"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Suala sio mkataba suala ni wapigaji wa hapo bandarini kusikitika wanapoona ulaji wao unawachomoka.

Kutoa kontena moja bandari ya Mombasa ni dola 1300 wakati kutoa kontena moja hapo TPA ni zaidi ya dola 3000.

Hiyo tofauti ya dola 1700 ndio chanzo cha maneno yote haya ya humu jamvini.

Ndio chanzo cha fitina na majungu mengi wanayofanyiwa wanasheria wa serikali mpaka muda huu.
Ficha ujinga wako, management ya bandari imeteuliwa na nani? kama kuna upigaji alaumiwe nani? kama wapigani weusi wenzenu mnawajua mnakaa kimya hao weupe mtawaweza? report ya CAG ni wizi mtupu ila mpaka November kujadiliwa bungeni ndio ujue hatupo serious kabisa kama nchi no wonder miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado nchi ni masikini..
 
Karibia kunakucha endelea kukomaa, endelea kupanda.mbegu very soon utakula kivulini, mwaka hautaisha hujalamba teuzi, take it from me.
Hakulamba kipindi Cha Kaka yake ngosha, Badi asitegemee kipindi hiki Cha Wala halua
 
Pascal katika Ushauri wako hiyo No. Kuwa mikataba yote ihusiyo maliasili ilidhiwe Bungen, sheria ya mwaka 2017 inasema hivyo ila kwa bahati mbaya ndo wamepeleka amendment Bungen kuondoa hicho kifungu.
 
Huko bado, hayo yanafanyika kwenye project agreements. Ndio maana ata kwenye hiyo IGA wanakueleza mikataba hiyo itakuwa siri baada ya kukubaliana.

Ndio tuelewe hiyo IGA aina maajabu yoyote out of the ordinary as far as treaties go. Sasa kama yaliomo humo wanasheria wetu yanawasumbua huko kwenye mikataba ya uwekezaji watakutana na scenarios za ‘probability analysis’ ya mrejesho wa investment on different projection scenarios. Kama uyaelewi hayo mambo investment inayorudisha hela yake kwa miaka 10 unaweza kuwekewa mazingira ikageuka 20 years.

Kwa team ile aliyoenda nayo waziri juzi sijaona mtu pale wa kuingia mikataba ya concession agreements, walau Kakoko ulikuwa ukimsikiliza unaona anauelewa mpana wa maswala ya investment. Hope team iliyokuwa chini yake bado ipo bandarini au serikalini.

Iyo IGA sio lolote, sinema hipo kwenye mikataba inayofuata.

Jitahidi ndugu Mayor Quimby unapoandika usiisahau "h", kwani wakati mwingine unapoisahau "h" , sentensi yako inaweza leta maana tofauti.
"ata" ni "hata".
"aina" ni "haina".
"uyaelewi" ni "huyaelewi"

Ni kweli kwenye ile team ya Mbarawa,hakuna "kichwa" cha kuingia mkataba kama ulivyoandika.
 
binafsi nimegundua viongozi wetu ni Vilaza waliotukuka sana , ndio maana nchi ina mkwamo wa maendeleo sababu kubwa tumeongozwa na watu wenye uwezo mdogo kiakili miaka mingi tu toka uhuru,
Tatizo la msingi sana sana hili,na ndio chanzo cha kutokupiga hatua kimaendeleo.

Watanzania wakishakuwa viongozi,wanajiona wao ndio wana akili sana sana zaidi ya wote wasio viongozi.

Kama nchi lazima turudi kwenye "drawing board" kutengeneza mfumo bora wa kutengeneza viongozi.

Huwezi kuendelea kama huna "succession plan", iwe kifamilia, kibishara, kinchi.
 
