Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Nimeileta hii kwa makusudi baada ya kutazama hiyo video hapo chini ya kina Mama wakijitetea kwa maafisa wa polisi juu ya kuondolewa kwao kwenye ukumbi wa starehe kwenye hafla yao.
Waliagizwa kuwa wazime muziki kwa sababu tunazozifahamu, lakini hoja kuu hapa ni kuhusu hawahawa maaskari kwa sisi tunaohudhuria baa na kumbi za starehe, huwa tunawaona wanakuja na gari zao na kupaki pembeni ya ukumbi kisa anakwenda meneja wa kumbi husika na kuwashikisha chochote kitu . Mara nyingi zitapita gari mbili au tatu kwa usiku mmoja. Kama Ndugu IGP halifahamu hili tungependa alifahamu. Na nitaomba uanzishwe uzi wa kutaja namba za hizo gari na Bar au kumbi waliyochukua mkwanja siku husika sababu zinafahamika.
Inashangaza kwa kweli kusahau maadili ya kazi zao lakini wanapokuwa na ajenda yao hujifanya kusimamia hichohicho wanachokihujumu.