Ijue deed poll (nyaraka inayotumika kubadilisha jina la mtu)

Ijue deed poll (nyaraka inayotumika kubadilisha jina la mtu)

tabibumtaratibu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2011
Posts
2,414
Reaction score
1,215
Deed Poll Ni nini?

Ni nyaraka ya kisheria inayotumika kubadilisha jina la mtu. Nyaraka hii hua inasainiwa na mtu ambaye anabadilisha jina pekee tofauti na nyaraka nyingine za kisheria ambazo zinasainiwa na watu wawili mfano Mikataba. Nyaraka hii kwa kawaida inashuhudiwa na kamishna wa viapo ambae ni hakimu au wakili.

Kwa nini Ubadilishe Jina?

Kisheria huwa ni halali mtu kubadilisha jina. Na baadhi ya sababu za kubadilisha jina zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Ndoa-Mtu ameolewa anataka achukue jina la mwisho la mke au mume wake.

2. Dini- Mtu amebadilisha dini ikapelekea kubadilisha jina lake.

3. Ulikua unatumia majina matatu mfano Jua Kali Halishi ukataka utumie majina mawili tu Jua Halishi

4. Kuna mkanganyiko wa majina kwenye nyaraka zako za kudumu mfano jina la kwenye cheti cha kuzaliwa ni tofauti na la kwenye cheti cha shule.

5. Nakadhalika.

Ufanyeje ili mabadilisho yako ya jina yatambulike kisheria?

Unatakiwa uwape(ule kiapo) kwa kutumia deed poll (nyaraka ya kubadilishia jina). Hivyo basi fika kwa hakimu au wakili yoyote ataandaa nyaraka hii kwa kumpa taarifa zako mwisho utatia sahihi yako na wakili au hakimu atashuhudia na kugonga muhuri wake kwenye deed poll aliyoiandaa kwa ajili yako.

Baada ya kupata deed poll ufanyaje?

Kwa mujibu wa sheria, deed poll inatakiwa isajiliwe na msajili wa nyara
ka ili iwe halali na uweze kuitumia sehemu mbalimbali mfano kwenye maombi ya passport, kuomba mkopo, kazi, mafao ya kustaafu nk. Hivyo Basi baada ya kupata deed poll yako unatakiwa uipeleke kwa msajili wa nyaraka (registrar of documents) ili iweze kusajiliwa na kutambulika katika matumizi mbalimbali.

Jinsi ya kusajili deed poll

Kipengle hiki kitaelezwa kwenye toleo lijalo. Usiache kusubscribe/follow na kushare ili uwe wa kwanza kujua jinsi ya kusajili deed poll na ntakuwekea na sample ya deed poll uweze kuiona.
 
me nakwambia inawezekana, kama umebadilisha jina kwa deep poll na ukaisajili kabisa unaenda nayo mamlaka walio toa cheti unaandika barua unaambatanisha unalipia fees then wanabadilisha. nishafanya sana ii kazi.
Je, wanaweza kubadilisha jina hadi kwenye certificates za O level? A level? Chuo..? Etc. Kama inawezekana, nitakuwa mteja wako.
NB. Vyeti original visome my new name, sio nipewe karatasi pembeni za utambulisho
 
me nakwambia inawezekana, kama umebadilisha jina kwa deep poll na ukaisajili kabisa unaenda nayo mamlaka walio toa cheti unaandika barua unaambatanisha unalipia fees then wanabadilisha. nishafanya sana ii kazi.
Vyetu vya shule havibadilishwagi
 
Back
Top Bottom