Shida kubwa ya azimio la Arusha .I dola kumiliki menejimenti ya njia kuu za Uchumi! Mengine yalikuwa safi.
Mkuu, ongezea na hili, kwamba nyakati zile ilikua ni lazma kuanza STRICTLY. Mambo ya kina Kambona baadae kwa ujyaji wangu natafsiri kama ilikua ni dalili za mwanzo kabisa za subversion. Issue ikiwa kwamba, TUSITOBOE kamwe. Yote yanejianika leo hii. Rejea pia andiko la Prof. Chachage (RIP) .. mambo ya makuadi. Muhimu ni pia kwamba tukiendelea kulala CHALI tusitegemee kutoka shimoni. Tufika pahala tutawaliwe na mashoga kama IRELAND, LUXEMBOURG....
 
Ficha ujinga wako, management ya bandari imeteuliwa na nani? kama kuna upigaji alaumiwe nani? kama wapigani weusi wenzenu mnawajua mnakaa kimya hao weupe mtawaweza? report ya CAG ni wizi mtupu ila mpaka November kujadiliwa bungeni ndio ujue hatupo serious kabisa kama nchi no wonder miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado nchi ni masikini..
Hizi mbwembwe za wanaharakati zinawapotezea wafanyabiahara wa kweli, fursa ya mabadiliko ya kimaendeleo yanayotaka kufanywa na DPW hapo bandarini.

Wizi ni sehemu ya DNA ya mtanzania hakuna report ya CAG isiyojaa madudu ya wizi kila sekta, lakini hauondoi umuhimu wa kuwekeza na kuleta teknolojia za kisasa hapo bandarini.

Ni vita ngumu kwani kukosekana kwa mifumo imara ya kisasa mahali pale ni fursa ya kudumu ya wapigaji kuweza kutengeneza pesa.

Sishangai kuona wanaopinga uwekezaji wakija na mada nzito za mpaka kutishia kuivunja Tanzania, maslahi yao maovu yanapoguswa wanapiga kelele kwa lugha zote wanazozijua lakini mwisho wao upo karibu sana.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa zenye maswali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kisha majibu utayatoa wewe mwenyewe!.

Angalizo.
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo!, hili ni bandiko la swali na sio bandiko la statement!. "Hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!". Swali ni Je Bunge letu nalo, lucha kushehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia, licha ya kuwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, nayo ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya ajabu hivi ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted or detected na ika sail through?!.

Umuhimu wa Angalizo
Umuhimu wa angalizo hili ni mimi mwenzenu huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuulizia jambo fulani, HAPA na HAPA Mhe. Mbunge kilaza mmoja, HAPA akaisoma makala yangu bila kuiona ile alama ya kuuliza na kunituhumu kuwa nimetoa statement fulani, akanishitaki kwa Spika, nikaitwa Dodoma kuhojiwa mbele ya kamati fulani!, HAPA nikaitika wito, nilipowaonyesha ile alama ya kuuliza, kesi ile iliishia pale!, hivyo sitaki tena kuandika kitu kisha nikaitwa kujieleza popote ndio maana natoa angalizo hili mapema kabisa, hapa sijatoa statement yoyote ni nimeuliza tuu maswali!.

Mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu bado umeshika kasi, huku ukijadiliwa kwenye fronts mbili kuu, front ya kwanza ni mijadala ya kisiasa, kwa wanasiasa mbalimbali kujitokeza kutoa hoja zao za kisiasa kwa kuita waandishi wa habari.

Front ya pili ni mijadala ya kisheria kwa wanasheria mbalimbali kujitokeza kutoa maoni yao ya kisheria, wakiongozwa na maoni ya Chama cha Wakili Tannganyika, TLS, wakiwemo wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama Prof. Issa Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, Jaji Sinde Warioba, Tundu Lissu na wanasheria mbalimbali

Wale wenye fedha zao, wataita waandishi ukumbi wa hoteli fulani na kuwakirimu waandishi wa habari, na wale wenzangu na mimi, akina Apeche Alolo, ama watawaita waandishi majumbani mwao, au kutoa maoni yao kupitia Club House.

