NI KUTOKA KATIKA VYAMA VITATU TOFAUTI VYA SIASA wanasiasa wanane wamejitokeza kuwania ubunge jimbo la igunga wakiwamo watatu wa chadema, wanne ccm na mmoja wa cuf. mkurugenzi wa sera na utafiti wa chadema waitara mwikabe aliwataja waliojitokeza kuwa ni Gidion kwandu, Anuary kashaga, na katibu mwenezi wa chama hicho Erasto Tumbo.
Alisema milango bado ipo wazi kwa mwanachama yeyote anayetaka kugombe ambapo mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 18 august saa 10 jioni. kwa upande wa ccm katibu wa ccm wilaya hiyo, Neema Adamu alisema pamoja na Amina fundikira wengine ni shamshu Ibrahim, Adam kamange na Ngasa George, mwisho wa kuchukua fomu ni Agosti 13 saa 10 jioni.
Kwa upande wa chama cha wanainchi cuf taarifa zilizopatikana mjini igunga zilieleza mgombea aliyeshindwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi uliopita ndiye atakayesimama tena katika uchaguzi huu.
Ni kweli mimi ndiye mgombea tena wa chama changu kimenipendekeza mwisho wa wiki baraza kuu watatoa taarifa, alisema mgombea huyo Lukas mahona. wanasiasa hao wanagombea jimbo hilo baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz kuachia ngazi kwa madai ya kuzidiwa na siasa uchwara.