Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
IJP Camillus Mongoso Wambura ni Mkuu wa Jeshi la polisi, Jeshi ambalo uwepo wake ni kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama muda wote.
Lakini Jeshi la polisi ( si tu wakati yeye akiwa IJP) linapokuja suala la jinsi ya kusimamia mambo ya siasa, hasa haki za vyama vingine mbali ya CCM, Jeshi la polisi viwango vyake viko chini sana.
Jeshi la polisi limekuwa si sehemu salama kwa wanasiasa wa vyama vingine hasa CHADEMA linapokuja suala la vyama hivyo kufanya siasa kwa uhuru.
Nakumbuka wakati NCCR -Mageuzi ilipokuwa na nguvu kisiasa, polisi walikiandama sana chama hicho kwa kukamata viongozi na wafuasi wake na kuingilia shughuli mbali mbali za chama hicho.
Kuanzia mwaka 2000 wakati CUF ilipokuwa kinara za siasa za upinzania Tanzania hasa huko Zanzibar, CUF ilisakamwa Sana.
Na linapokuja suala la polisi kuwapiga wafuasi wa vyama vya siasa hasimu kwa CCM , huwa hawana huruma Wala kuheshimu utu wa watu.
Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa CHADEMA imekuwa ndiyo chama kinachokutana na madhila mengi Sana toka kwa Jeshi la polisi.
Swali la kujiuliza, jee polisi wanaichukia CHADEMA, au polisi ni sehemu ya CCM hivyo CCM ikizidiwa kisiasa na wenyewe polisi wanakuwa kama na wao wanaathirika?
Jeshi la polisi kwa maneno na matendo limeonesha kuwa lenyewe CHADEMA kwao ni raia wenye hadhi duni kuliko watanzania walioko CCM. Lakini chanzo ni nini?
Hapa chini nimeweka video ya Zembwela na Maulidi Kitenge wakiuliza maswali ya msingi Sana kuhusu polisi na utendaji kazi wao Kwa CCM na dhidi ya vyama vingine.