Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro


Amesema hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa.

Nimeona viongozi wa Chadema wanakaripia askari, Tundu Lissu anakaripia watu wangu, namuonya sana, jana nimeongea na Mbowe, akae azungumze na watu wake watii sheria bila shuruti.

"Tundu Lissu hayupo juu ya sheria, tukiamua kutimiza majukumu yetu asilalamike,"IGP Simon Sirro

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, amri hiyo inatokana na IGP kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na matendo mbalimbali ambayo wanayofanya.

Akifafanua suala hili IGP Sirro amesema "Nimeona matukio kadhaa yakifanyika na Viongozi wa Chadema, wamekuwa wakikaripia na kuwagombeza Askari Polisi. Nimeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana na Viongozi wa Polisi".

"Jana nimeongea na Kiongozi wake Bwana Mbowe akae na viongozi wake wazungumze suala la kutii sheria bila shuruti. Anayoyafanya Watanzania wenye hekima na Wazalendo wanaona. Lissu hayuko juu ya sheria polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake. Vyama vipo karibu kumi na mbili, Jeshi la Polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zao ndani ya nchi hii, yeye hana uwezo wowote wa kupambana na Jeshi la Polisi."

"Asije akafika mahali akawa na kiburi akadhani ana uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi. Niwasihi sana na niwaombe sana ndugu zetu wa Chama cha Chadema hii tabia iishe. Tundu Lissu aende akaripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro ili aende akaeleze aliyoyafanya jana. Lakini niwaombe wanasiasa na Viongozi wote katika ngazi zote. Suala la Udiwani, Ubunge, Urais bila amani na utulivu huwezi kufanya siasa na huna uwezo wa kupambana na Jeshi la Polisi wewe kama wewe. Kwahiyo tuheshimu sheria zilizopo ili tuchague viongozi tunaowataka lakini inaonekana kuna ajenda ya siri ambayo viongozi wachache wanayoitaka ili uchaguzi usifanyike. Nawaambia uchaguzi utafanyika lakini itafika mahala tutawashughulikia sana."
View attachment 1587125
Ni kweli alichosema bwana zero kwamba Tundu Lissu yeye kama yeye hana uwezo wa kupambana na polisi lakini ni kweli unaojulikana popote duniani na watu wote wenye akili timamu kwamba hakuna jeshi la polisi lenye uwezo wa kuwadhibiti raia wote wa nchi husika wakiamua kuliamsha.

Cha msingi kila mmoja aheshimu mipaka yake, na jeshi lako bwana zero lifanye kazi kwa weredi.
 
Vyama viko 12 lkn kinachowapa makavu ni kimoja tu. Mimi siwezi kuwasapoti wakati sie tu wazaliwa zilipo dhahabu barabara za vumbi na hatuna maji lkn mnaenda kujenga uwanja wa ndenge Chato. Piga uwa nawaambia walioko huko wasidaganyike
 
Kimsingi sirro wakati huu wa uchaguzi kwa sheria ya uchaguzi alitakiwa kupeleka malalamiko yake kwene kamati ya maadili, na Lissu alivo wa vifungu subirini muone hili picha lazima wakamchukue na kalandinga hivihivi hichi kichwa hakitoripoti
 
IGP namuelewa. Kwa tension iliyopo ya kisiasa haswa upande huo mwingine na presha za wapambe, asipofanya jambo ataonekana haungi mkono.

Pole mkuu.
Ndo kazi.
Kwenye kazi unaweza fikishwa mahali ukatakiwa kufanya dhulma ambayo hata nafsi yako inakusuta.
 
Ni kweli alichosema bwana zero kwamba Tundu Lissu yeye kama yeye hana uwezo wa kupambana na polisi lakini ni kweli unaojulikana popote duniani na watu wote wenye akili timamu kwamba hakuna jeshi la polisi lenye uwezo wa kuwadhibiti raia wote wa nchi husika wakiamua kuliamsha.

Cha msingi kila mmoja aheshimu mipaka yake, na jeshi lako bwana zero lifanye kazi kwa weredi.

Police awafiki laki moja wataweza vipi dhibiti nguvu ya umma.
Mbeya tu walizidiwa nguvu na machinga Hadi wakaomba po na kumuomba Sugu awasaidie ndo wataweza nchi nzima.
Always polisi huwa ni vibaraka wa madikteta but jeshi halijawahi waangusha wananchi jeshi usimama na msimamo wa wananchi na kumsaliti dikteta.
 
Yule bwana baada ya kumuagiza mahera wa tume asiyejua Sheria za tume kugonga mwamba kaamua kumtumia ziro kumpiga biti,huu wito wa mitandaonii utaishia kwenye mitandao hivyo hivyo.
Hakuna kosa kumfokea polisi asiyefata sheria.
Juzi alianza yule Liberatus Sabas, Sirro nae leo katokea.
 
Huyu mbona anabwatuka na anasingizia eti Lissu anafokea watu wake,hapa kashinikizwa kuongea ili ionekane anakusaidia ccm,afanye anachoona kkinafaa Kama ana amri juu ya polisi atakavyo yeye,kacheo kanamzuzua
 
Anajua na kundi lake la NEC and others kuwa hooks and crooks lazima Jiwe ashinde....
Hivi nauliza igp ameshajua nan rais kama sio anapata wapi nguvu ya kumtisha mgombea kutoka chama kikubwa cha upinzani
 
Jiwe kila siku anawafokea na kuwakaripia polisi mbona amwambii akaripoti polisi. Aache kutisha wananchi, asiamshe hasira za watz.
 
Inasemekana sirro katukanwa sana na jiwe kwa kile kilochotokea moshi kuruhusu lissu kufanya mutano mpakasa usiku,so sirro anajaribu kumfurahisha boss kiwa anachukua hatua
 
Back
Top Bottom