IGP Sirro, kuna Polisi watatu Tip Top barabara ya kuelekea Mabibo wanakusanya rushwa

Moshi-Arusha wanajificha porini wapige tochi.
 
Ningekuwa Rais hiki kitengo cha trafiki ningewapa mamlaka ya kiraia. Polisi wanachafuliwa sana na hichi kitengo hovyo kabisa wanakula rushwa hovyo halafu virushwa vyenyewe 5k,10k.
Wanachukua elfu mbili tu Mkuu.

Za Kubrashia viatu.
 
Hawa na wale wa Magomeni lao moja kuna na kajamaa wanashirikiana nacho kazi yake ni kuvuka zebra na kurudi ili awabambikie watu kosa la kuvuka zebra , yaani wapuuzi sana , huko njia ya mbezi ndio usiseme kuna wamama wana vitambi kuliko wanaume wanakula rushwa kama vinyozi wanavyokula vichwa, ni aibu sana hawa askari, kwanza wana wivu pili wanadharau askari anamuuliza mtu eti unajitia uko kwenye kiyoyozi sisi maisha yetu juani
 
hivi ile taasisi ya kuzuia mirungura bado ipo kweli? au imebakia kibogoyo baada ya mama kuing'oa meno?
 
Mhh
Your browser is not able to display this video.
Your browser is not able to display this video.
 
Kuna Mwingine tupo hapa Sinza Mapambano jirani kabisa na Yard ya Mwanamboka, Mrefu Mweupe anakusanya Rushwa kama katumwa yaani. Hivi ninavyo andika katoka pokea rushwa ya 5000 kwa Kondakta wa Daladala ya Makumbusho Posta via Shekilango.
 
Unafikiri yeye anakosa mgao hapo?
 
Mkuu wapige picha kimya kimya afu uziweke humu au kuwaripoti sehemu husika, ili mamlaka wawafatilie na kuwachukulia hatua za kinidhamu.
Tena atumie camera ambayo sio ya simu. Maana ya simu wataanza kumtafuta
 
Niliyoyashuhudia leo mpaka moyo ulienda mbio. Nikfikiri nimepatwa na presha.

Kuna dereva mmoja wa bajaji alivyokuwa anampa yule askari konda bahati mbaya ikadondoka. Jamaa hakuogopa hata kuiokota
 
Ningekuwa Rais hiki kitengo cha trafiki ningewapa mamlaka ya kiraia. Polisi wanachafuliwa sana na hichi kitengo hovyo kabisa wanakula rushwa hovyo halafu virushwa vyenyewe 5k,10k.
Sio ndogo hizo akikusanya kwa watu 50x10000
alafu 50x5000 unapata ngapi hapo!?
 
Tena atumie camera ambayo sio ya simu. Maana ya simu wataanza kumtafuta
Ya ndo maana yake mkuu, maana kama watu hawajafanya kitu cha kuwaadabisha hawatokoma na wataendelea kuwasumbua raia kila siku.
 
Bongo watu wanaendesha magari kwa mateso

Ova
 
Tuulizane tu kwa uhalisia, je Polisi wakiacha kuchukua rushwa wakasimamia sheria utaweza kuendesha hilo gari lako? Je daladala zitaweza kufanya huduma zake?
Kwa uzoefu wangu hakuna dereva daladala anayelalamika kudakisha hizo 2000, huwa wanalia wanapoandikiwa faini ambayo ndio sheria yenyewe
 
Serikali ya kitu kidogo😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Zerro yuko bize kughushi RB ya Central kuonyesha makomandoo wa Mbowe walilala hapo na sio Tazara hana habari na Manzese
 
Nakubali.... Humu unakuta nusu wote hata leseni hawana ikiandikwa 30 barabara zitabaki nyeupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…