Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa zenye maswali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, kisha majibu utayatoa wewe mwenyewe!.
Angalizo.
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo!, hili ni bandiko la swali na sio bandiko la statement!. "Hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!". Swali ni Je Bunge letu nalo, lucha kushehenezwa na wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia, licha ya kuwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, nayo ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya ajabu hivi ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted or detected na ika sail through?!.
Umuhimu wa Angalizo
Umuhimu wa angalizo hili ni mimi mwenzenu huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuulizia jambo fulani,
HAPA na
HAPA Mhe. Mbunge kilaza mmoja,
HAPA akaisoma makala yangu bila kuiona ile alama ya kuuliza na kunituhumu kuwa nimetoa statement fulani, akanishitaki kwa Spika, nikaitwa Dodoma kuhojiwa mbele ya kamati fulani!,
HAPA nikaitika wito, nilipowaonyesha ile alama ya kuuliza, kesi ile iliishia pale!, hivyo sitaki tena kuandika kitu kisha nikaitwa kujieleza popote ndio maana natoa angalizo hili mapema kabisa, hapa sijatoa statement yoyote ni nimeuliza tuu maswali!.
Mjadala wa IGA ya DPW na Bandari zetu bado umeshika kasi, huku ukijadiliwa kwenye fronts mbili kuu, front ya kwanza ni mijadala ya kisiasa, kwa wanasiasa mbalimbali kujitokeza kutoa hoja zao za kisiasa kwa kuita waandishi wa habari.
Front ya pili ni mijadala ya kisheria kwa wanasheria mbalimbali kujitokeza kutoa maoni yao ya kisheria, wakiongozwa na maoni ya Chama cha Wakili Tannganyika, TLS, wakiwemo wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama Prof. Issa Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, Jaji Sinde Warioba, Tundu Lissu na wanasheria mbalimbali
Wale wenye fedha zao, wataita waandishi ukumbi wa hoteli fulani na kuwakirimu waandishi wa habari, na wale wenzangu na mimi, akina Apeche Alolo, ama watawaita waandishi majumbani mwao, au kutoa maoni yao kupitia Club House.
Tangu sakata hili la IGA ya DPW liibuke, mimi msimamo wangu ni ule ule haujawahi kuyumba, kama tumeshindwa kuiendesha Bandari yetu kwa ufanisi, hivyo hakuna ubaya wowote kusaidiwa!
HAPA
Nikasisitiza kitu kilichohitajika ni uelimishaji umma na ushirikishwaji wa Watanzania, mambo ambayo hayakufanyika watu wakaona tuu MoU zinasainiwa Dubai wakati wa Expo Dubai ile February 2022, IGA ikasainiwa kimya kimya October 2022, kisha kuletwa Bungeni kuridhiwa June 2023!. Hizi kelele za Watanzania kulalamikia IGA, mimi zikanishangaza
HAPA
Juzi Ijumaa, Jukwaa la Wahariri wakawaalika wahusika wakuu wa IGA ile wakiongozwa na Waziri husika, akiandamana na wanasheria kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali, ndipo nami kwavile pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikashuhudia ukilaza wa ajabu kabisa kwenye tasnia yetu ya sheria!. Hii IGA imechambuliwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu kama TLS, na Prof. Shivji, Dr. Rugemeleza Nshala, ikakutwa ina matatizo lukuki, halafu wanatuletea wanasheria vilaza tuu waliofeli LST, wala sio mawakili, kutuongozea timu za majadiliano ya hii IGA!, unatemea nini?. Wanasheria vilaza hawa wanapoibuka na kusema hii IGA ni safi, nzuri na haina matatizo yoyote!, hii no kuashiria TLS na wanasheria manguli wote wanaosema hii IGA ni matatizo, ndio vilaza?!...kweli?!. Mimi nami kama mwanasheria na wakili wa kujitegemea, nikatoa maoni yangu
HAPA
Kule nyuma niliwahi kuuliza
Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?, sasa ndio naanza kupata majibu, inawezekana kabisa Tanzania tuko hapa tulipo kwasababu ya wanasheria wa type hii, serikali yetu inaonekana ni serikali ya ajabu kwasababu ya wanasheria wa type hii!, na Bunge letu inaonekana ni Bunge la ajabu kwasababu ya wabunge wa type hii!.
Wakati wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar ile mwaka 1984, kulikomuondoa Abdul Jumbe aliyekuwa rais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na Idris Abdul Wakili, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema, "Wanasheria ni watu wabaya sana" sikumbuki alimaliziaje, ila kwenye hili sakata la IGA ya DPW, mimi naungana na Baba wa taifa kwa kusema "Wanasheria Vilaza ni Watu Wabaya Sana", ndio wametufikisha hapa kwenye hili la hii IGA ya DPW!, ndio source ya mikataba yote mibovu and in fact ndio the source of katiba hii mbovu iliyopo ambayo licha ya kuwa ni katiba mbovu, pia imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili
HAPA
Hitimisho
Nimalizie kwa wanasheria wetu na wanasheria wenzangu. Prof. Shivji anasema hii IGA ina matatizo, TLS wanaainisha kabisa vifungu, halafu wewe mwanasheria kinda, unaibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo, with all illegality nilio ainisha hapa, bado unathubutu kuibuka na kusema hii IGA ni safi na haina matatizo?.
Leo nimeandika makala kwenye gazeti la Nipashe, kwa kutoa rai kwa serikali, kuzijibu kisheria hoja za kisheria na tuufunge huu mjadala
Uzalendo wa kweli ni nia ya dhati kuisaidia nchi yako, kumsaidia rais wako, kuisaidia serikali yako, unapona jambo halijakaa vizuri, unakosoa na kushauri the right thing to do. Mimi nimekosoa na pia nimeshauri kuwa hata kama hii IGA ni tunabakwa, Mwanamke mgumba akibakwa, akapata ujauzito, atampenda mbakaji!
Wajua Kuna Ndoa Halali, Batili na Batilifu?. Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji?. Wajua Ubakaji unaweza kuwa Halali?. IGA Batili Yaweza kuzaa HGA Halali?.
Nimalizie kwa lile swali la msingi la bandiko hili kuwa hii IGA ya DPW imetusaidia sana Watanzania kujitambua!, kumbe tuna wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu wa kutosha!, lakini at the same time, pia tuna wanasheria vilaza wa ajabu sana!. Swali ni Je Bunge letu nalo pia ni Bunge la ajabu? na Serikali yetu pia ni Serikali ya Ajabu?, hii IGA ya DPW ilipita pita vipi kote huko ikiwa na vipengele so defective bila kuwa noted?!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.