SALOK
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 3,364
- 2,001
Katika kipindi kifupi cha Uhudumu wa huyu IGP mpya, pengine changamoto kubwa aliyokumbana nayo katika utendaji wake ni kukithiri kwa matukio ya ajali za barabarani.
Matukio haya yamekwenda sambamba na upotevu wa roho za watanzania, nguvu kazi ya Taifa. Inasikitisha sana.
Licha ya ajali kuongezeka kila usiku uchao, bado hatuoni vyombo vinavyohusika vikichukua hatua za makusudi kuhakikisha matukio haya yanapungua kama si kukoma kabisa hususani Jeshi la Polisi tena likiwa na IGP mpya kabisa katika nafasi hiyo baada ya mtangulizi wake kuteuliwa kuwa Balozi Nchini Zambia ambaye katika kipindi cha uhudumu wake alifanikiwa kiasi kikubwa kudhibiti ajali za barabarani.
Matukio ya ajali za barabarani katika siku za hivi karibuni kwa Watanzania imekuwa ni chai ya asubuhi isiyokuwa na vitafunwa ambayo huishilizia kwa kuwaachia Watanzania maumivu na majeraha ya vifo na vilema!
Ni dhahiri kwamba Jeshi la Polisi hasa hasa Idara ya usalama barabarani imefeli katika hili, na hapa tunaanza kuiona dosari kwa Mteule IGP.
Japokuwa mara zote chanzo cha ajali husemwa ni mwendokasi na uzembe wa dereva.
By the way; Sisis tunatekeleza wajibu wetu, kukosoa na kushauri.
#TanzaniaSalamaInawezekana