Ijue kesho leo: Sayansi ya mchezo wa Simba na Raja hii hapa

Ijue kesho leo: Sayansi ya mchezo wa Simba na Raja hii hapa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Mchezo wa Simba na Raja Leo!

Saa 1:00 kipyenga cha mwamuzi kitapulizwa! Mpira utakuwa wa kasi na tahadhali nyingi!

Simba watashambulia kuanzia dakika ya 1~20 ya mchezo!
Kipindi hiki ndicho muda pekee wa simba kutwaa ushindi Leo! Nguvu ya ulimwengu itawasaidia simba kupata ushindi kwa muda huo!

Endapo watakituliza kichwa watafunga magoli mawili, na mchezaji atayefunga goli ni miongoni mwa wachezaji watakaotanguliza mguu wa kulia wakati wakiingia uwanjani!

Miongoni mwa wachezaji watakaokuwa na bahati nzuri sana katika mchezo wa Leo ni shomari kapombe, Boko, kibu Denis, Baleke, Chama na Kennedy! Baraka za timu kwa siku na muda wa Leo zitabebwa na miongoni mwa watu hawa!

Baada ya dakika 20 kufika!
Mchezo utapoa na nguvu ya wachezaji wa timu zote mbili utalingana ! Hiki kipindi yoyote anaweza kufungwa either simba au raja!
Baada ya dakika 20 kupita simba wawe making sana maana hawatakuwa na msaada katika nguvu ya ulimwengu (itakuwa fair play yaani yoyote anaweza kufunga kwa maana simba wanaweza kuongeza goli kama watakuwa wamefunga awali, lakini hikohiko kipindi RAJA wanaweza kufunga goli la kizembe sana ambalo SIMBA wasipotulia watapoteana mchezoni)

Baada ya saa mbili kamili kupita!

Kipindi cha pili kitaanza! Simba itakimbizwa sana, Raja watashambulia kwa kasi sana, kipindi hiki cha pili simba wawe makini sana!
Lakini Raja watakosa sana magoli hata Yale ya wazi!
Watashambulia kipindi cha pili lakini bahati ya kufunga hawatakuwa nayo! (Ingawa wanaweza kubahatisha kufunga baada ya majaribio mengi)

Udhaifu wa simba unaweza kupenya kupitia kwa Inonga, Hivyo mchezaji huyu acheze kwa tahadhali kubwa maana anaweza kuighalimu team kwa leo! (Uchochoro wa kushindwa)

Miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa kwenye hatari ya kuumia wasipokuwa makini kwa Leo ni Manula, phiri, zimbwe, mzamiru, juma salim au guattara hawa wawe makini wasijelaumiwa (possibly to risky)

Simba watatamani refa amalize mpira!

Simba wasipotumia dakika 20 za kwanza Leo ushindi wa hiyo gemu wasahau! LAKINI kama watakuwa makini GEMU hii wanachansi kubwa ya kuimaliza mapema sana yaani (dakika 20 za kwanza SIMBA Itapata ushindi)

Nimewapa hii sasa ni saa sita mchana (12.01) kabla mechi kuanza!
Viongozi wa simba mliomo humu mwenye masikio na macho asome! Nitarejea! Baada ya mechi
 
Sasa ndo umetabiri Nini hapo, eti raja watashambulia sana lakini hawatafunga ila wanaweza kufunga baada ya majaribio mengi, ndo Nini sasa hapo

Upuuzi tu
 
Unawahi golini kufunga Mpira umeuacha nyuma.

Subiri dk 90.
 
Kwahiyo baada ya huo muda Dakika zitakazo bakia ni za Raja
 
Sasa ndo umetabiri Nini hapo, eti raja watashambulia sana lakini hawatafunga ila wanaweza kufunga baada ya majaribio mengi, ndo Nini sasa hapo

Upuuzi tu
Nimeeleza sayansi ya mchezo timing to win or loose!
Mchakato wa ushindi au kushindwa kwa silaha gani ni kama mammlaka ya hali ya hewa! Nimekupa data kwamba mvua itanyesha either ya kawaida,ya upepo, ya mawe, radi au ngurumo kwa majira na nyakati
 
Kwahiyo baada ya huo muda Dakika zitakazo bakia ni za Raja
Baada ya saa mbili kamili kupita RAJA watakuwa na nguvu sana lakini ushindi wao utategemea uzembe mkubwa wa simba!
Watashambulia lakini hawatakuwa na bahati ya kufunga! Watakosa kizembe but katika majaribio mengi yasipozibwa na simba watafunga!
 
Vigagula kwa mbwembwe hamjambo. Simba ipi ya kumfunga Raja? Boko, kibu, jeni bakuli, au yupi?
 
Back
Top Bottom