. Emu fanta utafiti kwanza walimu wa shule za umma wanakabiriwa na workload na mlundikano wa wanafunzi mkuuu mkondo mmoja wanafunzi Hadi 120
 
Mimi ni mwalimu Nina vipindi 72 Kwa wiki afu inasema demand ni ndogo. Emu fanta utafiti kwanza walimu wa shule za umma wanakabiriwa na workload na mlundikano wa wanafunzi mkuuu mkondo mmoja wanafunzi Hadi 120
Tunaposema Demand tunamaanisha Demand katika soko la ajira, sio huko mashuleni! Una elimu gani ndugu yangu? Concept ndogo kama hii inakushinda kuelewa?

Kwamba serikali inatoa nafasi 1000 za ajira kwenye soko, lakini mtaani kuna walimu laki 1 wanasaka ajira, means supply ni kubwa ila demand ni ndogo.
 
Unaelewa maana ya soko tuanzie hapo kwanza ww mwenye elimu kubwa
Sizungumzii soko, nazungumzia soko la ajira, legeza ubongo kidogo basi. Soko linaweza kuwa la viazi, ndizi, dhahabu nk; ila hapa specifically nazungumzia ‘SOKO LA AJIRA’. Pia sijasema nina elimu kubwa, nimeuliza tu elimu yako.
 
nyote mupo sahihi ila munaongelea muktadha tofauti, soko la ajira zinatangazwa kidogo kulingana na graduates, lakini uhitaji mashuleni ni mkubwa.
 
Mimi ni mwalimu Nina vipindi 72 Kwa wiki afu inasema demand ni ndogo. Emu fanta utafiti kwanza walimu wa shule za umma wanakabiriwa na workload na mlundikano wa wanafunzi mkuuu mkondo mmoja wanafunzi Hadi 120
Walimu walio mtaani ni wengi

Serikali haina uwezo wa kuajiri na ina upungufu wa walimu 171,000 kw shule za msingi

74,000 kwa shule za Upili
 
Tukubaliane na hali halisi, walimu wanaosubiri ajira mtaani ni wengi mno, na ambao wako mbioni kuhitimu na ni wengi, maelfu kwa maelfu, ukijumlisha na walio mtaani wanaweza kufika makumi ya maelfu.

Tusipochukua hatua hii, ipo siku idadi ya walimu itakuwa sawa na wanafunzi. Hivyo basi tujiulize, nini hupelekea mtu kusomea ualimu huku akijua kabisa tatizo lilipo la over-supply ya walimu? Je ni kukosa taarifa ya hali ya soko la ajira ya ualimu? Je, ni viwango vidogo vya ufaulu vinavyowekwa kama vigezo vya kusomea ualimu? Au ni nini hasa? Maana mishahara ni midogo, na mazingira ya kazi ni magumu pia, so then why mnasomea ualimu?

USHAURI:
1.) Vijana muende mkasome VETA, achaneni na ualimu, huku mtaani kuna demand kubwa ya watu wenye technical skills mbali mbali, huu mtego tuliowekewa na mkoloni kwa mfumo wake wa elimu umetutesa vya kutosha jamani, inatosha!!!! Enough is enough, huu uchawi wa mkoloni ufike mwisho, ni uchawi hatari sijawahi ona, ufike mwishoo!

2.) Serikali ipige kodi nzito mno bidhaa yeyote inayoagizwa toka nje ambayo pia inadhalishwa hapa nchini; tumeanza na fenicha toka China, angalau sasa vijana tunaona jinsi wanavyotusua kwenye biashara za useremala huko Instagram, vijana wamejiajiri na wanauza vitanda, masofa, makabati ya nguo , meza, dressing table n.k, kabla ya hapo waChina walikuwa wanaua kabisa hizi ajira na makabati yao ya pumba za maranda ya mbao. Na bado ongezeni kodi hizo fenicha ili walau vijana watakaoenda VETA wakitoka huko wajiachie na kujimwayamwaya kwenye nchi yao, tusiwanyanyase, pigeni kodi nzito!!!!

3.) Wachomelea mageti, Alluminium na glass nao naona wanakula kiulaini sana huko instagram, majengo mengi siku hizi watu wanaweka magrill ya chuma, glass na alluminium kwenye madirisha, vijana wanajimwayamwaya sana kwenye hii sekta, sasa kikubwa ni kuhakikisha wale wazalishaji wa ndani wa vitu kama alluminum , steel nk. wapewe upendeleo wa aina yake ili yale washindane na zinazotoka nje, vijana wapate ajira huko. Either way, vijana mkasomee huu utalaam wa kuchomelea mageti yale ya kisasa na madirisha ya alluminum, fungueni ma-account Instagram, tangazeni kwa fujo (sponsored ads) mle mema ya nchi yenu nyei, achaneni na ualimu.

