Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.

Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.

Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.

Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.

Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.

Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.

Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.

Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.

Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
  1. Hadhi ya Ubalozi ni nini?
  2. Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
  3. Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
  4. Privileges za diplomatic status ni zipi?.
  5. Ijue diplomatic immunity
  6. Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
  7. Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
  8. Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
  9. Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
  10. Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
  11. Ijue diplomatic Bag?
  12. The Doctrine of Diplomatic Reciprocity
  13. Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
  14. Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
  15. Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
  16. Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, as a local staff na kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America, atawaletea visa na mikasa mbalimbali ya balozi zetu mbalimbali.
 
Damage control!
 
Noted but hayo uliyasema kibongobongo hayatekelezeki ,Kwa mfano Sheria za vyombo vya habali zipo wazi uhuru ,mipaka yao nakadharika lakin mbona Huwa waziri au kiongozi yeyote anaweza piga mkwala taarifa frani itoke au istoke

Slaa ni kweli ana hadhi ya ubalozi kibongobongo hata Kama ikidhibitika Hana hatia hawez rudishwa ubalozini.
 
Mimi sio mshauri wa yoyote, ni mtu tuu mwenye ufahahamu wa issues za kidplomasia hivyo kujitolea kuelimisha watu humu kuhusu mtu kufutiwa hadhi ya Ubalozi Hakutokani na Ukosoaji, bali kufutiwa kule ni Zinduna tuu, Ambari iko nyuma...
P
Brother Mayalla sikukatalii bali nakazia tu kuwa ndani ya ccm lolote linawezekana tu.
 
Brother Mayalla sikukatalii bali nakazia tu kuwa ndani ya ccm lolote linawezekana tu.
Hadhi ya Ubalozi has nothing to do with CCM, tena usikute hata Rais has nothing to do with Dr. Wilbroad Slaa, lakini kwa vile Rais ndio mamlaka, amelazimika kutimiza wajibu wake ili mambo mengine yaendelee, ikukutikana sio kweli na hahusiki, anarejeshewa Ubalozi wake!.
P
 
Kwa hiyo unataka tuamini kwamba kufutiwa hadhi yake ya Ubalozi haihusiani na ukosoaji wa serikali ya mama SSH? Bro, haya mambo mengine hayahitaji shahada ya sheria au PhD. Yapo wazi. Why him and not someone else?
reality is: hivi vyeo vya kupeana kirafiki au kwa vile mtu amekufurahisha, hata kunyanganywa…..ni hivo hivo.

Kwa Tanzania yetu survival ya mtu kwenye mfumo ni matakwa ya watawala. Ndo maana kila mtu ni muoga kusema au kufanya lolote lenye mlengo tofauti na watawala.

Hata mtu akiangalia uchambuzi wako, your perspective is telling.

Wasalaam,
 
Hizo ni Sheria za umoja wa mataifa au ?
 
Mimi sio mshauri wa yoyote, ni mtu tuu mwenye ufahahamu wa issues za kidplomasia hivyo kujitolea kuelimisha watu humu kuhusu mtu kufutiwa hadhi ya Ubalozi Hakutokani na Ukosoaji, bali kufutiwa kule ni Zinduna tuu, Ambari iko nyuma...
P
Tanzania sheria zinatekelezwa kutokana na utashi wa kiongozi aliye madarakani na genge lake. Hata uorodheshe vipi matakwa ya kisheria ya ubalozi, bado utekelezaji utafuata mtazamo wa kiongozi na genge lake. Hivyo utakacholeta ni story za furahisha genge.
 
Asante sana Kwa Elimu nzuri.Huyo Babu aandae mawakili tuu na uzuri umeshaeleza kwamba sio wa kwanza kuvuliwa Ubalozi na umewataja wengine kibao.
 
Utanikuta St Peter bechi la kati kati ,upande wa kusini
 
Ule mkataba wa kihuni wa bandari alioingia Samia kwa kukiuka sheria za nchi, ndio umemfanya Dr. Slaa avuliwe hadhi yake ya ubalozi, hapa usipindishe maneno.

Samia kwa kumvua Dr. Slaa hadhi yake ya ubalozi amethibitisha yafutayo..

- Amevunja Katiba ya JMT 1977 inayotoa ruhusa kwa watanganyika kutoa maoni yao ilimradi wasivunje sheria za nchi, na amefanya hivyo kama alivyovunja sheria nyingine za nchi kwa kuruhusu ule mkataba wa hovyo wa bandari.

- Amejipambanua yeye ni kiongozi mwanamke dikteta asiyetaka kukosolewa.

- Ametuonesha ana kikundi chake cha wajinga wachache anaowapa vyeo kila wakitetea ujinga wake, akidhani anatukomoa, kumbe ndio anazidi kujivua nguo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…