Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Sasa had kijiko cha dhahabu na nyumba ya dhahabu...hata siwez enjoy....kwanza kwangu dhahabu siipi uthaman mkubwa kwamba kila kitu kikiwa cha dhahab nitakua plzd No big no
 
Dah kwel huko uraia tutapata kwel maan kunamamb mazur japo wanavi2 viwili tu lkn cc tunavitu vyote bado tunakosa vi2 vyote
 
79f7f58663a088142e9daea071a94169.jpg



1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu.

Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.

GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....

2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).

Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.

3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali

4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................

5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk..........

7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali

8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)
hii habar mkuu ni kama tamthilia nlkua nasoma maudenda yananitoka hamu ya kwenda huko imejaa pomoni ee mola nipeleke huko
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] bongo mtu akimiliki milioni 100 anajiita milionea
hata hivyo ukisoma tafsiri ya millionea au billionea utaona hata local currency ya mahala husika inatambulika kukupa hadhi hiyo ingawaje inapaswa kubainisha ni bilionea au millionea wa pesa ipi inapokuwa other than usd!!
 
iko bara gani mkuu tukaombe uraia?
Brunei is a tiny nation on the island of Borneo, in 2 distinct sections surrounded by Malaysia and the South China Sea. It's known for its beaches and biodiverse rainforest, much of it protected within reserves. The capital, Bandar Seri Begawan, is home to the opulent Jame’Asr Hassanil Bolkiah mosque and its 29 golden domes. The capital's massive Istana Nurul Iman palace is the residence of Brunei’s ruling sultan.
 
Mkuu haujaelezea jambo muhimu sana. Namna ya kupata uraia wa huko na upatikanaji wa viza.. MUHIMU SANA UTUFAHAMISHE NA HILO MKUU.
Ni kweli muhimu hilo nchi ina watu 417,784, kuomba uraia hapa ni sawa kabisa ili twende tukajaze nchi hiyo!!
 
hata hivyo ukisoma tafsiri ya millionea au billionea utaona hata local currency ya mahala husika inatambulika kukupa hadhi hiyo ingawaje inapaswa kubainisha ni bilionea au millionea wa pesa ipi inapokuwa other than usd!!
Nnachojua jua ili uwe millionaire lazima umiliki pesa yenye thamani ya dollar M1 na kuendelea.
 
Back
Top Bottom