IGP Sirro, Tafadhali usiligeuze jeshi la polisi kama mob

Km hawakuomba kibali unamlaumu vipi IGP?
Ndg yangu, nadhani Katiba na sheria za vyama vya siasa zinasema Chama cha siasa kilichosajiliwa rasmi kinatakiwa kutoa taarifa kwa Polisi si chini ya masaa 48 kama kinataka kufanya mkutano wa hadhara. Lengo kulingana na sheria hiyo ni kutoa fursa kwa jeshi letu la Polisi kujipanga ili kutoa huduma nzuri ya ulinzi. Siyo kwamba jeshi la polisi linatakiwa kutoa kibali kwa Chama cha siasa kufanya Kazi zake. Na kwa vikao vya ndani sidhani kama kunatakiwa kutoa taarifa hiyo polisi kwani hakutakiwi kuwa na ulinzi wa polisi. Lakini polisi wanaweza kuingilia kama wataona kunaweza kuwa na tishio la uvunjifu wa amani sehemu yoyote.Lakini ni busara Kama hali hiyo ikitokea washauriane na na Chama husika na siyo kutumia tu ubabe.
 
Haya yataisha siku tutakaposhikishana adabu.
 
Polisi wasiwajengee watu tabia ya kutoogopa kukamatwa tukifika huko ni hatari watu awatoogopa tena,wataona ni sawa na kwenda chumbani tu
 
Chonde polisi. Musielekeze nchi kwenye visasi na machafuko. Tendeni haki kuifanya nchi ibaki salama. Ni "USHAURI" tu.
 
Vyeo hivi ni mzigo sana.

Sirro wa 2010 pale Nyamagana sio Sirro wa 2020.

Legacy zao zitawahukumu.
Sirro anafuata maelekezo tu mkuu isitoshe RC na DC huku mikoani ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi hivyo wanaweza kumuamrisha RPC au OCD kuzuia mikutano kama hiyo ya wapinzani.

Tatizo kubwa lipo kwa wanasiasa japo kuna baadhi ya polisi wamejigeuza wanasiasa kama njia ya kujipendekeza (Jonathan Shana).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…