IGUWASA yatoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mdau aliyehoji utendaji wa Mamlaka hiyo

IGUWASA yatoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mdau aliyehoji utendaji wa Mamlaka hiyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
TAREHE: 9 JUNI 2026

TAARIFA KWA UMMA: KANUSHO LA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZINAZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) imebaini kuwepo kwa taarifa mbalimbali zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii zenye lengo la kupotosha umma kuhusu shughuli na utendaji wa Mamlaka.

Uongozi wa IGUWASA unapenda kuufahamisha umma, wadau na wateja wake kuwa taarifa hizo si sahihi na haziakisi hali halisi ya utendaji wa Mamlaka.

logoo (1).png

Hoja ya Mdau ~ Watumishi wa Mamlaka ya Maji Igunga (IGUWASA) tunaomba ufanyike uchunguzi dhidi ya ofisi yetu, mambo hayapo sawa

Tunawaomba wananchi kuzipokea taarifa hizo kwa tahadhari na kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia njia rasmi za mawasiliano za Mamlaka.

Tunawashukuru wateja wetu na wadau wote kwa ushirikiano wanaoendelea kutupatia, na tunawaomba waendelee kuwa na imani na Mamlaka huku wakipuuza taarifa za upotoshaji zinazolenga kuleta taharuki au kuharibu taswira ya taasisi.

Imetolewa na:
Tarehe: 9 Juni 2026
KITENGO CHA MAHUSIANO NA MAWASILIANO
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA)
 
Back
Top Bottom