IGP Simon Sirro; madaraka hupita, toba hutengeneza mwisho mwema

IGP Simon Sirro; madaraka hupita, toba hutengeneza mwisho mwema

Sina zaidi ya hilo nililokiambia my dear. Ila tu Mungu hadhihakiwi. Usichukulie uovu/dhambi ya mtu mwingine kuwa kisingizio cha wewe kuhukumu au kuunga mkono uovu.
Kumbuka tunakosea kwa kuwaza, kwa kunena kwakutenda na hata kwakutokutimiza wajibu. Basi chukua wajibu wako kama huwezi bora ukae kimya.

Wapi nilipounga mkono au kuhukumu. Hivi unajua kusoma na kuelewa kweli wewe au ni ushabiki unakusumbua!?

Mpigie simu Tundu aje hili neno liishe.... mbona alikuja kwenye kampeni!?

Asipokuja anatufikirisha zaidi
 
Nadhani ipo nafasi ukitika katika utumishi unachobaki nacho ni kama binadamu mwenye imani kwamba Mungu yupo nikumshukuru Mungu nakuendelea kumtukuza kwa uhai na madaraka uliyopewa.

Ukipewa madaraka, ukapewa maarifa ya mema na mabaya, ukapewa maarifa ya kujua pumzi si mali itokayo kwa mwanadamu bali kwa Mungu, basi utaheshimu kila nafsi ulilokabidhiwa kuilinda.

Nimemsikiliza mzee Sirro kauli yake dhidi ya Lissu, nimeumia kwamba uhai wa mwanadamu umepewa nafasi ndogo kuliko mshahara na ulinzi wa smg. Natamani viongozi waache kuona mshahara, waone Taifa na kuwaona binadamu.

Hiki alichokitamka huyu mzee kwa umri wake na kwa kutoshurutishwa na mtu naamini hakitoishi masikioni mwake. Ametenda kosa ambalo linawanufaisha wanasiasa lakini linachipa na kuimomonyoa nafsi yake hasa pale anapokuwa kwenye binafsi na ambayo anakwenda kuyaanza hivi karibuni.

Nimeumia kwa aina hii ya viongozi.
Kwa majibu ya Siro tumwachie Mungu aamue kama kweli Siro hajui chochote kuhusu kutaka kutoa robo ya binadamu mwezake
 
Wapi nilipounga mkono au kuhukumu. Hivi unajua kusoma na kuelewa kweli wewe au ni ushabiki unakusumbua!?

Mpigie simu Tundu aje hili neno liishe.... mbona alikuja kwenye kampeni!?

Asipokuja anatufikirisha zaidi
Mama D hakuna haja ya kuendeleza ubishi. Umesema mwenyewe kuwa "Mama alipokuwa makamu wa Rais alisema askari wa Tanzania hawezi mpiga mtu risasi tatu akamkosa" kwa tafsiri hii unaungana na Sirro kuwa Lissu alijipiga risasi mwenyewe/ watu wake walimpiga risasi kutafuka "kiki". Sikatai hilo ila "Mungu hadhihakiwi"
 
Kama bado Sirro hajatubu kwa ile kauli basi analo. Hadi natamani Lissu akubali uteuzi wa Mama Samia na awe waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Maana nasikia mama yupo tayari kumpa cheo chochote Lissu ili wajenge nchi kwa pamoja
Thubutu
 
Mama aliongea kama serikali wewe unampinga kwa uthubitisho gani???

Sirro nae kaongea kama serikali akimaanisha kama muathirika hatoi ushirikiano kwa vyombo husika inaleta maswali na majibu mengine.

Kuongea mitandaoni haina tija wala afya kwa Tundu mwenyewe, kwetu wala taifa.

Yeye aje tuwajue washika mtutu waliohusika kumpiga risasi
 
Kuna siku atajutia hii kauli,naona hajifunzi kwa yaliyomkuta Boss wake,dunia hii ina kanuni zake

Kwani boss wake yalimkuta yepi!??

Kufariki ni adhabu!??

Huna wazazi, ndugu, au jamaa waliofariki!?? Kwani hio ni adhabu kwao au ww mwenzetu na Jamii yako mmeandikwa kuishi milele

Acheni akili za kipuuzi kama mmenyofolewa ubongo bana
 
Watu wanadhani kufa ni adhabu
Wakati kiuhalisia kufa ni lazima na kiimani kufa ni kumaliza kazi za ulimwengu huu
 
"Lissu anatumia kilema alichonacho kupata fadhila za wazungu".

HII KAULI, KAULI HII! Haitakuacha salama Sirro. Iwe Leo duniani au kesho ahera, hutakuwa salama kwa kukejeli kilema cha mwenzio kilichosababishwa na watu unaowajua.

Yaani Lissu afurahie kuwa kilema kuliko kuwa mzima? Kwahiyo unaungana na kina Musiba walioitisha press conference na kusema Lissu hakupigwa risasi za moto bali risasi baridi (blanks)? Na wewe unatuletea jambo jipya kwamba Lissu yuko kwenye hali hiyo kwa kupenda kwake?

Yaani amefanyiwa operesheni zaidi ya 20 mwilini mwake ili tu apate ufadhili?

KWAMBA; Amukuwa tayari kuishi akitobolewa mwili, kuvunjwa mifupa na kuwekewa vyuma ili apate kufadhiliwa na Wazungu?

SIRRO! Tema mate chini braza, wewe ni Mkristo Mkatoliki si mpagani. Kumbuka ukuu wa Mungu na maelekezo yake kwa watu wake kuhusu huruma na upendo.

UNAJIMALIZA KIIMANI NA KIBINADAMU.
Mkuu, comment yako inaumiza sana kwa wenye mioyo yenye hofu ya Mungu. Nimejisikia kutoendelea kusoma comments zingine, maana naona hii kama imemaliza kila kitu kuhusu huyu Sirro. Tuombe uhai tuweze kumuona akiishi maisha yenye furaha.
 
Zombe anaishi maisha gani siku hizi?
 
Hukumu ya Mungu inamsubiri kwa udhalimu alioufumbia/alioshiriki kwa nafasi yake.

Mungu hadhihakiwi.
Nyinyi mnafikiri Mungu ana Pokea rushwa? Maana haya mnayo andika mnajaribu kumpa Mungu rushwa ya sifa! - "hukumu ya Mungu inamsubiri, Mungu hadhihakiwi etc". Mungu hasikilizi na kutenda kwa utashi wenu. Na hivi, nani aliwaambia Mungu yupo upande wa watu wanaopinga serikali tu?
 
Kwani boss wake yalimkuta yepi!??

Kufariki ni adhabu!??

Huna wazazi, ndugu, au jamaa waliofariki!?? Kwani hio ni adhabu kwao au ww mwenzetu na Jamii yako mmeandikwa kuishi milele

Acheni akili za kipuuzi kama mmenyofolewa ubongo bana
Umeniuliza maswali hapo juu,halafu ukajijibu mwenyewe,halafu ukatoa hitimisho.

Sasa kati ya Mimi na wewe nani aliyenyofolewa ubongo?
 
Kama bado Sirro hajatubu kwa ile kauli basi analo. Hadi natamani Lissu akubali uteuzi wa Mama Samia na awe waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Maana nasikia mama yupo tayari kumpa cheo chochote Lissu ili wajenge nchi kwa pamoja
We can't bargain with the devils to build our nation.. yule ni msaliti akapewe cheo huko huko Ubelgiji
 
Back
Top Bottom