Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura, leo Julai 31, 2026, amezindua rasmi Call Centre ya Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Dawati hilo uliofanyika mkoani Dodoma.
Call Centre hiyo imeanzishwa ili kuboresha upokeaji na ushughulikiaji wa taarifa, malalamiko na maombi ya msaada kuhusu ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto nchini kote kwa wakati na kwa ufanisi.
IGP Wambura amewaasa Wananchi kutumia huduma hiyo kwa kupiga simu namba 0699 913 200 na kutoa taarifa, kuwasilisha malalamiko au kuomba msaada, ambapo taarifa zote zitafikishwa kwa watendaji wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto katika maeneo husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki na kwa haraka.
safi sana, taifa linalojali na kulinda haki ya mtoto na mwanamke limebarikiwa na Mungu, sasa dawati lifanye kazi kwa ufasaha wapewe funding na vitendea kazi pia ili kuwalinda watoto na wanawake wetu, the only positive thing so far ...