Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

VIENNA CONVENTION 1961 inaanza kumlinda mtu huyo, yaani anapata upendeleo & kinga (privileges & immunity) za KIDIPLOMASIA.

Lakini, KINGA hii inaweza kuondolewa kwa muda, na wakati wowote na nchi yake (sending state) – inaitwa "WAVER"; Article 32 ya VIENNA CONVENTION, 1961. Isipokuwa, "WAVER" hutokea tu pale ambapo "receiving state" inapeleka maombi kwa "sending state" kwamba Balozi aondolewe KINGA ili atoe ushahidi mahakamani, akamatwe au ashtakiwe kwa kosa la jinai (under the local criminal jurisdiction). Nchi ya kituo cha kazi cha Balozi haiwezi kumnyang'anya Balozi kinga au haki hizo za KIDIPLOMASIA kama Balozi huyo si raia wake.

Hata hivyo, Balozi akimaliza muda wake wa utumishi nje ya nchi yake, au kama amerudishwa nyumbani (recall), pale tu anapoondoka kwenye nchi ya kituo chake cha kazi, anapoteza KINGA hiyo; Article 39(2) ya VC. Lakini, bado mtu huyo ataendelea kutambulika na hadhi ya Kibalozi anaporudi nyumbani. Ataitwa "Balozi mstaafu", kama anavyoitwa Rais au Waziri au Jaji mstaafu.

Under common law jurisdiction & Diplomatic law, Rais Samia ana MAMLAKA ya kumwondolea mtu "immunity" ili ashtakiwe kwa kosa la jinai, lakini Rais hana mamlaka ya kufuta "HADHI YA UBALOZI" wake kwa sababu hadhi hiyo inatokana na sheria za Kimataifa na Rais Samia hajapewa UWEZO wa kuingilia sheria hizo, isipokuwa tu kama sheria hizo zingetamka wazi! Kwa VIENNA CONVENTION ya 1961, au sheria zingine hazijatoa mamlaka hayo kwa Rais wa nchi yoyote.

Hakuna, kwenye sheria zetu za ndani au za Kimataifa umewekwa utaratibu wa kunyang'anya hadhi ya Ubalozi ya mtu, isipokuwa tu kumwondolea kinga ili ashtakiwe kwenye mahakama za nchi ya kituo chake cha utumishi. Hili suala hapa nyumbani, linafanyika KISIASA tu.

Hivyo, kwa msimamo huu wa kisheria, Dr. Willibrod Peter Slaa
 
Hii inaitwa jino kwa jino
 
Kaka Paskali, asante kwa hili. Mimi ni mmoja wa wanaosubria kwa hamu elimu hiyo..!!
 
Kama nimekuelewa kaka itoshe kusema bwana Slaa bado ni balozi

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo wewe ndiye mshauri wa rais wa JMT?
Hivi sisi hatuna mwanasheria mkuu? Hatuna inside political analysts and advisers? Au washauri wetu wako nje ya mfumo? Mbona vitu vinafanyika halafu vinakuja kuonekana sheria zimekiukwa then unasikia mabadiliko.
Chukua mfano wa suala la ukodishwaji wa bandari. Tunapeleka timu ya wabunge dubai kujifunza na kuona uendeshaji wa DPW, tunarudi bungeni kuja kuridhia mkataba ambao ulishasainiwa tangu mwaka jana! Mfano Bunge lingesema (unless ilishapangwa) tubadilishe baadhi ya vipengele, ingekuwaje?
Suala hili hili tena, mkataba umeshasainiwa lakini tukajikuta kumbe kuna sheria ya ulinzi wa rasilimali inakinzana na baadhi ya vipengele vya mkataba.
Turudi kwenye mada, Dr Slaa amekamatwa na kushitakiwa kwa uhaini, tunakuja kugundua baadae kumbe alikuwa na hadhi ya ubalozi na alitakiwa avuliwe kwanza! Hatukuwa na watu wa kuyaona haya? Wewe umesoma sheria, au inatumika reversal kwa mtu kujipinga mwenyewe baada ya kutoa maamuzi ya awali?
 
Kuwa na hadhi ya ubalozi siyo ajira. Usifananishe kama mtumishi wa umma anapokuwa na jinai, anasimamishwa utumishi, kesi ikiisha, hana hatia, automatically anarudi na utumishi wake. Ubalozi haurudi automatic, ni mpaka impendeze mwenye mamlaka ya uteuzi, nieona nikuweke sawa kdg hapo
 
Angalia pia waliounga mkono suala la bandari. Utaona kwenye mabadiliko ya baraza
 
Elimu za kuunga sana kaka
 
Mimi sio mshauri wa yoyote, ni mtu tuu mwenye ufahahamu wa issues za kidplomasia hivyo kujitolea kuelimisha watu humu kuhusu mtu kufutiwa hadhi ya Ubalozi Hakutokani na Ukosoaji, bali kufutiwa kule ni Zinduna tuu, Ambari iko nyuma...
P
Mkuu Pascal ninamaswali mengi kuhusiana na UBALOZI nafikiri mpaka mada inaisha nitakuwa nimeipata majibu
 
Ibada njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…