Uchaguzi 2020 IGP Sirro asidhani kuwa anaweza kudumisha amani visiwani Pemba kwa kutumia mitutu ya bunduki na magari ya washawasha

Uchaguzi 2020 IGP Sirro asidhani kuwa anaweza kudumisha amani visiwani Pemba kwa kutumia mitutu ya bunduki na magari ya washawasha

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Imenenwa katika kitabu cha Mithali katika Biblia katika sura ya 14:34 ikisema hivi nanukuu " Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Tumemsikia wenyewe IGP Sirro akitutisha watanzania kuwa Jeshi lake la Polisi liko imara na linafanya mazoezi ya nguvu ili kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani huko visiwani Pemba, wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hebu tumuulize huyo IGP Sirro anawezaje kulinda amani ya nchi, huku akiwalinda watawala walioko madarakani ambao hawatendi haki?

Yeye anajua kuwa huko visiwani Pemba ndiko ambapo watawala wa CCM kwa kuitumia Tume yao ya uchaguzi (ZEC) hawataki kuitenda haki kwa kuwaengua wagombea 15 kati ya 18 wa visiwani humo wa chama cha ACT Wazalendo.

Inajulikana kisheria kuwa wanaoruhusiwa kuweka pingamizi ni wagombea wenzao.

Wakati hali ni tofauti huko Pemba, ambako badala ya wagombea kuwawekea mapingamizi wagombea wenzao, badala yake ni Tume yenyewe ya Zanzibar, ndiyo iliyowawekea mapingamizi ya mizengwe hao wagombea wa ACT Wazalendo!

Mwanzoni Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilituaminisha kuwa wagombea hao wa chama cha ACT Wazalendo wamewekewa pingamizi na wagombea wenzao wa CCM.

Hata hivyo wagombea hao wa CCM "wamewaruka kimanga" Tume hiyo kwa kukanusha kuwa siyo wao walioweka pingamizi hizo!

Ni dhahiri kuwa Tume hiyo ndiyo ilyounda "mizengwe" hiyo kwa kuwawekea pingamizi hizo ambapo ni kinyume cha sheria, kwa kuwa wao siyo miongoni ya watu wanaoruhusiwa kuweka pingamizi hizo!

Tunapata picha gani hapa?

Kuwa utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 umepania kuiondoa amani iliyopo nchini mwetu kwa kutotenda haki katika sanduku la kura kwa "kulazimisha" wapiga kura wawapigie wagombea wa CCM ambao wao wananchi siyo chaguo lao.

Inafahamika katika historia ya vyama vingi miaka yote tokea mwaka 1995 urudishwe tena mfumo wa vyama vingi nchini, tukishuhidia huko Pemba, chama cha CCM kikiambulia 0 dhidi ya chama ambacho huwa anakuwepo Maalim Seif ambacho huwa kinazoa kura zote.

Pamoja na juhudi zote za watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 "kumtumia" Profesa Lippumba kuivuruga CUF, hatimaye Maalim Seif akaamua kumwachia chama "chake" huyo Profesa Lipumba na yeye Maalim Seif kuhamia chama cha ACT Wazalendo, bado tu watawala hawa wa awamu ya 5 hawajaaacha kumsakama Maalim Seif na hivi sasa ndiyo wameamus kuwaengua wagombea wao 15 kati ya wagombea wao 18 visiwani humo Pemba!

Watawala wetu wanapaswa kujikumbusha historia ya dunia hii tokea iundwe, ambapo hakujawahi kutokea nguvu za kijeshi zikashinda nguvu ya Umma!

Vivyo hivyo huko visiwani Pemba mwaka huu huyo IGP Sirro astegemee kuwa kwa kuulinda huu udhalimu unaofanywa na watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 ndiyo ataweza kudumisha amani kwa kutumia mtutu wa bunduki na magari ya washawasha!

Hataweza kuwazima wananchi wa visiwa hivyo vya Pemba ambao wanajua wazi kuwa wagombea wao wa chama cha ACT Wazsendo wameenguliwa kihuni!

