IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

Hivi mnafikiri wankyo kakosea!!!?hapana anajua asemacho ni suala la muda tu atakuwa IGP!!

Mama kamrudisha makao makuu ILI awe IGP!!!

Ngojeni nione!!
 
Huyo Wankyo kifupi anaonyesha alikuwa hataki uhamisho kwa nini yeye ndie anajua.

Anaonyesha wazi kuwa alikuwa haivi na IGP kwa nini yeye ndie anajua
Lakini ni kama mtu kaamua kuwa sihami Pwani
Pwani TAMU Sana mkuu..

Hususani kibaha.

Pwani pana hela sanaaaaa
 
Tatizo ni RPC kufanya comedi kwenye tafrija zenye raia.

Msameheni bure konyagi ilipaa mkichwa au hakuandika text ya hotuba yake
 
Taarifa zilizopo ni kwamba RPC KAGERA ambaye ametoka Pwani na kupelekwa mkoa Kagera ndugu Wankyo nadhani kauli ya jana ya kuhitaji ukuu wa Jeshi la Polisi imemuungiza matatani hii imeonesha hana nidhamu ya hali ya juu ndani ya jeshi hivyo basi staff officer aliyepo mkoa wa Rukwa ameteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera na Wankyo amepelekwa makao makuu ya jeshi mkoani DODOMA ambapo ni mji mkuu wa tanzania.

Ikumbukwe kuwa kauli aliyotoa jana kiutendaji ndani ya jeshi la polisi huku akijuwa mkuu wake wa kazi yupo na anafanya kazi hakustahili kusema kuwa mkuu wake wa kazi anafanya kazi ila yeye akipewa ukuu wa jeshi anaweza kufanya vizuri zaidi hii imeonesha kuwa nafasi aliyeteuliwa na amri jeshi mkuu hatoshi kuliongoza jeshi hivyo basi kwa kuwa jeshi huongozwa kwa nidhamu ya hali ya juu ndiyo maana mabadiliko hayo yamefanyika ili akae makao makuu ajifunze nidhamu pamoja na kuandika vipeperushi mabalimbali vinavyolihusu jeshi la polisi.

Pia soma: Wankyo Nyigesa RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

 
Sirro hastahili hiyo heshima kutokana na ukweli unaoufahamu
Wewe kwasababu uko too politicalised siwezi kubishana na wewe! Jeshi lina mistari yake. Huyo RPC Inawezekana kadanganywa na wanasiasa kama ninyi!

It's totally completely wrong kijeshi! Huyo anaweza kushughulikiwa hata na jeshi la ulinzi ili awe na adabu na awe mfano! Mkikosa adabu jeshini nchi inaondoka dogo!
 
Hivi mnafikiri wankyo kakosea!!!?hapana anajua asemacho ni suala la muda tu atakuwa IGP!!Mama kamrudisha makao makuu ILI awe IGP!!!Ngojeni nione!!
Kama ni hivyo hapo planners ni zero.

Undispline plan na hapo hata ukifanya ubabe wanajua namna ya kukutia adabu!

Hii ni nchi sio familia [emoji2955]
 
Huyu afande ana akili nyingi Sana, hakutaka kwenda Kagera. Alijua akim- provoc Mkuu wake, obviously atapelekwa makao makuu. Pale ndo atajijenga na Kisha ndoto zake zitatimia.

Hivi mnapajua Kagera?! Waache waende hao waliotoka Rukwa labda watapata nafuu.

Mawazo binafsi.
Kama u IGP ungekuwa na mipango hii nchi ingeshakuwa Congo. Hatuna nchi ya ovyo kwa kiwango hicho. Hiyo mipango ni kwenye mamlaka za kiraia sio kwenye majeshi na hasa top position kama hii.

IGP ni senior next to CDF! Hapo hata wapikaji wakipika chakula hakitoiva. Hii ni nchi, tena Tanzania [emoji1241]. Huyo RPC kapotoka tu maneno mazito mno!
 
Huyu afande ana akili nyingi Sana, hakutaka kwenda Kagera. Alijua akim- provoc Mkuu wake, obviously atapelekwa makao makuu. Pale ndo atajijenga na Kisha ndoto zake zitatimia.

Hivi mnapajua Kagera?! Waache waende hao waliotoka Rukwa labda watapata nafuu.

Mawazo binafsi.
Kuna nini mkuu huko Kagera?
 
Back
Top Bottom