IGP Sirro wa Tanzania amemuita haraka IGP wa Mozambique na kufika Mtwara jana na kuzungumza kuhusu mauaji ya wakulima 9 wa kitanzania waliokua Mozambique kwa shughuli za kilimo kisha kuuawa na kundi la kigaidi
IGP Sirro ametaka ufunguzi wa mpaka kati ya Tanzania na Mozambique kijeshi, hivyo sasa Tanzania itaingiza jeshi lake la police kwenda Mozambique kuwasaka hao wahuni, jeshi shupavu la police la Tanzania tayari lilishatuma majasusi wake Mozambique undercover na hivi sasa tayari wamo Mozambique kuanza show.
Itakumbukwa hawa wauaji ndio wale waliokua kwenye mapango ya amboni kule Tanga na Kibiti huko Pwani, waliuwawa kama kuku na jeshi shupavu na hodari la police, sasa wabaki kuvizia Watanzania waishio nchini Mozambique ili kulipa kisasi, Tanzania Police Force halitawaacha salama kamwe.