Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Nimeelewa sana....mimi 1999 niliona eti vyuo au fani kama sociology agriculture ualimu etc havina soko kwenye ajira labda wajiajiri wenyewe...nikabadilisha fani....sasa kilio kumbe kiko pale pale....sasa fundi mchundo....
 
Update: 05/03/2023

Serikali imetoa nafasi kwa vijana wote wa kuanzia miaka 18 - 35 kusomeshwa bure kwenye vyuo vya ufundi stadi VETA, unatakiwa kwemda kuchukua fomu na kuijaza tu, serikali itakulipia ada kwa 100% , walemavu watapewa kipaumbele
 
 
Hakika ndugu FRANCIS DA DON ulikuwa na maono ya mbali.
Kongole sana na Mungu akubariki sana.
 
 
Info nzuri sana. Changamoto kijana anaona kuiweka pembeni division one points 6 au 7 halafu aende akasome Tailoring, Welding au Embroidery VETA au Taasisi yoyote ya ufundi anahisi kama umemtukana hivi. Kasumba ya kufika chuo kikuu anawagharimu. Kwa wakati huu maarifa uliyopendekeza ni sahihi kabisa.
 
Kozi nyingi formal ni saturated na zitaondolewa na AI iwe kwa kutaka au kutotaka, zitakufa tu naturally.

Kazi za mikono hazitakufa kamwe, watu wajikite huko, watu waache kiburi na majivuno, waende VETA wajipige brush maisha yatasonga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…