IGP Mahita: Said Mwema alipewa u-IGP kwa figisu

Huu ni uongo mtupu, magari zaidi ya 20 nyumbani kwake hio imekua yard ya magari ?? Unataka kumsafisha Kikwete tu, ila ukweli utabaki serikali yake ilikua ya kishkaji sana ndio mwanzo wa kuanguka maadili kwa nchi yalipoanzia.
 
Luckily Kikwete alikuwa Mkwere majority ya watu wa Pwani hawakuwa Wameenda Shule ivo Serikali ilijaa watu wa maeneo mbalimbali kwenye top posts just imagine angekuwa Msukuma au Mchaga
 
Said Mwema alioa mwanamke (sasa marehemu, RIP) ambaye alikuwa anamuita Kikwete mjomba nafikiri. I know the family closely.

Hivyo ni kweli Said Mwema alioa kwenye ukoo wa kina Kikwete.

Lakini pia, Said Mwema alikuwa na sifa zote za kuwa IGP. Tena si za ndani ya Tanzania tu, Said Mwema alifanya kazi mpaka Interpol, Interpol ni taasisi ya Polisi ya dunia nzima.

Kwa hivyo, hata kama Mwema alioa kwa Kikwete, alipoteuliwa kuwa IGP alikuwa na uzoefu mkubwa sana kuliko wengine na alifaa kuteuliwa kuwa IGP.

Na hata watu wanaoifuatilia Polisi ya Tanzania watakubali kuwa Said Mwema alipeleka jeshi kiweledi sana kulinganisha na ma IGP wengine. Alifanya reforms kubwa sana. Aliingiza mambo mengi ya kwenda na teknolojia ya kisasa huko Polisi.

Mimi sipendi nepotism, mimi sipendi kupeana kazi kwa kujuana.

Lakini, ikiwa mimi ni rais, na kuna mtu ambaye alitokea kuoa kwenye ukoo wangu huko nyuma miaka mingi kabla hata sijawa rais, na mtu huyo ni Polisi, na ndiye mwenye sifa kubwa kabisa za kuwa IGP, niache kumteua IGP kwa sababu tu alioa kwenye ukoo wangu huko?

Hapana, nitamteua, si kwa sababu ni ndugu yangu katika kuoa kiukoo huko, bali kwa sababu ni mtu mwenye qualifications nzuri kabisa.

Siwezi kumlaumu Kikwete kwa kumteua Said Mwema kuwa IGP. Angalau tunajua kuwa Said Mwema hajateuliwa kuwa IGP kwa sababu ya kuwapiga wapinzani kama Omar Mahita, aliteuliwa kwa credentials zake za Polisi Tanzania mpaka Interpol.
 
Alikuwa mwadui mine pale
Kulikua na police post
Wakati huo hadi wakina Stephen mashinganga nk walikuwa hapo mwadui mine,hyo longtime mzee
Wazee wamekaa huko na kupiga kazi

Ova
 
Huu ni uongo mtupu, magari zaidi ya 20 nyumbani kwake hio imekua yard ya magari ?? Unataka kumsafisha Kikwete tu, ila ukweli utabaki serikali yake ilikua ya kishkaji sana ndio mwanzo wa kuanguka maadili kwa nchi yalipoanzia.
Wewe bwege unabishana na ukweli au Mahita baba yako??
 
Hivi IGP wa sasa anaitwa nani?? mbona amepwaya sana. Au ndio huyo anaesikika sana akiitwa Muliro.?
 
Sema mzee nimempenda, kanyooka kama ruler.
Amesema kabisa matumizi ya risasi za moto kwa raia hapana, ni kuwapiga mabomu ya kuwapiga risasi za rubber, wataanguka huko n.k
Kule Pemba walitumia risasi gani wakati akiwa IGP 2001?
 

kwangu kitu pekee positive kwa Kikwete kilikuwa ni hicho alikuwa na uwezo ( sasa sijui kama ni yeye ndiye aliyeibua watu wenye cv nzito lkn alikuwa ni raisi) kuteua vichwa au watu waliobobea kwenye fani zao sio Saidi Mwema tu, alimteua yule mwingine nimesahahu jina lake wizara ya madini ambaye pia ni geologist mwenye cv nzuri, alimleta mama Tibaiijuka wizara ya ardhi ambapo Tibaijuka alikuwa na cv iliyoshiba pia sana kwenye mambo ya ardhi na wengine wengi tu kwenye taasisi mbali mbali kuna yule wa uwekeaji alimtoa south afrika nafikiri i mean, alikuwa anateua experts ambao walibobea kwenye fani zao sana, hata Magufuli mwenyewe pamoja na mapungufu yake lkn aliiweeza na kuimudu wizara ya ujenzi vizuri tu.

