IFIKE MUDA UKUBALI KUWA HUYO SIO HADHI YAKO, ACHIA WENYE HADHI YAKE WANYOOSHANE 😊

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
KUNG'ANG'ANIA ASIYE HADHI YAKO SHARTI UKUBALI KUIGIZA NA KUTUMIKISHWA 😔

Sio vibaya kukubali kuwa huyo hamuendani kuliko kujitutumua uonekane ni hadhi yake huku sirini unaumia na kunyanyasika.

Mtu ambaye anataka matumizi ya laki tano kwa mwezi ilihali mshahara wako kabla ya makato ni laki nne hadi kukufikia una laki tatu na nusu ila unajionyesha umwamba wa kutaka kummudu? Utakopa sana na usipokuwa makini utajikuta kwenye tabia za utapeli sasa yote hayo ya nini? Mwache tu akaendane na wa hadhi yake huko ili wanyooshane vizuri.

Kuna mambo ya kuvumilia na kuna mambo ya kunyoosha mikono kuwa umeshindwa sasa uwaachie wanaoweza ili wanyooshane la sivyo utaanza maisha ya kuigiza furaha ilihali una majeraha mabichi au utaanza kuigiza maisha ili ujikuze kwenye hadhi yake ambapo utaumia zaidi.

Kuna mtu mpaka analazimika kununua vitu fulani ili ajiweke kwenye hadhi ya kupendwa na fulani ni kweli utafanikiwa kumfanya apende vitu vyako ila je utaweza kuishi hivyo muda wote? Siku ukirudi kwenye uhalisia wako unadhani kutakuwa na mapenzi tena?

Lazima tujifunze kula kulingana na urefu wa kamba zetu ili tuwe salama na kuepuka kuishi maigizo ili tuwavutie wasio tupenda bali wanapenda tulivyo kwenye maigizo.

Kama kweli unataka muishi vizuri na kwa muda mrefu usikubali kumfanyia vilivyo nje ya uwezo wako ni bora akuache tu kuliko kugeuzwa mtumwa na pia usikubali kujipa uvumilivu usioweza ni bora muachane tu ili akuvumiliwe na wengine huko.

Mwanasayansi Saul kalivubha
Fikia Ndoto zako.
 
1724257660565.jpg
 
Kwa kifupi mapenzi ni biashara.
 
Back
Top Bottom