IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia?

IGP Simon Sirro, kwanini askari polisi wanatumwa field na silaha nzito wamevaa kiraia? Kwanini unatuma askari na silaha nyingi tukio dogo la kiraia?

Wewe nini wasi wasi wako, ikiwa hizo silaha mzito hupigwi nazo. Ni vizuri ungetuwekea taratibu za operation za polisi hapa, tuone kama wanakosea au la.

Na kama wanavunja katiba ya nchi, weka hapa hiyo aya, inaoelezea operation za polisi wanatakiwa waweje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hizo silaha, tatizo nini kwa mtu mwema. mnataka waende mikono mitupu, alafu mtu mwenye kisu, au bastola awakimbize.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama askari wa upelelzi, unajua kwa nini hawavai uniform? Tuanzie hapo kwanza. Kama una akili hata kidogo basi utaona jinsi gani huna ufahamu.
 
Unitorm hazitoshi, wanasuhiri Rais awambie wanujue kama alivyo fanya shule ya ubungo
Ni jambo ambalo linazidi kuenea Tanzania. Mara nyingi unakuta askari polisi wanatumwa kwenye tukio linalohitaji silaha (japo ni machache Tanzania) huku wakiwa wamesheheni silaha na bado wamevaa kiraia. Kwa nini wanafanya hivyo? Je inaruhusiwa kwa askari polisi aliye kwenye response unit kwenda akiwa na silaha kamili za kuingia filed lakini akawa amevaa kiraia?

Nimeangalia askari walioenda kumkamata huyu mama wa Iringa alietoroka kambi ya Corona, na karibu askari wote walioenda walikuwa wamesheheni silaha lakini wamevaa kiraia.

Halafu, hili tukio si la ujambazi. Kwa nini Polisi wapeleke kikosi chenye uzito wa silaha kiasi hiki kumkamata mwanamke mmoja aliekimbia kambi ya Corona? Hivi polisi wetu wanawashwa kubeba silaha na kuzitumia?

Nchi haiko vitani, unapeleka kikosi cha polisi kumkamata mwanamke mmoja aliyetoroka kambi ya Corona utafikiri unaenda kumkamata kiongozi wa Al-Qaeda, Unataka kumtisha nani na askari wako na silaha zao, wananchi wa Tanzania?

Unapeleka askari na silaha kwenye tukio dogo kama hili utafikiri huyo mwanamke ndio Corona yenyewe unaenda kuikamata! Mkitukanwa mnatumia nguvu badala ya busara mnalalamika. Hii display ya force kwenye tukio kama hili inawasaidia nini hasa? Polisi badilikeni. Mnatuaibisha.

Siku moja askari wako wenye silaha na wamevaa kiraia watakuja kuuwawa wakidhaniwa ni majambazi.

View attachment 1407862

View attachment 1407865
 
Nimeangalia askari walioenda kumkamata huyu mama wa Iringa alietoroka kambi ya Corona, na karibu askari wote walioenda walikuwa wamesheheni silaha lakini wamevaa kiraia.
Kachero havai sare
Anti robbery unit hawavai sare
Inategemea response imedakwa na kitengo gani,na hawawezi kwenda kwenye tukio bila silaha,ni sawa na gari la zimamoto kufika kwenye tukio bila maji
Tanzania ya sasa,hasa Dar,ukiona polisi alievaa sare amebeba silaha,basi ujue kwamba anaenda kulinda benki au amepangwa kwenye mataa ya kuongoza gari
 
Anti-robbery kwenda kumkamata mama aliyetoroka hospitali kwa ajili ya Corona? Au tuwatafsirie polisi wetu maana ya anti-robbery?
 
Kachero havai sare
Anti robbery unit hawavai sare
Inategemea response imedakwa na kitengo gani,na hawawezi kwenda kwenye tukio bila silaha,ni sawa na gari la zimamoto kufika kwenye tukio bila maji
Tanzania ya sasa,hasa Dar,ukiona polisi alievaa sare amebeba silaha,basi ujue kwamba anaenda kulinda benki au amepangwa kwenye mataa ya kuongoza gari
Kwa hiyo wanaenda na mabunduki kuishambulia Corona??
 
Tatizo labda iwe hizo silaha ila sio nguo.
Hao askari wa idara ya upepelezi, ambao kimajukumu hawavai uniform.
Gafla wakikutana na tukio njian ambalo linahitaji kutumia silaha lets say gafla wakakuta majambazi wanaganya tukio....polisi waanze kutumia fimbo au mawe??
 
Back
Top Bottom