ndiyo maana kwangu its really confusing kinachoendelea sasa hivi kwani kama wanavyosema kwamba ana power na influence kubwa kiihivyo kwenye current regime mbona sasa hsaidii kuteua watu ambao yeye akiwa raisi aliwaleta? iweje sasa kuna wizara zimejaa watu wasio na uwezo kabisa wakati mwingine siamini kama kweli ana power kiihivyo angalia wanaoongoza afya, wizara ya elimu mpaka naibu atleast, ujenzi i mean, hakuna wizara 1 inayoongozwa vizuri wakati zamani wizara hata zilikuwa ndiyo mahali ambapo viongozi walipotokea tuliona kazi za waziri xyz na kuona huyu anatufaa hata kuwa raisi leo hii hakuna hata waziri mmoja ambaye unaweza kusema huyu labda anafaa kuwa rasisi kwa utendeaji wake so what happened? kwa maana wakati wa uraisi wake alikuwa na watu wazuri sana hata yule Gavana wa bot nafikiri alishafariki alikuwa pia na cv iliyoshiba, linganisha waziri mkuu wake Pinda na huyu wa leo.

hata mambo ya islamism Kikwete aliwakatalia islamist kadhi court ( sina infos zote labda namsifia bure tu wanaojua zaidi watasema ) kwa kusema kwamba tanzagiza ni secular, mambo ya islamism yanayoendelea leo hii aliyapinga kwenye uraisi wake, its confusing ...
 
Si huwa mnasema kwamba mstaafu akianza kuchomoa betri ujue amenyimwa fursa yeye au kizazi chake. Sasa huyu huwa ana mjukuu wake ni afisa wa polisi alisikika sana kwenye kesi ya Mbowe. Chunguzeni labda mzee anataka mjukuu wake apewe fursa mfano RPC lakini system inagoma
 
Kilichotokea Tanzania ni a very slow and gradual decline in the culture of grooming and preparing people for leadership. With the advent of multiparty, especially the Samia era, uchawa unakuwa na nguvu kuliko uwezo.

Watu wenye uwezo wanashindwa kwenda kichawachawa, wanashaurishauri sana, wanakosoakosoa sana. Mtawala dikteta hataki kukosolewa. Wenye uwezo hawatoboi.

Tatizo tunamuangalia Kikwete alivyomteua Tibaijuka tu. Lakini mpaka Kikwete anamteua Tibaijuka, Tibaijuka alishakuwa na PhD na kufanya kazi UN Habitat. Sasa Tibaijuka alipita vipi mpaka kupata PhD na kufanya kazi UN?

Kulikuwa na watu wameandaliwa tangu awali. Ndio hao kina Dr. Salim Ahmed Salim, kina Dr. Augustine Mahiga, Dr. Anne Tibaijuka, etc.

Serikali ilikuwa ina groom watu. Mpaka huyu Makamu wa Rais Nchimbi alikuwa na degree moja ya Mzumbe nafikiri, Mkapa akamuona akasema wewe utakuja kuwa kiongozi miaka ijayo degree moja haikutoshi ongeza kisomo. Akasomasoma leo Dr.

Sasa huu utamaduni ulikuwapo sana enzi za Nyerere, Mwinyi, mpaka Mkapa.

Ukaanza kufifia, watu wakawa wanateuliwa kwa uchawa zaidi ya merit. Magufuli alijaribu pia ila yeye alikomba sana academics.

Sasa miaka ilivyosogea mbele, hata baada ya wasomi kuongezeka, teuzi zikafanywa kwa kujuana na kuwa loyalist zaidi. Wenye uwezo wakashindwa katika ligi ya uchawa.

Madikteta hawataki watu competent. Wanataka watu loyal.

Ndiyo maana leo unaona tuna Waziri wa Mambo ya Nje hata Kiingereza hajui. Anasema atawalipia ma Seneta wa Marekani waje Tanzania kuangalia hali, hajui kwamba hiyo kauli tu ni faux pas, ni kosa la kidiplomasia, Seneta wa Kinarekani ukimlipia gharama aje Tanzania ni kama umemuhonga, sheria za Marekani haziruhusu, utamaduni wa Marekani hauruhusu.

Huyu waziri kapewa kazi kwa sababu ni loyalist wa Samia, si kwa sababu ana uwezo mkubwa.
 
Sahivi akili ndogo zinawaongoza watu wenye akili kubwa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…