Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamezidi rushwa ndio maana ajali kila sikuYaan hao wenye mavaz meupe ndio kama wamejipa majukumu wamebaki kuokoteza kama wanakusanya hela za mchezo, pita maeneo haya uone utafikiri kama wao vijumbe wa michezo.
1 Mwembe yanga
2😀arajani njia hii kama unaenda kutokea keko
3😛ale relini (DEVIS CONNER) kama unakwenda Buza.
Lazima ajari zitokee sana, watu wamejipa majukumu mengine badala ya kusimamia
Wametajirika sana hakuna traffic asiye na magari na majumba ya kifahariTatizo polisi wameshaona kupokea rushwa na kuchukua hela za raia ni haki yao.. hapo usitegemee watatimiza majukum yao hata akija nani. Madereva wengi hata akiwa amekamilisha kila kitu lakini bado anatakiwa kuwa na hela ya trafiki na sio ya faini
Ubovu wa breki ni ubovu wa gari ni jukumu lao piaUmesema chanzo kikubwa ni mwendo kasi... nakupinga hili..
Ajali zote za mkoa wa mbeya asilimi zaidi ya 80 ni ubovu wa mifumo ya magari hasa upande wa brake...
Kingine ni miondombinu ya barabara..mfano moja ya ajli za Mbeya derea wa roli alihama upande wake akaajaa kulia kisa akwepe shimo lilikua upande wake...sasa hapa siro sijui tumuweke wapi.
naomba nimalize ....
Asante kwa kunisaidiaKama nimesoma uzi vizuri mleta uzi ametaja ubovu wa magari ambayo breki inaingia humo na ubovu wa barabara ameutaja pia.
Kumbuka polisi kikosi cha usalama ni jukumu lao kukagua ubovu wa gari lkn wao huegemea makusanyo tu
PamojaAsante kwa kunisaidia
Katika visababishi vya ajali ulivyoviainisha umesahau kimoja ambacho kinaweza kuwa kikubwa kuliko hivyo vingine nacho ni ubovu wa barabara zetu.Kwako Afande IGP Sirro.
Kwanza naomba nikupongeze kwa jitihada zako nyingi unazozifanya kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa salama pamoja na mali zao.
Najua kipindi hiki ni kigumu sana hasa tukizingatia wimbi jipya la mauaji ya kikatili yaliyoibuka hivi karibuni ambapo kumekuwa na mauaji mengi sana yanayisadikiwa yanasababishwa na wivu wa mapenzi, imani za ushirikina na visasi.
AJALI
Pamoja na hayo mauaji niliyoyataja hapo juu, kuna hili wimbi la ajali ambalo karibu kila baada ya siku 3 au wiki kunakuwa na tukio la ajali.
Kamanda Sirro, haya matukio ya ajali za kila mara linatia doa sana utumishi wako uliotukuka.
Ukifuatilia matukio haya kwa undani, chanzo kikuu ni mwendo kasi wa madereva.
Maeneo ambayo ajali za hivi karibuni ni mikoa ya:
1. Mbeya, mkoa huu ajali zimetokea zaidi ya mara 5 ndani ya miezi 2 na ajali ya mwisho mkoani humo ni leo Jumanne saa 10 jioni kwa lori kugonga basi dogo la abiria na zaidi ya watu 6 kupoteza maisha na majeruhi wengi.
2. Iringa, ilitokea ajali ya lori na basi dogo la abiria na zaidi ya watu 18 kupoteza maisha papo hapo.
3. Mikoa mingine ni Arusha, Singida, Tanga, Geita, Shinyanga, Morogoro, Manya na Dodoma ambayo imetokea wiki iliyopita.
Na ajali zote hizi zimeondoa maisha ya Watanzania na kusababisha ulemavu wa kudumu.
Hii haikubaliki na haikubaliki tena.
Ajali za barabarani huwa na vyanzo mbalimbali kama uzembe wa madereva, ubovu wa magari, mwendo kasi na ubovu wa barabara pia huwa ni chanzo.
Katika utafiti mdogo nilioufanya nimegundua zaidi ni mwendo kasi wa madereva pamoja na ubovu wa magari.
Haya makosa mawili niliyainisha yako ndani ya uwezo wa udhibiti wa jeshi la polisi.
NINI KIFANYIKE?
1. Nashauri mabadiliko ya mabadiliko ya Kamanda wa kikosi cha barabarani, pamoja na juhudi zake lakini nimegundua hana mbinu mpya za udhibiti wa ajali na
2. Kamanda huyu hana sauti ya kiungozi hivyo makamanda wa mikoa na wilaya hawaiheshimu sauti yake hivyo inaonyesha ameachiwa apambane mwenyewe.
3. Inaonyesha makamanda wa usalama barabarani hawana mwitikio kumpa ushirikiano Kamanda wa usalama barabarani taifa.
Katika hiki sitaingia ndani wewe una vyanzo vingi vya kupata taarifa ukifuatilia ndani ya siku moja utafahamu yaliyojificha nyuma mgomo huu baridi.
4. Ninashauri ikikupendeza umrudishe Kamanda Fortunatus Muslim, pamoja na madhaifu yake lakini yanarekebishika sio sawa na ya kamanda wa sasa.
Ksuli mbiu yake ya KAMATA au nyakua nyakua ilisaidia sana kupunguza ajali na aliwamudu makamanda wa mikoa na wilaya yaani RTO NA DTO
Vilevile sababu ya msingi iliyokufanya umuondoe kwenye nafasi yake...mvutano wake kati yake na aliyekuwa ZTO haupo tena...
Ikiwa yupo Kamanda unayeona atafaa zaidi pia itapendeza ilimradi pawepo na usalama barabarani Afande wangu.
Ninakutakia utumishi uliotukuka na umalizie utumishii huu kwa rekodi nzuri.
![]()
WATU WATANO WAFARIKI DUNIA AJALI YA MCHOMOKO SIMIYU
Malunde1 blog Fahari ya Shinyanga ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.www.malunde.com
[emoji778][emoji820] AJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE WAKIENDA KUZIKA TABORA[emoji1313][emoji117]AJALI YAUA WATU SITA NA KUJERUHI WANNE WAKIENDA KUZIKA TABORA
Mbona ametaja?Katika visababishi vya ajali ulivyoviainisha umesahau kimoja ambacho kinaweza kuwa kikubwa kuliko hivyo vingine nacho ni ubovu wa barabara zetu.
Barabara zetu sii rafiki kabisa katika uchumi wa kati na kuenda huko juu. Labda tuendelee kubaki dunia ya tatu kwa kushindwa kwenda speed ya uchumi wa kati kwa kuzuia au kuulaza uchumi pale tunapokatisha safari za usiku kwa wasaka uchumi.
Magari yanazuiwa kusafirish abiria usiku kwa sababu kubwa ya ubovu wa barabara.
Soma hapo[emoji116][emoji116][emoji116]Katika visababishi vya ajali ulivyoviainisha umesahau kimoja ambacho kinaweza kuwa kikubwa kuliko hivyo vingine nacho ni ubovu wa barabara zetu.
Barabara zetu sii rafiki kabisa katika uchumi wa kati na kuenda huko juu. Labda tuendelee kubaki dunia ya tatu kwa kushindwa kwenda speed ya uchumi wa kati kwa kuzuia au kuulaza uchumi pale tunapokatisha safari za usiku kwa wasaka uchumi.
Magari yanazuiwa kusafirish abiria usiku kwa sababu kubwa ya ubovu wa barabara.