"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Pasal wewe ni figure "kubwa". Umeandika muda mrefu na kujijengea jina kubwa.
Thanks
Nikueleza ukweli...umekuja kukengeuka wakati wa Magufuli na ulipoitwa na bunge. Ulitishwa na ukatishika na kugeuka nyuma ukawa Jiwe. Afadhali ungelinyamaza kuliko kukengeuka na kubadili msimamo!
Sikuwahi kukengeuka wala kubadili msimamo wowote!, kosa langu ni moja tuu na hili nitaingia nalo kaburini!, ni kuwa mkweli daima!.
Si wengi wanaofahamu kuwa hata shetani mwanzo alikuwa malaika!, sasa kwa watu walioaminishwa shetani ni mbaya, ukiuzungumzia umalaika wa shetani, utaonekana umekengeuka!.

Pamoja na madhaifu yote ya Magufuli, alikuwa na mazuri yake and over the time he kept changing for the better, sasa ukiwaeleza watu ukweli wa mazuri ya Magufuli, unaonekana umekengeuka!.
Mama Tanzania Mbatia, baada ya kunyanganywa chama na Mutungi, amekaa kimya lakini hakukengeuka!
Kiukweli kabisa kuna mengi, makubwa, mabaya nayajua na nimenyamaza!.
Finally, we angalia wanavyokuandika hapa JF, kila mmoja anasema you were smart huko nyuma, not today
Kama mtu ni smart bonafide genuine, he will always be smart!.
Nakukumbuka sana toka nyuma ulipokuwa MC pale Peakcock Hotel harusi ya akina Malinzi! I was there!
Duh...!. Umenikumbusha mbali!. Kumbe tunafahamiana in person!. Kina Malinzi ni watu wangu toka enzi za DJB!. Walinipeleka South Africa, Dubai na mpaka nimefika kwenye lile kasri lao Tum park lane, London!.

Naomba nikuhakikishie Pasco yule wa Kiti Moto ni yule yule wa juzi, jana na leo!, kilichobadilika ni the environment.
P
 
haelewekagi huyu. Mimi nimekimbilia kwenye reactions sijaona like ya the boss wala faizafoxy nikaona ngoja nisome. Leo kaliponda bunge Kama mwabukusi.
Nafikiri ni kitengo. Uzi kama huu ni kuficha kazi yake rasmi.

Anakwambia maslahi ya CCM ni muhimu kuliko ya Taifa.
 
"kama tumeshindwa kuiendesha Bandari yetu kwa ufanisi, hivyo hakuna ubaya wowote kusaidiwa! HAPA" Tanzania ni nchi inasomesha wananchi wake na haitakiwi iseme haiwezi kujiendesha hivyo itawakodi watu wenye akili zaidi kutuendesha nchi! Mimi ningeunga mkono swala hili la bandari endapo ningesikia watanzania wamepelekwa huko kwenye watu wenye akili wakajifunze, badala yake eti tulipeleka wabunge na wapiga debe!
Nahitimisha kwa kusema watanzania tumeamua kuwa watu wakubwabwaja siasa kwakua tumeshindwa kuendesha makampuni yetu, sijui hali hii nayo itatuchukua miaka 100? Mungu wao aliyewaumba na mungu wetu wanatofauti kubwa sana.
 
Mkuu, kuwapata kwenye tovuti ya TLS ni ngumu, maana database iliyopo kule ni ya mawakili wa kujitegemea. Tanganyika Law Society ni chama cha mawakili wa kujitegemea Tanganyika ( Tanzania bara), kabla ya 2019 mpaka mawakili wa serikali walikuwa wanaruhusiwa kuwa wanachama TLS lakini baada ya hapo sio wanachama wa TLS, kwa hiyo kutowaona huko haimaanishi kuwa ni vilaza. Wameanzisha society yao kama kumbukumbu zipo sawa.

