IGP Sirro, amewaomba viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya kukaa kimya

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Posts
9,213
Reaction score
14,925
Ametoa ombi hilo leo Agosti 22, 2020 akiwa anaongea na viongozi wa dini visiwani Zanzibar, kuhusuiana na suala la amani, katika kipindi chote cha uchaguzi ambapo amesema viongozi wa dini ni moja ya wadau wa amani nchini.

"Niwaombe sana kwasababu mnasikia baadhi ya maneno yanayotamkwa na baadhi ya wanasiasa lakini mmekaa kimya hamsemi, mmekaa kimya hamkosoi, mmekaa kimya mekuwa woga niwaombe sana ni muda sasa kuona kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tulikemee", - alisema IGP Sirro.

Aidha IGP Sirro amesema kuwa baadhi ya viongozi wa dini hawako kwa ajili ya kusaidia watanzania badala yake wapo kwasababu ya tama waliyonayo ya kutaka madaraka .

Hata hivyo IGP Sirro amewaonya viongozi wote wa dini wanaojihusisha na uhalifu kuwa atawachukilia hatua bila kujali nafasi yao katika jamii kwani ukikiuka sheria lazima uadhibiwe kwa mujibu wa sharia.

"Padri ukishajiingiza kwenye uhalifu mimi ntakushughulikia kama uhalifu mwingine, Padri ukishakuwa mbakaji ntakugonga kama mbakaji mwingine, Shehe/Padri ukijiingiza kwenye ugaidi ntakushughulikia kama gaidi hiyo kwasababua heshima ina ukubwa zaidi kuliko mtu binafsi" alisema

Najiuliza!! Mbona IGP ana hangaika sana?
Kuna jambo gani wamelipanga??
 
UPUUZI MTUPU! ZERO anatumika kutaka kuminya haki na uhuru wa Lissu. Kauli chungu nzima za wahuni wa maccm zinazotishia amani Nchini hajawahi kuzisikia.

 
Huyo Sirro kaongea na hao viongozi wa dini ili kuwatisha na kutaka waongee kile anachotaka. Hivi anadhani hao viongozi wa dini hawaoni double standard yake kwenye kushughulikia uhalifu? Au anadhani wanakaa kimya kwa kupenda?
 
Hivi mamlaka za uteuzi walitumia vigezo gani kumpendekeza Sirro kuw igp, namuona kama muoga, asiyejiamini na mnafiki anayejipendekeza kwa jiwe
 
Dawa muhimu ya kuendeleza amani nchini ni kwa Tume ya Uchaguzi kutenda haki. Bila haki hakuna amani.
 
Tena ilibidi awaambie waanze kukemea kauli zilizotolewa na yule mwanasiasa jimboni kwa Bwege wakati anatoka kumzika mkapa Eti hawezi peleka maendeleo jimboni kwa mpinzani πŸ˜‚πŸ˜‚
 
..Viongozi wa Dini wakianza kuikemea CCM itakuwaje?

..toka TL arudi nchini IGP amechanganyikiwa.

..nadhani hakutarajia kama TL atakanyaga ardhi ya Tz.
Namuonea huruma sana Sirro. Inabidi Father Kitima katibu mkuu wa baraza la maaskofu ampe counseling kubwa sana!!

Sijui Barua za Amaterdam zimemchanganya maana Naona kila akiwaza haoni kama Arrest Warrant ya ICC itamkosa mwaka huu!!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Aanze walau kumuonya mwenyekiti wa CCM ndipo tutamuelewa
 

..IGP awe mkweli kuwa anataka viongozi wamkemee Tundu Lissu.

..lakini kabla ya kumkemea wanapaswa kusisitiza atendewe HAKI, haswa ktk jaribio la kumtoa roho.
 
Hivi mamlaka za uteuzi walitumia vigezo gani kumpendekeza Sirro kuw igp, namuona kama muoga, asiyejiamini na mnafiki anayejipendekeza kwa jiwe

Cheo kimembadilisha Tabia.

Alipokua Mwz kama RPC alijitengenezea heshima yake baada ya kusema Wenje atangazwe kama ni yeye ameshinda uchaguzi huo maana police hawana resources za kuzuia watu walioko hapo nje ya ofisi za jiji wakichoma moto magari.

Baada ya hapo akarudishwa makao makuu kusoma magazeti akapewa cheo cha boss wa OP Maalumu.

Alipokuja kuteuliwa kua IGP hapo ndipo credibility yake imeanza kushuka kwa kasi.
 
..IGP aseme tu viongozi wa DINI wamkemee Tundu Antiphas Lissu.

..lakini wakifanya hivyo tutawauliza walikuwa wapi kukemea shambulizi dhidi yake?

..au walikuwa wapi kulihimiza jeshi la Polisi kuwa-serious na uchunguzi wa jaribio lile la mauaji?

..au viongozi wa dini walikuwa wapi wakati serikali na bunge wakimnyima matibabu, kumfuta ubunge, kumtisha, kumtukana, na kumkejeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…