3.) Washonaji wa seatcover za magari nao nimeona wanafaidi vinono huko instagram, sasa kikubwa yale maseat cover ya kutoka China yapigwe kodi nzito hadi waagizaji waone kizunguzungu, kiukweli huu utaalam inabidi vijana muende VETA mkasomee hii taaluma, inaitwa ‘CAR UPHOLSTERY’ aisee hii ni tamu, nadhani zile ngozi zinazotupwa vinginguti zitakuja kiwa lulu, maana Upholstery inakuwa tamu kupindukia ukitumia ngozi halisi, achana na yale maleather famba toka China, yaani gari inarekebishwa Dashboard inakuwa tamu hadi unatamani uilambe, seat covers za ngozi zinautamu wake jamani, Instagram watu wanafaidi sana kwenye hiki kitengo, achaneni na ualimu, tumieni akili vijana, magari yenye uchakavu wa interior ni mengi kupita maelezo, go where the demand is!

Nikiamka asubuhi naweka list ya vitengo kama kumi hivi ambapo watu wanalamba asali kiulaini huko instagram, ila kwenye mzinga wangu sitawaambia, bado nalamba lamba mwenyewe kwanza, nikishiba nitawaambia.[emoji23]

==================================

4.) Huko Instagram nimebaini pia kuwa kitengo cha BAKERY (CAKES) wananyonya vitamu kiulaini sana! Siku birthdays zimekuwa ni kitu cha kawaida, hadi watu wazima wanafanya birthday, na hii shughuli kiungo chake muhimu ni Keki, halikadhalika graduations za vyuo, maharusi nk; kote huko keki zinahitajika. Vifaa vya kutengeneza keki vinapatikana kwa urahisi na ni bei nafuu sana; mkosomee kozi za bakery jamani, tena ukija kubabatiza order za keki za harusi ndio utaona utamu wa bakeries, keki unatumia laki2 kutengeneza ila unauza laki8. Unatafuta hata bodaboda unaemuamini anakuwa anafanya deliveries sehemu mbalimbali, anapewa pesa on delivery anakuletea. Tena hii unaweza kufanya baking ya keki hata chumbani kwako, unatangaza Instagram kwa sponsored ads wateja wanamiminika tu, keki ziko on high demand jamani, tukajifunze BAKERY!

=============================
Update: 25/10/2021


==========================
Update: 10/08/2022


===========================
Update: 05/03/2023

Serikali imetoa nafasi kwa vijana wote wa kuanzia miaka 18 - 35 kusomeshwa bure kwenye vyuo vya ufundi stadi VETA, unatakiwa kwemda kuchukua fomu na kuijaza tu, serikali itakulipia ada kwa 100% , walemavu watapewa kipaumbele
Coz zipo nyingi, pia wanaohotimu ni wengi, ni , achaguo Yao Nini wakasomee. Lakini sisi ambao tayar tumepita huko tujaribu kuwashauri Ili tusijazane wa kozi Moja huku mtaani[emoji24][emoji24][emoji24] ni shidaaa.
 
Niliwahi kumpatia huu ushauri Shangazi yangu ambaye anamlipia ada dogo mmoja ambaye alidahiliwa kusoma Bachelor of Education with psychology..

Nilishauri kuwa kulingana na mazingira huyo dogo akasome VETA kutafuta ujuzi.. nilijibiwa kuwa haiwezekani mtu amefaulu vizuri halafu aende akasomee vitu vya ajabu.
Hata kama hakuna ajira ila huwezi fananisha bachelor degree ya kitu chochote na veta
 
 
092009AE-333A-4150-A815-E0A6AD247108.jpeg
 
 
Tatizo mfumo hovyo wa elimu ya kikoloni..
Lazima ufike chuo eti..!?? Uvae tai..

Hakuna mijitu ina hela saivi kama mifundi ujenzi
Ni kweli aisee.
Fundi ujenzi anakabidhiwa kazi pamoja na materials yote yashaandaliwa halafu malipo ya ufundi wake anapewa kati ya 2m hadi 3m kwa kazi ambayo ataifanya ndani ya wiki 2 tu wakati pesa kama hii kwa mwalimu kuishika ni ndoto labda hadi aende kukopa benki.
Kuna vijana fulani pia nawajua wamesimea veta mambo ya umeme na mitambo wanakula mishahara ya takribani 800k kwa Azam ambayo ni mara 2 ya mshahara wa mwalimu.
Maisha wakati mwingine ni hesabu na ujanja sio kukariri.
 
Kusoma VETA ni wazo zuri

Ila maisha yanahitaji zaidi soft skills kwa kiasi kikubwa kuzidi hard skills

Wapo mafundi wengi Sana wamepita VETA n.k Ila bado hawana positive impact kwa jamii zao n.k


Swala la demand and supply lazima liendane na jinsi MTU alivyo smart kichwani (Upstair)

Ukiwa Una hard skills bila soft skills utakuwa MTU wa kutumikishwa na WATU maisha yako yote.

Hivyo kila MTU akae kwenye eneo lake analolimudu vizuri
 
Wanaoishauri na kusimamia serikali wamejitangaza dhahiri niwezi wa kura. Hatutasonga mbele.
 
Back
Top Bottom