Ifike wakati mambo ya Muungano yasijadiliwe kama turufu za wanasiasa, tuendako siko!


CHAWA HUNA HOJA. WATANGANYIKA WANYONYAJI.
 
Muungano unahusu watu sasa iweje usijadiliwe? Kuna nini mnachoficha ? Au kuna siri gani ? Jibuni hoja zinazoibuliwa kama mnauona ni mzuri elezeeni hayo mazuri watu wapime wenyewe
HUYO KILAZA HAJUI LOLOTE. USIDHANI NAYE NI MTU
 
ukosefu wa kazi kwa wanasiasa mahali pengi duniani hua kuna vihoja na songombingo sana. na wengine hua rahisi sana hata kurubuniwa, kushikwa akili na na mabwenyenye na kukubali kua puppets🐒
Nani sio puppet hapa africa?
 
Tulia watu tufurahie amani na umoja na mshikamano. TANZANIA ni njema atakae aje
 
Hamna kitu kugumu kama penzi la kulazimisha. Lazima itafika mahali litavunjika tu.
 
Dikteta asiyevuma lakini yupo...

Hypocritical wao wakijadili ni sawa ila wengine si sawa
 
Unaweza kunitumia kero kumi za muungano alizotatua ili tuanzie hapo
kwanini nikutumie mim hali ya kua nimekushauri bayana cha kufanya....

fuatilia vizuri, kwa utulivu na umakini bajeti ya wizara husika, na utajifinza na kujua mambo mengi zaidi ya hayo machache sana kumi, ambayo unahitaji kutoka kwangu

hili jambo ni la umma sio la mtu binafsi. halihitaji uvivu kulifuatilia na kulijua vema....,

uelewa na ufahamu mdogo kwa wengi juu ya kero za mambo ya muungano zilizopo na zilizotatuliwa na ambazo ziko bayana kabisa ni mkubwa..., labda kwasababu ya muda au majukumu, wengi wa wanainchi hususan wewe mnakosa fursa ya kufuatilia na kuelewa mambo haya....

ndio maana nakusanua tena na tena wewe pamoja na JF fraternity kwa ujumla, fuatilieni bajeji ya wizara mahususi inayoshughulika na mambo ya muungano, kero, maswali na majibu kuhusu muungano zitabainishwa huko na si vinginevyo....
 
Dikteta asiyevuma lakini yupo...

Hypocritical wao wakijadili ni sawa ila wengine si sawa
Vyama vya siasa vipelekewe amendment ya nyongeza itakayo ongezewa katika taratibu zao za usajili, "katika siasa zao, suala la muungano sio suala la kisiasa, hivyo halitakuwepo katika kunadi sera zao!, kwa sababu lina Senate yake maalumu,ambayo inahusika na suala hilo, chama kitakachokataa kusaini kitakuwa kimejifuta chenyewe, hatupendi awamu ya sita, iwe ya maaribufu, tunataka awamu ya sita iwe ya uimarishaji katika kila sekta!
 
Wizara hiyo ipo, facts, lakini kwa unyeti wa suala hili mkazo zaidi unahitajika ili kulilinda kwa Senate yake maalumu. Itakayokuwa chini ya rais wa "" jamuhuri ya muungano ya watu wa Tanzania.""
Baraza la Senate linaweza kuwa wazo zuri, lakini litaundwaje bila marekebisho ya Katiba.
 
sheria IPO: Chama Cha siasa kilichosajiliwa kitaweza kufutwa kama chama Cha siasa iwapo Moja ya malengo yake ni kuvunja Muungano.
Kifungu hiki kipo labda kingeundiwa kanuni zake.
 
Tunachosikia ni mapambio tu rais Samia ametatua kero nyingi za muungano kuliko Marais wote lakini kero hazitajwi ndioaana nimekuuliza wewe unayezijua ututajie.
 
Tunachosikia ni mapambio tu rais Samia ametatua kero nyingi za muungano kuliko Marais wote lakini kero hazitajwi ndioaana nimekuuliza wewe unayezijua ututajie.
halipo ambalo halijajibiwa kwenye bajeti, you are free usome kwenye bajeti ama laa
 
Mnataka kuficha nini?
 
halipo ambalo halijajibiwa kwenye bajeti, you are free usome kwenye bajeti ama laa
Waziri wa Muungano ni Jaffo yeye ndiye aliyemsifia rais ametatua kero kushinda Marais wote , sizungumzii hotuba ya bunge hili.
Kwa kifupi kero kubwa ya muunganoni usiri wa kufanya maamuzi bila kuwashirikisha wadau ambao ni wananchi.
Na hizo wanazoita kero Wala sio kero Bali ni upendeleo wanaotaka Zanzibar .
Juzi tumemsikia Zitto akilalamika Zanzibar kupewa asilimia 2 ya.mapato ya muungano lakini hasemi kuwa hata hiyo asilimia wanayopewa hawastahili sababu hawachangii chochote.
Wamedai wapewe payee wanayotozwa wafanyakazi wa Zanzibar waliopo serikali ya muungano wakati hata hiyo mishahara hawachangii chochote Bali ni Kodi zinazokusanywa bara.
Hata mshahara na pesa anazotumia rais ni Kodi za watu wa Tanganyika.
 
ikiwa unatamani kuskia unachotamani au kutarajia wewe kiwe ni jambo jema, lakini si lazima wengine wafikiri hivyo pia....

usipopenda kuskia au kujua usichokipenda, hilo linabaki jambo binafsi, lakin kwenye bajeti kila kitu kimeelezwa vyema sana na kinagaubaga na tunasonga mbele vizuri sana kuhusu muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…