Tangu sakata hili la IGA ya DPW liibuke, mimi msimamo wangu ni ule ule haujawahi kuyumba, kama tumeshindwa kuiendesha Bandari yetu kwa ufanisi, hivyo hakuna ubaya wowote kusaidiwa! HAPA

Nikasisitiza kitu kilichohitajika ni uelimishaji umma na ushirikishwaji wa Watanzania, mambo ambayo hayakufanyika watu wakaona tuu MoU zinasainiwa Dubai wakati wa Expo Dubai ile February 2022, IGA ikasainiwa kimya kimya October 2022, kisha kuletwa Bungeni kuridhiwa June 2023!. Hizi kelele za Watanzania kulalamikia IGA, mimi zikanishangaza HAPA

Juzi Ijumaa, Jukwaa la Wahariri wakawaalika wahusika wakuu wa IGA ile wakiongozwa na Waziri husika, akiandamana na wanasheria kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali, ndipo nami kwavile pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikashuhudia ukilaza wa ajabu kabisa kwenye tasnia yetu ya sheria!. Hii IGA imechambuliwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama TLS, Prof. Shivji, Prof. Anna Tibaijuka, Dr. Rugemeleza Nshala, na wengine wengi, ikakutwa ina matatizo lukuki, huku TLS wakiainisha kifungu kwa kifungu na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua, halafu wanatuletea wanasheria vilaza waliofeli LST, wala sio mawakili, kutuongozea timu za majadiliano ya hii IGA!, unategemea nini?!.

Wanasheria vilaza hawa wanapoibuka na kusema hii IGA ni safi, nzuri na haina matatizo yoyote!, hii ni kumaanisha, TLS na wanasheria manguli wote wanaosema hii IGA ni matatizo, ndio vilaza?!...kweli?!.

Mimi nami kama mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikatoa maoni yangu HAPA

Kule nyuma niliwahi kuuliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?, sasa ndio naanza kupata majibu, inawezekana kabisa Tanzania tuko hapa tulipo kwasababu ya wanasheria wa type hii, serikali yetu inaonekana ni serikali ya ajabu kwasababu ya wanasheria wa type hii!, na Bunge letu inaonekana ni Bunge la ajabu kwasababu ya wabunge wa type hii!.

Wakati wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar ile mwaka 1984, kulikomuondoa Abdul Jumbe aliyekuwa rais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Idris Abdul Wakil, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo!, aliwahi kusema, "Wanasheria ni watu wabaya sana" sikumbuki alimaliziaje, ila kwenye hilo sakata, aliyeshughulikiwa, sio rais wa Zanzibar pekee, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo, Wolfgang Dourado, pia alishughulikiwa kikamilifu!.

Wakati wa Bunge la Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, naye alileta za kuleta kule Dodoma, wakati wa upigaji kura kupitisha katiba pendekezwa. Sisi washauri wa bure tukashauri Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Kwenye hili sakata la IGA ya DPW, mimi naungana na Baba wa taifa kwa kusema "Wanasheria vilaza ni watu wabaya na hatari sana kwa taifa letu",

Ni wanasheria hawa ndio wametufikisha hapa kwenye hili la hii IGA ya DPW!, wanasheria ndio the source ya mikataba yote mibovu and in fact ni wanasheria ndio the source of katiba hii mbovu iliyopo ambayo licha ya kuwa ni katiba mbovu, pia imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili HAPA

Kwa hoja hizo, hakuna ubishi kuwa tuna wanasheria vilaza wa ajabu, swali sasa jee serikali yetu pia ni serikali ya ajabu?, na Bunge letu Tukufu pia ni Bunge la ajabu kupitisha mambo ya ajabu ajabu?.

Hitimisho
Nimalizie kwa wanasheria wetu na wanasheria wenzangu. Prof. Shivji anasema hii IGA ina matatizo, TLS wanaainisha kabisa vifungu, halafu wewe mwanasheria kinda, unaibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo, with all illegality nilio ainisha hapa, bado unathubutu kuibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo?.

