Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Lisu ni mshindi maana mti wenye matunda ndio upigwa mawe
 
Nafikiri Lissu ashasema hayuko yeye kama yeye. Yuko yeye na Wanachama wake, Bob Amsterdam, UN, AU vitengo vya haki za binadamu, vyombo vya habari vya kimataifa, Umoja wa Ulaya n.k

Angekuwa yeye kama yeye wala Sirro asingefanya press angekuwa kashamalizana nae huko huko. Nasubiria maneno ya utangulizi ya Lissu. Nafikiri ataripoti kituo cha polisi cha mahali alipo kwasasa hawezi kurudi Moshi.

Badala ya kuongea na Mbowe tu nafikiri kiitishwe kikao cha viongozi wa siasa, dini, polisi, tume na Serikali watu wakubaliane kuhusu HAKI itakavyotendeka na ionekane imetendeka kabla ya siku ya kura otherwise kuna hatari mbele maana uchaguzi huu wapinzani ni Sauli na Daud. Saul kajaribu kumaliza gemu nje ya uwanja toka 2017 imeshindikana.

Tunamsubiria Mungu mwenye HAKI na mwamuzi wa HAKI ambaye kisasi ni juu yake tuone analipaje kisasi uchaguzi huu.
 
Huku NEC, Huku Msajili, Huku Polis Huku CCM ..Wote mishale yao inaelekea kwa Lissu ...
Yote haya nikujaribu kumtafutia faraja Bw Yule Bingwa wa Ubaguzi. Hali yake ni mbaya hawezi tena kunadi miradi yake kazi kubwa hivi sasa ni kuwafokea na kuwatisha Wapiga Kura.

Tamko la Siro siyo la ajabu kwani Mteuzi wa Vyombo Vya Usalama toka mwanzo anajulikana kuwa kawapa Kazi Maalum Wateule wake. Kazi kubwa waliopewa na Mamlaka za Teuzi ni kuwanyanyasa kuwatesa Wapinzani.
 

..asante sana.

..ungekua hapa baa nilipo ningekupa offer ya nusu kuku, chipsi, na chupa mbili za heineken.
 
Ben, kama unabadilisha gia hewani hivi! Show your really colors sasa, siyo kung’ata na kupuliza!
 
Sirro ameonya kwa kusihi sana, siyo kwa amri kama tulivyomzoea.
 
Huyo kibaraka wa mabeberu aende haraka sana akaripoti polisi, huku NEC inamsubiri, ngoja tuone huyu kibaraka ataishia wapi. Na Watanzania hawana simile ile 28.10.2020 lazima wamkate vibaya mno.
 
Nyinyi endeleeni kumvimbisha kichwa tu huyo Lissu. Atakapoanza kunyea ndoo mtakaa kimyaa kama wakati ule Faru John ananyea ndoo mlikuwa mbaliii.
Sema kosa lake akanyee ndoo , sema jiwr ameshikwa pabaya anaanza kutumia kila linalowezekana kumdhibiti kisiki lisu .....
 
Lissu kawashika pabaya baada Magu kutepeta kwa Mwamba wakaja NECCM nao wakakuta mziki wa LISSU cd 700 Sasa wamefanya sub mwingine ambaye ni Sirro wakati Sirro anaingia huku Diwani kaambiwa awe anapasha
Nyie mjazeni tu upepo, akianza kushughulikiwa msilalamike. Jeshi la polisi limekua na uvumilivu sana kipindi hiki, limefumbia macho mambo mengi sana ya uvunjifu wa sheria wa makusudi kabisa. Lissu amefikia hatua mpaka anawagombeza polisi wanamuangalia tu. Siku akitandikwa makofi msilalamike kadhalilishwa. Kuwa mgombea u Rais haimaanishi kutotii mamlaka, sheria na vyombo vya dola.
 
Ndiyo mlichobaki nacho. Yaani hamjiamini kabisa yaani kila mara ICC.

Hivi Kati ya CCM na CHADEMA Nani asiyejiamini?
Huyu ambaye anataka ashinde kwa Goal la mkono kwa kutumia NEC,MSAJILI na POLICCM au huyu anayesema akinyang'anywa ushindi kwa Goal la mkono atawashtaki ICC??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…