IGP Sirro, amewaomba viongozi wa dini kukemea baadhi ya maneno yanayotamkwa na wanasiasa badala ya kukaa kimya

IGP Sirro amewataka viongozi wa dini kuhakikisha nyumba za ibada zinatumika kiibada na zisiwe vichaka vya wanasiasa na wahalifu.

Sirro amesema viongozi wa dini wanapaswa kujikita kwenye mambo ya kiimani na kuhubiri dini na siyo kuhubiri siasa kwani siasa wako Wanasiasa wenye jukumu hilo.
Kamanda amewahakikishia viongozi wa dini kuwa wakati wote wa uchaguzi amani itatamalaki kwa sababu wamejiandaa vyema.

IGP Sirro amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini wa Zanzibar.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Sirro anajua reaction ya serikali, viongozi wa dini walipokemea juu ya tabia ya kinyama ya kupoteza watu, kuteka, kuua na kushambuliwa, mambo yaliyoasisiwa kwenye awamu hii ya tano?

Sirro anajua Rais Magufuli atareact vipi viongozi wa dini wakikemea kauli zake za kibaguzi kama zile za watu wa Mwanza wasibomolewe nyumba zao kwa sababu walimchagua (kungine ni sawa wabomokewe)? Au kauli ile ya Rais Magufuli ya kuwa kwenye awamu hii, 'wa kasikazini wasubiri' Au kauli ile ya Rais kuwa, kwenye awamu hii tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote (bila hata ya kuwa na kosa lolote).

Sirro angeongea kwanza na Rais, ili Rais aje mbele ya watu awaambie kuwa sasa yupo tayari kukosolewa anapokosea, na wala vyombo vyake havitawadhuru wakosoaji tena, kama ambavyo amekuwa akifanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kama hana baraka za Mkulu,basi anakoelekea anaweza kupigwa chini wakati wowote ule.
 
Kwani yeye Sirro na Magufuli hawawezi kumjibu Lissu hadi waombe msaada wa Viongozi wa dini? Walipoketi kikao kufanya Uamuzi wa kufanya waliyoyafanya waliwaalika Viongozi wa dini? Labda Pengo ndo maana wanataka kumpa barabara, malafa sana Hawa jamaa
 
Haki kukaa kimya ni Bora zaidi
 
Anataka kujikosha, mambo yakiwa mambo. Lakini anachotakiwa Sirro kukijua ni kuwa Dunia imekwishafanya maamuzi juu ya utawala wa awamu ya 5 kutokana na rekodi yake mbaya ya igandamizaji, kuwaondolea watu haki za kuishi, kuwanyima watu uhuru wa maoni, kuua uhuru wa vyombo vya habari, kuua demokrasia, upendeleo na ubaguzi.

Wanasubiriwa kwenye incha 4, mojawapo tu inatosha kubadilisha historia.

Sirro asipoteze muda kuwahadaa watu, badala yake aende akafanye his core responsibility. Kujishikiza na watawala na CCM hakutamsaidia, zaidi ya kumletea majuto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana ila Gwajima je yupo upande gani sasa?
 
ujumbe uende directly mojakwamoja kwa gwajiboy
 
mhhhh...............
 
Tumkumbushe tu siro ya kwamba kiongozi wa dini akikemea tena ataambiwa sio raia,na tra watakuja kumpigia hesabu za mapatao na matumizi,huku msajili akimlima barua wajieleze kwaniniwasifutiwe usajili wanachanganya siasa na dini
 
Huyu kamanda naye ana ongea sana utadhani ni polepole
 
baada ya kuacha kukemea amekuwa mtanzania na pasipoti karejeshewa labda siro ajui kuhusu hilo
 
Mbona kama ana msema rais anaye shinda na viongozi wa dini
 
pia aongee kuhusu wanasiasa watumiao dini kupiga kampeni huku wakigawa rushwa makanisani kwa miaka mitano sasa,hi si ni kuchanganya dini na siasa
 
awmu hii inamuogopa lisu kuliko kuogopa shida za watz
 
Naona kaanza mapema kampen zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…