Leo nimeandika makala kwenye gazeti la Nipashe, kwa kutoa rai kwa serikali, kuzijibu kisheria hoja za kisheria na tuufunge huu mjadala

Uzalendo wa kweli ni nia ya dhati kuisaidia nchi yako, kumsaidia rais wako, kuisaidia serikali yako, unapona jambo halijakaa vizuri, unakosoa na kushauri the right thing to do. Mimi nimekosoa na pia nimeshauri kuwa hata kama hii IGA ni tunabakwa, Mwanamke mgumba akibakwa, akapata ujauzito, atampenda mbakaji! Wajua Kuna Ndoa Halali, Batili na Batilifu?. Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji?. Wajua Ubakaji unaweza kuwa Halali?. IGA Batili Yaweza kuzaa HGA Halali?.
A Way Forward.
  1. First and foremost serikali ijibu kisheria hoja zote za kisheria zilizoibuliwa kupinga hii IGA, na sio kujibu hoja za kisheria kwa majibu ya kisiasa.
  2. Kwa vile hii sii mara ya kwanza, tumetunga sheria ipo halafu serikali yetu inatuletea mikataba kinyume cha sheria!, kama tumeona sheria hazifai, tuzibadili kwanza sheria ndipo tuingie mikataba.
  3. Kwa vile hii IGA imeisha sainiwa na kuridhiwa na Bunge letu, hii maana yake ni HGA inafuata. Nashauri hiyo HGA iwe as transparent as hii IGA ili tuone maoni ya wananchi yamejumuishwa.
  4. Imeelezwa itaundwa kampuni ya ubia na itasajiliwa Tanzania, kisha 35 shares zitakuwa floated for public. Hizo shares zikiuzwa kupitia soko la hisa, DSE, then watu wenye the purchasing power ni wale wale matajiri, nashauri hizo shares zihodhiwe na mifuko ya hifadhi za jamii ya NSSF na PSSSF, ili waitumie faida kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wote.
  5. Tubadili sheria zetu, mikataba yote ya rasilimali za taifa liidhinishe na Bunge na sio kuridhiwa tuu.
  6. Bunge letu libadilike, liache kuwa ni Bunge rubber stamp la kupitisha tuu kila kinachoitwa, mengine ni madudu kama hili dubwana!.
  7. Bunge letu liache kuwa ni Bunge kibogoyo lisilo na meno!. Maadam sheria imelipa Bunge the power to review, then Bunge litimize wajibu wake kikamilifu.
  8. Wanasheria, tuheshimiane, na kuheshimu professionalism na wanataaluma manguli wabobezi na wabobevu na kuheshimu maoni ya vyama vya kitaaluma, kama TLS, hii itazuia kuitana vilaza na mbululaz!.
  9. Kwangu mimi hii IGA ya DPW na Bandari yetu ni issue ndogo!, kuna ma issues makubwa, muhimu zaidi kama ubatili ndani ya katiba yetu unaonyima haki Watanzania, watu wako kimya!, halafu issue ndogo hii ya Bandari kelele mpaka karibu mbinguni!.
  10. Nimalizie kwa lile swali la msingi la bandiko hili kuwa hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!. Swali ni Je Bunge letu nalo pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted?!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Stop beating around the bush Pascal! Tatizo ni muhimili uliojichimbia chini
 
Pascal wewe hueleweki.
Mkuu Retired , kwanza naheshimu mawazo yako. Muda wa unielewa utakapo wadia, utanielewa.
Mimi huwa sikuamini! Ukiitwa kuteuliwa huwezi kuwa na msimamo......
Naheshimu mawazo yako
umesaka kuteuliwa muda mrefu.
Sijawahi kusaka kuteuliwa hata mara moja!. Msaka teuzi hawezi kuwa critical!.
Kama ukatili wa magufuli wooote uliuunga mkono, hupashwi kuaminiwa.
Sijawahi kuunga mkono ukatili wa aina yoyote!.
  1. Kwanza ile 2014 ni mimi ndio niliwaeleza humu kuwa Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli humo kuna kitu nililisema!.​
  2. Baada ya uchaguzi Mkuu kabla matokeo hayajatangazwa rasmi, nilisema Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!
  3. Ni mimi ndiye the one and only who dared ask such questions Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
Kuna popote nimeunga mkono?
SAWA NA DR SLAA, SIWEZI KUMWAMINI KATU! HANA ANALOLISIMAMIA NI TUMBO. ANAPIGA KELEL SASA AKIPEWA UBALOZI ANGEUKA , MSIMWAMINI
Naheshimu mawazo yako
P.
 
