IGP Wambura ampa Bajaji kijana aliyepoteza mguu wakati akipambana na uhalifu

IGP Wambura ampa Bajaji kijana aliyepoteza mguu wakati akipambana na uhalifu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilius Wambura, ametoa msaada wa Bajaji kwa kijana Masima Nyau kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi baada kujeruhiwa mguuni wakati akitekeleza majukumu yake ya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwenye oparesheni za kupambana na wahalifu hali iliyopelekea mguu huo kukatwa.

Akikabidhi msaada wa Bajaji hiyo kutoka kwa IGP Wambura kama ishara ya kutambua uzalendo wa kijana huyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi George Katabazi amefikisha salamu za pole kwa kijana huyo.

 
Back
Top Bottom