Tovuti ambayo unaweza kuona mawakili waliopo kwenye rejista ya mawakili nchini (kwa idadi kubwa) ni ewakili.judiciary.go.tz hii ipo chini ya Mahakama ya Tanzania ambao ndio watunzaji wa daftari na ndio wanaowasajili mawakili.

Hata hivyo, sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu (utendaji kazi) na hata sheria ya mawakili, inawatambua wanasheria walioajiriwa kwa nafasi za mawakili wa serikali (state attorneys au Law Officers) kuwa ni mawakili, bila kujali kama wapo kwenye database ya mahakama au ya TLS.
 
Wanyumbani uliniangusha sana kwa kuuma uma maneno kwa hoja nzuri na jadidifu kama hii!

Unajitetea kwa nani kwamba thread hii bomba isionekane ni statement bali ionekane ni questionair!

Mbona katikati mwa bandiko lako umesema wazi kwamba kuanzia Serikali, Bunge na Mahakama kuna vilaza wa kufa mtu, je hilo ni swali au ni statement?

Kwanini ujitetee kwa kutoa hoja za kweli na zenye manufaa kwa umma?

Au bado una kihoro cha kuburuzwa Bungeni kwenda kusimangwa?

Hata hivyo kwenu wanasheria, Bunge kujigeuza kuwa ni mahakama ya kuadabisha watu wanaoonekana kulikosoa, hili limekaaje kisheria ni sawa?

Kwanza walikulipa nauli ya kwenda na kurudi pamwe posho ya njiani na malazi, au ulienda kavu kavu?

Mkuu weka statement sawa kwamba Serikali nzima (ikiwemo Bunge na Mahakama) imeoza inahitaji reform ya ki ICU, vinginevyo tunakokwenda kama Taifa, tunaenda kuangukia pua.
 
Na ulipotoka kule ukaufyata, kabadilika na kuwa Pascal Mayalla mpya, mwoga, mtafuta teuzi... au nakusingizia rafiki yangu

Hili andiko lako n zuri nilikuwa sijaliona... sikumbuki kuliona
 
Ukiacha kutetea DP world tutakuunga mkono
Mkuu JakiDubai, kuna watu wanaandika jf ili waungwe mkono?, utaniunga mkono ili iweje?.
Anyway karibu, hili ni moja ya mabandiko yangu kuunga mkono IGA ya DPW na Bandari zetu, angalia tuu tarehe ya bandiko hili ili ulinganishe na wengine, na ikitokea una uwezo wa kusoma contents, soma contents uone jinsi ninavyoisupport DPW na Bandari zetu!.

Karibu

P
 
Paskali
Sikuwahi kusoma.hili andiko lako.

Nimelisoma, pia narufia kusoma ili nipate uelewa mpana kisha nizingatie maangalizo uliyoyatoa.

Je msimamo wako bado ni ule ule?
 
Mkuu Paschal Mayalla, kati ya wanasheria na waandishi wa habari wagumu kuwaelewa, wewe ni mmoja wao!! Kwa maneno yako mwenyewe wakati debate inapamba Moto, uliilinganisha hii IGA na kishika uchumba. Nilikuona mwanasheria wa ajau kama unavyowashangaa wanasheria wengine walihusika kipindi cha kuisaini hadi kuipitisha bungeni.

Msimamo wako ni msimamo wa kila Mtanzania anaependa maendeleo ya nchi hii kwamba bandari zetu ziendeshwe kwa ubia na wawekezaji hilo halina ubishi. Lakini wawekezaji wababaishaji na waporaji kama DPW, natofautiana na wewe hata kama hiyo IGA itabadirishwa. Nia yao mbaya imeonyeshwa kwenye huo mkataba ambao mnauita makubaliano. Bila kuangalia kesi lukuki za hii kampuni kote duniani, huo mkataba ambao naamini waliutayarisha wao, inatosha kabisa kutokuaamini.