Umekengeuka! Ungelijua kabila langu ungekwenda kutubu kanisani! Au mnatubu kwa shetani wewe na Jiwe
Kuna makabila mapya kama lile la mafisadi, wapambe, vilaza nk. Maendeleo ya kiteknolojia na uchumi yanaondoa mipaka ya asili ya makabila
 
Kwa heshima kabisa, kuna.kitu tunakichanganya kwenye hii IGA ya DPW. Vitu hivyo ni muundo/viwango na maudhui. Nitaelezea.

Kwa ufupi sana;
Baada ya kuisoma na kuisoma tena hii IGA ya DPW binafsi nimegundua haina hiyo illegality inayoongewa na wengi w sisi wanasheria (mawakili) kwakuwa inafikia vigezo vyote vya mkataba kimuundo/kiviwango.

Sasa tatizo lilipo ni wapi?
Wengi wa wanasheria (mawakili) wanachanganya sana suala la yale waliyokubaliana pande mbili na misingi ya kisheria. Ukweli ni kuwa kwenye makubaliano yaani kile tulichokubaliana Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tulikosa watu wakuweza kubargain hii kitu kwa jicho la maslahi ya taifa yajayo.

Sijaeleweka;
Nitatoa mfano, ni sawa na kuwa gari linauzwa alafu mnunuzi amekuja na pesa milioni 10 lakini thamani halisi ni milioni 5 na akanunua kwa milioni 12. Halafu baadaye wakatokea ndugu na marafiki wakamwambia ule mkataba wa kuuziana gari una illegality kisa kauziwa gari la milioni 5 kwa milioni 12.

Ndicho kilichopo kwenye IGA ya DPW tulikosa watu wakupambania maslahi ya Taifa ndani ya makubaliano hayo. Na hili siwezi kutupa lawama kwa wanasheria wa serikali waliohusika bali lawama naweza kuzitupa kwa Bunge la Jamhuri pia.

Mimi ni hayo tu kwa sasa.
 
Mkuu Retired , kwanza naheshimu mawazo yako. Muda wa unielewa utakapo wadia, utanielewa.

Naheshimu mawazo yako

Sijawahi kusaka kuteuliwa hata mara moja!. Msaka teuzi hawezi kuwa critical!.

Sijawahi kuunga mkono ukatili wa aina yoyote!.
  1. Kwanza ile 2014 ni mimi ndio niliwaeleza humu kuwa Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli humo kuna kitu nililisema!.​
  2. Baada ya uchaguzi Mkuu kabla matokeo hayajatangazwa rasmi, nilisema Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!
  3. Ni mimi ndiye the one and only who dared ask such questions Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
Kuna popote nimeunga mkono?

Naheshimu mawazo yako
P.
Pasal wewe ni figure "kubwa". Umeandika muda mrefu na kujijengea jina kubwa.

Nikueleza ukweli...umekuja kukengeuka wakati wa Magufuli na ulipoitwa na bunge. Ulitishwa na ukatishika na kugeuka nyuma ukawa Jiwe. Afadhali ungelinyamaza kuliko kukengeuka na kubadili msimamo!
Mama Tanzania Mbatia, baada ya kunyanganywa chama na Mutungi, amekaa kimya lakini hakukengeuka!

Finally, we angalia wanavyokuandika hapa JF, kila mmoja anasema you were smart huko nyuma, not today
Nakukumbuka sana toka nyuma ulipokuwa MC pale Peakcock Hotel harusi ya akina Malinzi! I was there!
 
Back
Top Bottom