Jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wassira aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Chadema kimepanga mpango huo wenye lengo la kuwaandaa wanachama wake waone wameibiwa kura pindi CCM kitakapotangazwa mshindi.Tunazo taarifa za uhakika kuwa wamepanga kutumia magari ya matangazo kutangaza kuwa Chadema imeshinda, hata kabla ya kura kuhesabiwa ili wapate leseni ya kuanzisha vurugu, alisema Wassira.
Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), alisema tayari CCM wameviarifu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchukua hatua na pia kuwaelimisha na kuwasihi wananchi kutoingia katika mtego huo.
Lengo ni kuwaharibu vijana kisaikolojia kwamba yakitangazwa matokeo tofauti waone wamechakachuliwa kura zao na CCM. Tunawasihi Chadema na wanachama wao watulie wakati wananyolewa, alisema Wassira.
Wassira alisema wanakusudia kutumia mikutano ya hadhara ya kampeni iliyobakia wiki hii ya lala salama, kuwaeleza wananchi juu ya mpango huo wa Chadema ambao alidai hauwatakii mema wananchi wa Igunga.
Kwa maneno haya ya Wassira nahisi kuna harufu ya uchakachuaji...