Rai yangu kwako ndugu Mayalla, wewe ni mwandishi wa habari wa. muda mrefu, chukua upande ili msimamo wako ueleweke. Hii ya kuandika makala nyingi na ndefu zinazopingana kutokana na upepo wa kisiasa haikupi heshima kama mwanasheria. Lugha yako inaonyesha wazi kuna kitu unakitafuta. Si mbaya kutafuta lakini kuwa mkweli na mtu mwenye msimamo kutakuongezea heshima.
 
Hivi unawezaje kupata usingizi kwa mashambulizi haya. Unajitahidi sana lakini kila nikipita mitaa hii naona unashambuliwa tu.
Japo nina ngozi ngumu kama gamba la kobe, lakini ni kweli sipati usingizi ndio maana niko macho mpaka saa hizi
P
 
Japo nina ngozi ngumu kama gamba la kobe, lakini ni kweli sipati usingizi ndio maana niko macho mpaka saa hizi
P
Pole mkuu, angalia afya yako, maana dunia hii hata ukifanya vizuri vipi binadamu huwa ni wale wale hatubadiriki. Nadhani kwa umri wako umeshaona mengi sana yasiyopendeza na yenyekupendeza. Umejifunza miaka mingi kukosoa mifumo yetu hii unaambulia matusi na masimango,hata kama ushauri wako uliikoa Dunia na janga la maangamizo.
Nafahamu uandishi ndio unakupa mkate wako wa kila siku, lakini labda ungekuwa ukiishatupa jiwe gizani nawe unaendelea na maisha mengine. Hii kutujibu sisi nadhani itakuletea stress bure, na magonjwa ya moyo.
 
Asante sana nitazingatia ushauri na baada ya kujibu post hii nimezima data kutafuta usingizi.

P
 
Asante sana nitazingatia ushauri na baada ya kujibu post hii nimezima data kutafuta usingizi.

P
Pumzika mkuu, hutobadirisha misimamo ya watu kwa kuandika au kuzungumza hata kama ungekuwa na sauti kali au nene kama simba. Toa mchango wako, na endelea na maisha mengine.
Hutowea kushinda kwa kubishana humu. Humu tupo watu wa kila namna.
Lala pumzika na shemeji, akifurahi moyo wako unaimarika. Hata ukipumzika vizuri utaamka uko vizuri, na afya yako itaimarika.
Ubarikiwe sana.
 
Nimeandika nimeona Bora nifute.
Kwa Bei rahisi ngoja niseme kidogo tu.

Raisi wa Marekani Donald Trump na Mchungaji Christopher Mtikila walieleza kila kitu kuhusu nchi za Kiafrika na Waafrika.

Hao walisema hivyo kwakuwa ni watu walio shika mafundisho ya Dini zao vizuri.

Sisi Waafrika ni Bora Kama tungekuwa tunaendelea kutawaliwa na Wazungu kwa mkataba wa miaka miambili na hata zaidi hadi tustaarabike.

Ni kwamba Waafrika Weusi bado hatujafikia hatua ya kuwa Binadamu kamili aliye staarabika.

Bado tuna Unyani mwingi sana.
Hata tuwe na PhD mia hali ni hiyo hiyo.
Tazama mambo anayoyafanya Profesa mmoja maarufu wa chama flani cha upinzani.
Huyo ndio Profesa Mweusi mahili sana katika fani yake.

Muweke Mtu yeyote Mweusi pale kwenye kiti cha Enzi mambo ni Yale Yale au zaidi ya Yale

Ki ukweli hatuwezi kujitawala.

Nenda Kongo, Somalia, Sudani, Nigeria, Msumbiji, na nchi nyingine
wanazokaa Waafrika Weusi mambo ni Yale Yale.

Huwa najisikia fedheha kubwa sana kuitwa mtu mweusi mbele ya Wazungu kwa Jambo hilo tu.

Hadi muda huu kuitwa "Black Man" ni tusi kubwa sana.

Jiulize ni kwa nini liwe tusi, hali ya kuwa rangi haina shida yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…