Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE NGASSA: "TUNATENGENEZA BARABARA ZA KUUNGANISHA KATA NA KATA KWA AJILI YA KUFUNGUA UCHUMI WA VIJIJINI"
"... Mwaka huu wa Fedha Tumeweka msisitizo kutengeneza Barabara zinazounganisha Kata Moja kwenda Kata ingine kwa lengo la kufungua na kukuza uchumi wa vijiji vyetu..."
".... Dunia ina kwenda kasi na Sisi hatuna budi kukimbizana na mabadiliko ya uchumi wa Dunia. Ni vyema kuwa na muunganiko kutoka mashambani, viwandani na masokoni..."
"... Uchumi wa Soko huria unahitaji tugangamale kweli kweli, tusibweteke na kile kidogo tunachozalisha. Tuumize vichwa kuongeza uzalishaji mali kwenye Kilimo, Ufugaji na Viwandani..."
Nicholaus George Ngassa
Mbunge wa Jimbo la Igunga