Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Kesi 1,840 zafutwa kwa kukosa ushahidi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali(IGP) Camilius Wambura, amesema kesi 1,844 ambazo zimekosa ushahidi wa kutosha kupelekwa mahakamani zimeondolewa, huku kesi zingine 2,117 zikifanyiwa mabadiliko.
IGP Wambura alikuwa akizungumza jana katika Shule ya Polisi Moshi(TPS), wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipokwenda kufungua Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi.
Pia alisema alisema takwimu za makosa makubwa ya jinai nchini zimeongezeka kwa kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu. Alisema makosa hayo yameongezeka kutoka makosa 24,848 kipindi kama hicho mwaka 2021 hadi makosa 27,848, sawa na ongezeko la asilimia 11.2.
"Ongezeko hili linatokana na jeshi la jolisi kufanya operesheni na misako mbalimbali kukabiliana na uhalifu. Jambo ambalo limesababisha ongezo la makosa hayo," alisema.
Alisema miongoni mwao makosa hayo ni watu kupatikana na mirungi, bangi, pombe haramu ya moshi, watu kukutwa na nyara za serikali, mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi, ushirikina, ulevi na migogoro ya ardhi.
Chanzo: Nipashe