IGP wa Zambia ashindwa kumaliza kiapo kwa kutetemeka, nawaza angekuwa hayati Magufuli

IGP wa Zambia ashindwa kumaliza kiapo kwa kutetemeka, nawaza angekuwa hayati Magufuli

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Nchi ya Zambia baada ya mabadiliko ya chama tawala na Rais, wameamua kulifumua Jeshi la Polisi ikiwa ni kutekeleza ahadi ya Rais wakati akiomba kura. Katika hali ya kustaajabisha, IGP Remmy Kajoba alishindwa kumaliza kiapo baada ya mtetemo kuzidi wakati akiapa.

Rais Hakainde Hichilema alitoa busara ya kumuomba mtu mwingine amsomee kiapo kwa niaba yake na kukikamilisha.

Ghafla nikamkumbuka Naibu wa Waziri mteule wa Wizara ya Madini, Francis Kumba Ndulane enzi za utawala wa Magufuli alivyochemsha kusoma kiapo na kilichomkuta.

IGP Zambia.jpg
 
Picha tafadhali.
 
Zambia ni karibu na Sumbawanga kwa kina Hayati Chrisant Majiyatanga Mzindakaya
 
hap ndio wanasiasa wajanja huwapiga wananchi wanyonge.

huyu anawekwa watu wake watakaomtii,anadanganya kaondoa uozo.
kikawaida huwezifanya kazi na watu waliofanya kazi na utawala ulioutoa madarakani.
 
Biblia na matunguri kuna wakati vinatwangana hasa kwenye makamera mengi kama hayo
 
Huyu Kajoba alifukuzwa na Lungu 2015 kwa kuonewa sana akiwa amesimamia haki, leo alikua anatetemeka kwa kutokuamini kuwa kwamba amekua IG wa nchi
 
wanasaikolojia,wachungaji na watunguri tufahamisheni,shida nini?
 
Hii ndio tofauti ya Hichilema Rais wa Zambia na viongozi wengine wanoko wa kiafrica , hali iliyomkuta IGP wa Zambia iliwahi kumpata mmoja wa Wateule wa hapa Tanzania , sasa badala ya kusaidiwa kuapa Rais wa Tanzania wa wakati ule Dr Magufuli alitengua uteuzi wake bila huruma wala uungwana .

Hii ni tofauti na yaliyotokea huko Zambia leo ambako Rais aliomba wasaidizi wake kumsaidia kuapa IGP mpya aliyekumbwa na kitete wakati wa kuapa .

Hivi kumsaidia mtu kuapa hicho kiapo kitakuwa valid?

Nikiharibu kwenye majukumu yangu halafu nikisema sio mimi nilieapa mahakama inaweza kunifunga?
 
Back
Top Bottom