IGP Sirro, kuna Polisi watatu Tip Top barabara ya kuelekea Mabibo wanakusanya rushwa

Moshi-Arusha wanajificha porini wapige tochi.
 
Ningekuwa Rais hiki kitengo cha trafiki ningewapa mamlaka ya kiraia. Polisi wanachafuliwa sana na hichi kitengo hovyo kabisa wanakula rushwa hovyo halafu virushwa vyenyewe 5k,10k.
Wanachukua elfu mbili tu Mkuu.

Za Kubrashia viatu.
 
Hawa na wale wa Magomeni lao moja kuna na kajamaa wanashirikiana nacho kazi yake ni kuvuka zebra na kurudi ili awabambikie watu kosa la kuvuka zebra , yaani wapuuzi sana , huko njia ya mbezi ndio usiseme kuna wamama wana vitambi kuliko wanaume wanakula rushwa kama vinyozi wanavyokula vichwa, ni aibu sana hawa askari, kwanza wana wivu pili wanadharau askari anamuuliza mtu eti unajitia uko kwenye kiyoyozi sisi maisha yetu juani
 
hivi ile taasisi ya kuzuia mirungura bado ipo kweli? au imebakia kibogoyo baada ya mama kuing'oa meno?
 
Mhh
IMG_20211123_210605.jpg
 
Kuna vijana wako watatu, WP wawili na mwanaume mmoja mwembamba. Wako hapa TipTop barabara ya kuelekea Mabibo. Wanakusanya rushwa kwenye daladala na bajaji kama vile konda anavyokusanya nauli kwenye daladala.

WP kazi yao ni kusimamisha halafu konda wa kukusanya ni huyo mwanaume.

Nilikuwa Arusha, same style kwa daladala zinazowaisha akina mama sokoni asubuhi. Watu wanalalamika kimya kimya.

N:B Rushwa ikiendelea kwa kasi hii haswa ndani ya jeshi la polisi, muda si mrefu wananchi wataanza kukinukisha
Kuna Mwingine tupo hapa Sinza Mapambano jirani kabisa na Yard ya Mwanamboka, Mrefu Mweupe anakusanya Rushwa kama katumwa yaani. Hivi ninavyo andika katoka pokea rushwa ya 5000 kwa Kondakta wa Daladala ya Makumbusho Posta via Shekilango.
 
Kuna vijana wako watatu, WP wawili na mwanaume mmoja mwembamba. Wako hapa TipTop barabara ya kuelekea Mabibo. Wanakusanya rushwa kwenye daladala na bajaji kama vile konda anavyokusanya nauli kwenye daladala.

WP kazi yao ni kusimamisha halafu konda wa kukusanya ni huyo mwanaume.

Nilikuwa Arusha, same style kwa daladala zinazowaisha akina mama sokoni asubuhi. Watu wanalalamika kimya kimya.

N:B Rushwa ikiendelea kwa kasi hii haswa ndani ya jeshi la polisi, muda si mrefu wananchi wataanza kukinukisha
Unafikiri yeye anakosa mgao hapo?
 
Hawa na wale wa Magomeni lao moja kuna na kajamaa wanashirikiana nacho kazi yake ni kuvuka zebra na kurudi ili awabambikie watu kosa la kuvuka zebra , yaani wapuuzi sana , huko njia ya mbezi ndio usiseme kuna wamama wana vitambi kuliko wanaume wanakula rushwa kama vinyozi wanavyokula vichwa, ni aibu sana hawa askari, kwanza wana wivu pili wanadharau askari anamuuliza mtu eti unajitia uko kwenye kiyoyozi sisi maisha yetu juani
Niliyoyashuhudia leo mpaka moyo ulienda mbio. Nikfikiri nimepatwa na presha.

Kuna dereva mmoja wa bajaji alivyokuwa anampa yule askari konda bahati mbaya ikadondoka. Jamaa hakuogopa hata kuiokota
 
Ningekuwa Rais hiki kitengo cha trafiki ningewapa mamlaka ya kiraia. Polisi wanachafuliwa sana na hichi kitengo hovyo kabisa wanakula rushwa hovyo halafu virushwa vyenyewe 5k,10k.
Sio ndogo hizo akikusanya kwa watu 50x10000
alafu 50x5000 unapata ngapi hapo!?
 
Washenzi mno kuna mmoja nilimkimbia Sinza njia ya kutoka Tandale juzi tena ni demu! Kasimamisha Eicher 2 njia nyembamba tamaa anataka namie nisimame mbele nikajifanya kama simsikii nikanyoosha hadi mataa ya kijiweni😅!

Hawana sababu zaidi ataomba leseni ili akufosi kukuandikia😅 kosa lolote umpe hela!
Bongo watu wanaendesha magari kwa mateso

Ova
 
Tuulizane tu kwa uhalisia, je Polisi wakiacha kuchukua rushwa wakasimamia sheria utaweza kuendesha hilo gari lako? Je daladala zitaweza kufanya huduma zake?
Kwa uzoefu wangu hakuna dereva daladala anayelalamika kudakisha hizo 2000, huwa wanalia wanapoandikiwa faini ambayo ndio sheria yenyewe
 
Serikali ya kitu kidogo😁😁😁
 
Zerro yuko bize kughushi RB ya Central kuonyesha makomandoo wa Mbowe walilala hapo na sio Tazara hana habari na Manzese
 
Tuulizane tu kwa uhalisia, je Polisi wakiacha kuchukua rushwa wakasimamia sheria utaweza kuendesha hilo gari lako? Je daladala zitaweza kufanya huduma zake?
Kwa uzoefu wangu hakuna dereva daladala anayelalamika kudakisha hizo 2000, huwa wanalia wanapoandikiwa faini ambayo ndio sheria yenyewe
Nakubali.... Humu unakuta nusu wote hata leseni hawana ikiandikwa 30 barabara zitabaki nyeupe
 
Back
Top Bottom