Ihefu yauchagua kutumia uwanja wa CCM Liti wa Singida kwa mechi zao za nyumbani

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
RASMI Ihefu SC imehamia mkoani Singida baada ya kuuchagua uwanja wa CCM Liti kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu mzima.

Leo watendaji wote wa timu za ligi kuu wametumiwa taarifa rasmi ya kuwa michezo yote ya nyumbani ya Ihefu SC itachezwa CCM Liti, Singida.

Nini kimejificha kwenye sakata la Singida na Ihefu? Mbona kama siasa mchezoni hizi?
 
Nilisema hili lingekuja kutokea. Imebaki sasa kwa SFG kufanyiwa figisu za kuwatimua kutoka Singida.


Kuna kuogopa wanasiasa walio nyuma ya hili sakata kiasi kwamba sheria na kanuni zinazohusiana na umiliki na uuzaji wa timu na wachezaji zimefumbiwa macho. Mpaka sakata hili liishe tutaona na kusikia mengi.
 
Dahhh! Wanasiasa wataua football ya Tanzania, Nchemba ana uhuni sana huyu jamaa. Kahamishia wachezaji wake wote Ihefu baada ya kuinunua. SFG inaenda kufa.
 
Dahhh! Wanasiasa wataua football ya Tanzania, Nchemba ana uhuni sana huyu jamaa. Kahamishia wachezaji wake wote Ihefu baada ya kuinunua. SFG inaenda kufa.
Uhuni wa waziwazi. Watu wa Fountain Gates wameingia cha kike. Natamani waamue kupambania haki zao, liwalo na liwe
 
Timu ya maderu inarnda kuweka masikani kalibu na kwao Kila lenye heri
 
Duh uhuni wa wazi....timu iitwe ihefu halafu maskani yawe Liti- Singida?!
 
Ihefu ikija kuifunga yanga tena nipigwe ban ya maisha hunu jf,over.
 
Wakome kutumia majina ya Mbeya hao mafala kuanzia Ihefu na Mbeya kwanza zitumie majina ya hao waliozinunua.
 
na singida fountain gate wamechagua uwanja wa ccm kirumba.......[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…