Kama watawala hawa wa serikali ya awamu ya 5 wanataka kudumisha amani ya kudumu visiwani humo hawana bidi kuyarejesha majina ya wagombea wa ACT Wazalendo walioenguliwa na waendeshe uchaguzi ulio huru na wa Haki

Kinyume cha hapo watawala wetu wanataka kutuletea machafuko makubwa ya umwagaji damu kwenye uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu
 
Wanasiasa wapambane kisiasa
Wanaokimbilia kuvunja amani watashughulikiwa tu
 
Ila wapinzani wana moyo, wakati mwingine matendo yanayofanywa na jeshi la polis yanauma zaidi.polis katika kipindi hiki cha uchaguzi muda wote in kuanzisha chokochoko na wapinzani.Fikiria mfano wale wagombea ubunge na udiwani waliokamatwa na polis Dodoma Jana wakifuatilia rufaa zao tume. Muda mwingi polis wetu wanatafuta uhasama na wapinzani.
 
Hawa Polisi ndiyo watakaoleta umwagaji damu nchi hii.........

Wasidhani kuwa wananchi kukaa kimya pamoja na maonevu makubwa wanayofanyiwa na watawala hawa dhalimu wa CCM, ndiyo kuwaogopa hao Polisi........

Watawala wetu ni lazima wafahamu kuwa kila chenye mwanzo kitafikia mwisho wake.............
 
Sasa wewe hebu niambie hivi kuwaengua wagombea kwa mizengwe ndiyo kupambana kisiasa?
Kuwekeana mapingamizi ndo siasa hiyo
Wapambane kisiasa na/au kisheria
Hata hao ACT walifanya, sasa wakizidiwa nguvu wasikimbilie kuvunja amani
 
So Wakivunja amani watashughulikiwa...hii wala sio siri, ipo wazi
 
Sirro aache upumbavu na ukibaraka. Pemba maji ni mazito. Umwamba utamvua kombati kininja. Haki italeta amani na siyo gobole la Polisi. Mtu mzima mithili ya Maalim Seif anapotamka "ukhanithi sasa BASI" ujue si neno la kitoto. Gaddafi pamoja na kuwa na Jeshi bora akaenda kufia kwenye karavati. Sirro na Jiwe wako msituharibie nchi tafadhali. Kama ninyi siyo raia wa nchi hii ondokeni kwenu mtuachie nchi yetu salama.
 
Mimi naamini kabisa ndani ya jeshi la polisi wameingizwa vijana wa UVCCM na "green guards" ambao wameamdaliwa kufanya uhalifu wakati wa uchaguzi.
 
Magufuli kakusudia kuandika historia yake ya kumwaga damu za Waislm huko Pemba.
Lakini Allah Akbar mara hii ni pemba yote itatoka kupambana
Ataua 30 elfu walobaki watasonga mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika historia ya dunia hii, hakuna mahali popote duniani ambapo kuliwahi kutokea maguvu ya Jeshi yaliwahi kushinda nguvu ya Umma iliyojizatiti
 
CCM ikitoka tu madarakani mwaka huu, serikali za awamu zikazofuatia huku Tanganyika na Zanzibar itazipasa kuanzisha "zoo" ambazo ndani yake tutawaweka baadhi ya makada fedhuli wa chama hiki. Hawa watakuwa ni wale ambao siku zote walikuwa ni watu wasioishiwa vituko, hila, ukatili na uovu mwingi na wa kila aina, ambao kwa makusudi kabisa mienendo yao ilikwenda kinyume na viapo walivyoviapa vya kuilinda, kuitii na kuitunza katiba.
 
Umenena vyema
 
Ila wapinzani wana moyo, wakati mwingine matendo yanayofanywa na jeshi la polis yanauma zaidi.polis katika kipindi hiki cha uchaguzi muda wote in kuanzisha chokochoko na wapinzani.Fikiria mfano wale wagombea ubunge na udiwani waliokamatwa na polis Dodoma Jana wakifuatilia rufaa zao tume. Muda mwingi polis wetu wanatafuta uhasama na wapinzani.
Ndio maana maeneo mengine ...baada ya mabadiliko watu Kama hao huwa wanatafutwa!
 
Sirro aache upumbavu na ukibaraka. Pemba maji ni mazito. Umwamba utamvua kombati kininja. Haki italeta amani na siyo gobole la Polisi. Mtu mzima mithili ya Maalim Seif anapotamka "ukhanithi sasa BASI" ujue si neno la kitoto. Gaddafi pamoja na kuwa na Jeshi bora akaenda kufia kwenye karavati. Sirro na Jiwe wako msituharibie nchi tafadhali. Kama ninyi siyo raia wa nchi hii ondokeni kwenu mtuachie nchi yetu salama.
Huo ukhanithi mtafanyiwa sana na Jamba mtakachofanya
 
Back
Top Bottom