Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Imenenwa katika kitabu cha Mithali katika Biblia katika sura ya 14:34 ikisema hivi nanukuu " Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.
Tumemsikia wenyewe IGP Sirro akitutisha watanzania kuwa Jeshi lake la Polisi liko imara na linafanya mazoezi ya nguvu ili kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani huko visiwani Pemba, wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hebu tumuulize huyo IGP Sirro anawezaje kulinda amani ya nchi, huku akiwalinda watawala walioko madarakani ambao hawatendi haki?
Yeye anajua kuwa huko visiwani Pemba ndiko ambapo watawala wa CCM kwa kuitumia Tume yao ya uchaguzi (ZEC) hawataki kuitenda haki kwa kuwaengua wagombea 15 kati ya 18 wa visiwani humo wa chama cha ACT Wazalendo.
Inajulikana kisheria kuwa wanaoruhusiwa kuweka pingamizi ni wagombea wenzao.
Wakati hali ni tofauti huko Pemba, ambako badala ya wagombea kuwawekea mapingamizi wagombea wenzao, badala yake ni Tume yenyewe ya Zanzibar, ndiyo iliyowawekea mapingamizi ya mizengwe hao wagombea wa ACT Wazalendo!
Mwanzoni Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilituaminisha kuwa wagombea hao wa chama cha ACT Wazalendo wamewekewa pingamizi na wagombea wenzao wa CCM.
Hata hivyo wagombea hao wa CCM "wamewaruka kimanga" Tume hiyo kwa kukanusha kuwa siyo wao walioweka pingamizi hizo!
Ni dhahiri kuwa Tume hiyo ndiyo ilyounda "mizengwe" hiyo kwa kuwawekea pingamizi hizo ambapo ni kinyume cha sheria, kwa kuwa wao siyo miongoni ya watu wanaoruhusiwa kuweka pingamizi hizo!
Tunapata picha gani hapa?
Kuwa utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 umepania kuiondoa amani iliyopo nchini mwetu kwa kutotenda haki katika sanduku la kura kwa "kulazimisha" wapiga kura wawapigie wagombea wa CCM ambao wao wananchi siyo chaguo lao.
Inafahamika katika historia ya vyama vingi miaka yote tokea mwaka 1995 urudishwe tena mfumo wa vyama vingi nchini, tukishuhidia huko Pemba, chama cha CCM kikiambulia 0 dhidi ya chama ambacho huwa anakuwepo Maalim Seif ambacho huwa kinazoa kura zote.
Pamoja na juhudi zote za watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 "kumtumia" Profesa Lippumba kuivuruga CUF, hatimaye Maalim Seif akaamua kumwachia chama "chake" huyo Profesa Lipumba na yeye Maalim Seif kuhamia chama cha ACT Wazalendo, bado tu watawala hawa wa awamu ya 5 hawajaaacha kumsakama Maalim Seif na hivi sasa ndiyo wameamus kuwaengua wagombea wao 15 kati ya wagombea wao 18 visiwani humo Pemba!
Watawala wetu wanapaswa kujikumbusha historia ya dunia hii tokea iundwe, ambapo hakujawahi kutokea nguvu za kijeshi zikashinda nguvu ya Umma!
Vivyo hivyo huko visiwani Pemba mwaka huu huyo IGP Sirro astegemee kuwa kwa kuulinda huu udhalimu unaofanywa na watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 ndiyo ataweza kudumisha amani kwa kutumia mtutu wa bunduki na magari ya washawasha!
Hataweza kuwazima wananchi wa visiwa hivyo vya Pemba ambao wanajua wazi kuwa wagombea wao wa chama cha ACT Wazsendo wameenguliwa kihuni!
Kama watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 wanataka kudumisha amani ya kudumu visiwani humo hawana bidi kuyarejesha majina ya wagombea wa ACT Wazalendo walioenguliwa na waendeshe uchaguzi ulio huru na wa Haki
Kinyume cha hapo watawala wetu wanataka kutuletea machafuko makubwa ya umwagaji damu kwenye uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu