The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Kila mtu alishangaa sana Rais Samia kuwapa nafasi hizo maaskari hawa (Camillius Wambura - IGP na Ramadhani Kingai - DCI)
Hawa ndiyo waliokuwa vinara wa kutengeneza kesi bandia ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA - taifa Mh. Freeman Mbowe mwaka 2020.
Tuliwaona walivyokuwa wababaishaji na wasio na uwezo wa kujitetea wala kujieleza mahakamani kutetea kazi mbaya ya akili na mikono yao wakiwa mashahidi wakuu wa upande wa mashitaka wa kesi ile maarufu ya "UGAIDI WA MBOWE mwaka huo..."
Watu hawa eti ndiyo wamepewa dhamana muhimu ya kuongoza jeshi la polisi Tanzania (TANPOL).
Yesu Kristo katika moja ya mafundisho yake anasema, mti wa mchongoma hauwezi kuzaa matunda ya zabibu na vivyo hivyo mzabibu hauwezi kuzaa miiba toka ktk mti wake.
Mtu mbaya na mwovu hawezi kuzalisha au kutoa kitu chema toka ktk matokeo ya kazi ya kazi ya akili na ufahamu wake.
Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na factors zingine nyingi, elewa tu kuwa, matukio yote haya ya utekaji, utesaji na mauaji ya raia wasio na hatia hapa nchini sababu kuu ni hawa watu IGP Wambura na DCI Ramadhani Kingai viongozi wako wakuu wa Jeshi la polisi ambao ambao wana "zero morals", incompetent na wao wenyewe hapo walipo ni wahalifu.
Anza na hawa, watoe katika nafasi zao kwanza. Unda tume huru ya kijaji kuchunguza mauaji haya chanzo chake, sababu na wanahusika.
Na wakati huohuo fanyia kazi recomendations na findings za ripoti ya Tume ya Haki Jinai uliyoiunda mwenyewe na kuongozwa na Jaji Mstaafu Athuman Chande kulisafisha na kuliunda upya Jeshi la polisi.