Ijue historia ya soko kuu la Kariakoo

Historia Mujaraaabu kabisa! Safi sana. Nimeipenda
 
nafikiri nyerere ndiye aliyepewa sababu hakuwa na kazi baada ya kuacha kazi ya uwalimu kwa ajili ya siasa,ukiwasoma akina dosa aziz na tewa said tewa walivojitoa na uhuru na namna walivoishia..wala hushangai ukiambiwa palikua panasikika kelele za kuogofya kwenye kaburi la mwalimu
 
Utafuti hupingwa kwa tafiti, anzisha uzi wako tuone mapungufu ya huu uzi ili tuongeze maarifa.
 
Ebu kazia hapo chini mkuu
 
Hao akina Dosa Aziz na Tewa Said Tewa waliishiaje mkuu? Nahisi kama vile waliishia pabaya kwa kutendwa na Nyerere.
 
Kutokana na kusoma mabandiko kadhaa yahusuyo historia ya Mzizima na viunga vyake kuhusianishwa na mapambano ya uhuru wa nchi hii, nachelea kusema kuna mengi yamepindishwa na kufichwa dhidi ya historia ya ukweli halisi ya mapambano hayo.
 
Figiri kwaajili ya kupunguza gesi tumboni!! [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Unazijua nyumba za kariakoo enzi hizo
Mm niliiona moja mwaka 2000 imejengwa kwa miti emeezekwa kwa makuti
 
Amini usiamini wanaume wa Dar Es Salaam ndo walioleta Uhuru wa Tanganyika...!Nimetoka nje ya mada....Dar ndo sehemu iliyoanza kujanjaruka na itaendelea kujanjaruka milele na milele licha ya figisu zinazopigiwa...I Love Dar
 
Vipi kuhusu jengo la Rupia lililopo karibu na kituo cha mabasi Msimbazi? Umemuacha kusudi au umemsahau?
 
Unawezaje kutaja historia ya kariaoo bila kumtaja mzee na tajiri John rupia??au kwa kuwa mgalatia??

Mi nashindwaga kuelewa ina maana kariaoo ni gerezani tu??na Lumumba?

Mzee john rupia akimilikia ghorofa kadhaa kwenye kona ya msimbazi na Uhuru. Na inasemekana ndiye aliempa nyerere nauli ya kwenda UN.unaachaje kumtaja??

Kariaoo mitaa ya misheni kota,magira,muhonda,likoma,ndanda ndiyo mitaa ya wazee wetu kina John rupia,kina mzee kiame na kanisa katoliki tangu kabla ya uhuru lipo kariakoo misheni kota.

Ila wafia dini hawataki kusema ama kwa sababu zao ama kwa kuu uhadaa uma..ionekane wakristu hawaku shiriki
 
Unaposema viazi mviringo vilikuwa haviliwi si sahihi labda imetokana enzi hizo wenyeji wa Dar kutosafiri kwenda mikoani, mikoa ya nyanda za juu kusini viazi hivyo vipo enzi na enzi vinajiotea hovyo kutokana na umande wa baridi na mvua.
 
Naona ni mashekhe tu ndio waliokuwa wakiishi mjini na kuanzisha mipango mbalimbali ya kimaendeleo.
 
Raba za Bata ziliitwa Twiga zilikuwa imara sana na hivyo vya mpira BataTanga vilipendwa sana na washihiri waliokuwa wakipita mitaani kukopesha nguo (enzi hizo matapeli hawakuwapo) toka Uajemi wakija kwa majahazi. Umenikumbusha wali kima (wali nyama ya kusaga) kwenye hoteli za washihiri na lifti pekee Dar ya kamba pale Mnazimmoja Uhuru na Bibititi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…