IGP Komesha wauaji ya raia au hadi samia aseme na wewe?

IGP Komesha wauaji ya raia au hadi samia aseme na wewe?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetangaza ‘dau’ la Sh1.5 milioni kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya Juliana Lukono (51) aliyeuawa na wasiojulikana wilayani Magu.

Mauaji ya mwanamke huyo yanadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo Mei 12, 2023 alipokuwa akiishi katika Kijiji cha Bugumangala Kata ya Nyanguge baada ya majirani kukuta mwili wake umetupwa kwenye shamba la mihongo lililopo karibu na mahali alikokuwa akiishi.

Mtoto wa dada wa marehemu, Salome Faustine amesema baada ya kupigiwa simu na majirani, alifika eneo hilo na kukuta mwili wa mama yake mdogo ukiwa umetelekezwa katika shamba la mihogo huku ukiwa ametapakaa damu.

"Baada ya kupewa taarifa nilikimbia kufika hapa, nikakuta mwili wa mama umelala hapo shambani huku ukiwa umetapakaa damu," amesema Salome

Aidha, Diwani wa Kata ya Nyanguge wilayani Magu mkoani hapa, Hilali Elisha amesema bado chanzo cha mauaji ya mwanamke huyo hakijajulikana kwani hajawahi kupokea taarifa ya kuwepo ugomvi wala migogoro katika familia ya marehemu.

“Ifike wakati tujitafakari haiwezekani mtu unafikia kumuua binadamu mwenzako hatuwezi kujua ni mpenzi wake au nani maana kwa hali ya kawaida hakuna faida ya kumuua mtu na kuacha ndugu wanateseka,” amesema Elisha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilboard Mutafungwa amefika eneo hilo na kutoa ofa kwa mtu mwenye taarifa zitakazosaidia kuwakamata wahusika atapatiwa Sh1.5 milioni.

“Hili tukio liwe la mwisho lazima atajwe aliyehusika, lazima kinamama wawe na usalama katika mambo yao, faragha zao na mambo mengine hatuwezi kuendelea kuvumilia watu wachache wanaojichukulia sheria mkononi,” amesema Mutafungwa.
 
 
Back
Top Bottom