Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Huku NEC, Huku Msajili, Huku Polis Huku CCM ..Wote mishale yao inaelekea kwa Lissu ...
Bila kusahau vyama vingine ambavyo badala ya kunadi sera zao wamejikita kumnanga Lisu
 
Tatizo chadema wanataka kufanya uanaharakati kwenye campaign. Kinachotakiwa ni kueleza sera na siyo matusi au kufanya Fujo.champain is just like interview. Sasa unafanyiwa interview then unawadanyia Fujo wenzio na mabosi wako.
 
Big up sana kwa Jeshi la Polisi kwa walichokifanya jana. Japo muda ulikua umeisha ila walimvumilia Tundu Lissu hadi akafika uwanjani na kusalimia..japo Lema nae alihutubia hadi zaidi ya saa 12 ila Polisi walikua kimya. Mungu awabariki
 
Kumtenganisha TL na wapiga kura Ili aende kituo Cha polisi kuhojiwa, ni kuhatarisha amani ya kituo Cha polisi na usalama wa raia. TL analindwa na escort 4 na kundi la zaidi ya watu elfu kwa wakati mmoja.kumuita polisi IGP hujaitakia polisi haki. Ili kuweka mambo sawa muite wewe kwenye kituo Cha polisi nawe uwepo kituoni hapo uone Hali halisi. Raia wako frustrated kimaisha na wamekatwa tamaa wanaona suluhu ni TL. Polisi tumieni hekima kwa hili .
Maisha huku mtaani ni magumu sana,kukikucha ni heri ya jana,asilimia kubwa ya wananchi wameshakata tamaa ya kuishi,hata ikitokea wakaamasishwa Leo kuingia barabani wako tayari kwa kuwa hawana cha kupoteza ,ukiwauwa kwao wanaona umewasaidia kuwapumzisha.ccm shukuruni Mungu viongozi Wa upinzani ni wastaarabu sana,ndio wameshikilia amani ya nchi hii.

Ikitokea kiongozi akaamasisha watu waandamane Leo hapatakalika,watatoka kwa wingi sana kwa sababu wanajua wakiingia huko mtaani watavunja hata maduka ya wahindi wapore chochote.

Vyombo vya dola na nyie mtende haki ,fanyeni kazi kwa weledi kama mlivyofundishwa maadili ya kazi zenu,msi pendelee chama tawala..
 
Watu wanamshangaa anapoongea ulaghai na uongo wa kijinga na kuchokoza vyombo vya dola eti kisa kateuliwa na wazungu kuja kugombea !!
Uwezo wako wa kuchakata mambo ni mchache mno, alamsik!
 
Kwanza tumuulize Sirro alishawashughulikia waliompiga risasi Lissu.

Huyu Mzee vipi , hajui Kesho anaweza amka akakuta yeye siyo IGP.
Sirro acha blah blah miaka 5 mnaminya uhuru wa watu kukutana na kujieleza .

Not only Lissu....!!!Kuna wale waliomwua Mwenyekiti CHADEMA mkoa Geita comrade Alphonce Mawazo, walio wateka na kuwapoteza Azory Gwanda na Ben Saanane......!?? Tuanzie hapo.
 
Tatizo chadema wanataka kufanya uanaharakati kwenye campaign. Kinachotakiwa ni kueleza sera na siyo matusi au kufanya Fujo.champain is just like interview. Sasa unafanyiwa interview then unawadanyia Fujo wenzio na mabosi wako.
Unapotaka kutusemea sisi wananchi tokea lini umekuwa msemaji wa wananchi?
 
Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

View attachment 1587125

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
Pumba tupu.
Ndio maana makonda alikutuhumu kula rushwa ya shisha maana alishakuona kamanda wa maneno mengi yasiyo msingi.
 
Tundu Lisu kayataka mwenyewe.
yaaani amekuwa akiwa tukana Askari hadi mimi mwenyewe naogopa!!!
halafu cha kushangaza wakati huo huo anataka ulinzi !! Duh!!
Acha ushamba lissu ana jeshi lake watu wamevaa mitambo so policcm wamevaa tu night dress
 
Nafikiri Lissu ashasema hayuko yeye kama yeye. Yuko yeye na Wanachama wake, Bob Amsterdam, UN, AU vitengo vya haki za binadamu, vyombo vya habari vya kimataifa, Umoja wa Ulaya n.k

Angekuwa yeye kama yeye wala Sirro asingefanya press angekuwa kashamalizana nae huko huko. Nasubiria maneno ya utangulizi ya Lissu. Nafikiri ataripoti kituo cha polisi cha mahali alipo kwasasa hawezi kurudi Moshi.

Badala ya kuongea na Mbowe tu nafikiri kiitishwe kikao cha viongozi wa siasa, dini, polisi, tume na Serikali watu wakubaliane kuhusu HAKI itakavyotendeka na ionekane imetendeka kabla ya siku ya kura otherwise kuna hatari mbele maana uchaguzi huu wapinzani ni Sauli na Daud. Saul kajaribu kumaliza gemu nje ya uwanja toka 2017 imeshindikana.

Tunamsubiria Mungu mwenye HAKI na mwamuzi wa HAKI ambaye kisasi ni juu yake tuone analipaje kisasi uchaguzi huu.
Hii uliyoiandika inaitwa hekima na busara.
 
Leo ndio nimeamini kuwa hata saa mbovu kuna wakati inasema kweli
 
Amevunja sheria gani?
Nyinyi endeleeni kumvimbisha kichwa tu huyo Lissu. Atakapoanza kunyea ndoo mtakaa kimyaa kama wakati ule Faru John ananyea ndoo mlikuwa mbaliii.
 
Back
Top Bottom