Elections 2010 Igunga: Helkopta 2 za CCM zatua

Kuna kipindi nakuamini kuna kipindi sikuamini vile vile tehe tehe tehe tehe. Naona umepita na magamba kwa spidi shaaaah, wakisoma hii comment yako watatamani wajinyonge tuu.
 
Natabiri Helicopter 1 ya CCM itaanguka kabla ya Kufika Jumamosi jioni ikiwa na Makada maarufu wa CCM ndani yake...Hilo ni angalizo tu wawe makini sana.
 

Hivi mkuu phase-1 iliishakamilika siyo. Yaani yule dogo hata hawakumhitaji mkwenye hii shughuli.
 
Jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wassira aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Chadema kimepanga mpango huo wenye lengo la kuwaandaa wanachama wake waone wameibiwa kura pindi CCM kitakapotangazwa mshindi.“Tunazo taarifa za uhakika kuwa wamepanga kutumia magari ya matangazo kutangaza kuwa Chadema imeshinda, hata kabla ya kura kuhesabiwa ili wapate leseni ya kuanzisha vurugu,” alisema Wassira.

Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), alisema tayari CCM wameviarifu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchukua hatua na pia kuwaelimisha na kuwasihi wananchi kutoingia katika mtego huo.

“Lengo ni kuwaharibu vijana kisaikolojia kwamba yakitangazwa matokeo tofauti waone wamechakachuliwa kura zao na CCM. Tunawasihi Chadema na wanachama wao watulie wakati wananyolewa,” alisema Wassira.

Wassira alisema wanakusudia kutumia mikutano ya hadhara ya kampeni iliyobakia wiki hii ya lala salama, kuwaeleza wananchi juu ya mpango huo wa Chadema ambao alidai hauwatakii mema wananchi wa Igunga.


Kwa maneno haya ya Wassira nahisi kuna harufu ya uchakachuaji...
 
Hizo Helcopter za kichina zimeshatua au bado zinasubiri kibali au zinasubiri masanduku hewa yaliyopigwa kura?
 


Kweli tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…