The hammer,
Dingiswayo,
Sendoro Mbazi,
Queen Esther,
Nguruvi3,
nimeangalia matokeo ya shule za Same na Mwanga kwa kweli utatamani kulia. wilaya zetu hazikubahatika kuwa na maliasili kama wilaya nyingine za tanzania. elimu ndiyo iliyotuwezesha wenyeji wa same na mwanga kuwa na mchango katika nchi hii. katika mkoa wa KILIMANJARO wilaya ya Same ndiyo inashika mkia kwa kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa. miaka ya zamani, enzi wa wilaya ya Pare, tulikuwa tunaongoza katika masuala ya elimu. Kwa kweli katika mazingira haya itachukua miongo mingi sana kuwapata wakina Elangwa Shaidi, Abdulrahman Msangi, Akili Danieli,Nassoro Mnzava, Mishael Muze, Mahamoud Mwindadi, Keto Mshigheni,na wasomi wengine wa kupigiwa mfano. ninasema hivi kwasababu wasomi wote hao walitokea vijijini ambako miaka hii kumekuwa na hali mbaya mno. kwa kifupi wilaya zetu zinarudi nyuma badala ya kusonga mbele.