IGP Wambura, ukijiuzulu hutapungukiwa chochote zaidi ya kujiongezea Heshima mbele ya Jamii

Jina lako litaandikwa Kwa wino wa Dhahabu kuwa,

"Ni IGP pekee aliyejiuzulu Kwa kuchukizwa na kupotea Kwa wananchi anaosimamia kuwalinda kisheria".
 
Wew jamaa kuna muda ni kama akili huwa zinakuja na kusepa. Kama mtu anayetumia dawa so siku akisahau kutumia ndiyo hivyo tena unakuwa kama hivi
Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Tanzania kujiuzuru ni PhD ya D² ambayo haipatikani popote duniani, wale wanaojiuzuru kwa matakwa yao wenyewe hukute hana hasara yoyote kutokana na familia yake.

Vinginevyo hawa wengine ni ngumu sana sababu wanaona mfumo ulivyo mbovu hivyo ajiuzuru ili iweje na kwa sababu zipi?.

Nchi yetu bado sana kufika hapo kwa kiongozi kufanya madudu au aliye chini yake alafu atoke kirahisi tu!
.
 
Inawezekana,

Mbona juzi tu, Naibu waziri Mambo ya nje kujiuzulu?

Waziri wa Utalii Zenji alijiuzulu majuzi?

Ndugu Wambura ajiuzulu Ili kurudisha Imani Kwa polisi ambayo imekwishapotea.
 
Reactions: I M
Inawezekana,
Mbona juzi tu, Naibu waziri Mambo ya nje kujiuzulu?
Waziri wa Utalii Zenji alijiuzulu majuzi?

Ndugu Wambura ajiuzulu Ili kurudisha Imani Kwa polisi ambayo imekwishapotea.
Soma reply yangu vizuri uelewe mkuu, hata huyo naibu waziri nimeandika pale nk.
 
Kwa taarifa yako wakati wa dhalimu magu, huyu IGP ndio alikuwa kiongozi wa watu wasiojulikana. Ni bahati tu huyu mama sio muumini wa moja kwa moja wa udhalimu. Vinginevyo ingekuwa balaa.
 
Sio hulka yetu.
 
Kwa taarifa yako wakati wa dhalimu magu, huyu IGP ndio alikuwa kiongozi wa watu wasiojulikana. Ni bahati tu huyu mama sio muumini wa moja kwa moja wa udhalimu. Vinginevyo ingekuwa balaa.
Unaposema Si muumini unamaanisha nini ilhali watu wanapotea Yeye akiwa Rais na IGP hawajibiki Wala kuwajibishwa?
 
Reactions: I M
Unaposema Si muumini unamaanisha nini ilhali watu wanapotea Yeye akiwa Rais na IGP hawajibiki Wala kuwajibishwa?
Sio muumini wa moja kwa moja rejea hao, vinginevyo wangepotea wengi zaidi ya hawa. Sehemu kubwa ya huyu mama ni laghai, na muuza nchi, ila kwenye udhalimu hayupo. Hiyo mbinu anaitumia tu maana washauri wanamshauri hivyo, lakini sio kama alivyokuwa dhalimu magu.
 
Kwamba Mbinu hii anatumia sababu tu ya ushauri wa wasaidizi🤔

Hiki ulichoandika unakielewa?
 
Vipi asipojiuzuru unachukua hatua ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…