Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ni jambo ambalo linazidi kuenea Tanzania. Mara nyingi unakuta askari polisi wanatumwa kwenye tukio linalohitaji silaha (japo ni machache Tanzania) huku wakiwa wamesheheni silaha na bado wamevaa kiraia. Kwa nini wanafanya hivyo? Je inaruhusiwa kwa askari polisi aliye kwenye response unit kwenda akiwa na silaha kamili za kuingia filed lakini akawa amevaa kiraia?
Nimeangalia askari walioenda kumkamata huyu mama wa Iringa alietoroka kambi ya Corona, na karibu askari wote walioenda walikuwa wamesheheni silaha lakini wamevaa kiraia.
Halafu, hili tukio si la ujambazi. Kwa nini Polisi wapeleke kikosi chenye uzito wa silaha kiasi hiki kumkamata mwanamke mmoja aliekimbia kambi ya Corona? Hivi polisi wetu wanawashwa kubeba silaha na kuzitumia?
Nchi haiko vitani, unapeleka kikosi cha polisi kumkamata mwanamke mmoja aliyetoroka kambi ya Corona utafikiri unaenda kumkamata kiongozi wa Al-Qaeda, Unataka kumtisha nani na askari wako na silaha zao, wananchi wa Tanzania?
Unapeleka askari na silaha kwenye tukio dogo kama hili utafikiri huyo mwanamke ndio Corona yenyewe unaenda kuikamata! Mkitukanwa mnatumia nguvu badala ya busara mnalalamika. Hii display ya force kwenye tukio kama hili inawasaidia nini hasa? Polisi badilikeni. Mnatuaibisha.
Siku moja askari wako wenye silaha na wamevaa kiraia watakuja kuuwawa wakidhaniwa ni majambazi.