Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Ijue kwa undani nchi ya Brunei ambako Raia hawalipi kodi ni kula bata tu

Na yule mfalme nasikia anawachapa mamiss balaa na akiamka asbhi $100000 unasepa zako
Huyo mfalme anapiga bia kama hana akili nzuri!...ila yeye anakataza raia wake kutumia...

Kazi yake kuwala akina Beyonce, Mariah Carey, Pamela Anderson etc kwa pesa chafuu, sema mle kwenye Kasri wanaingia kwa siri mno..
 
wabongo tutaishia kusoma story Kama iz tu

ii nchi umejaa kila aina ya uchafu na dhambi alafu tunataka tuishi kama peponi

labda na sisi tumrudie Mungu maana wao ndio silaha yao kubwa DINI
 
Huyo mfalme anapiga bia kama hana akili nzuri!...ila yeye anakataza raia wake kutumia...

Kazi yake kuwala akina Beyonce, Mariah Carey, Pamela Anderson etc kwa pesa chafuu, sema mle kwenye Kasri wanaingia kwa siri mno..
Beyonce wa jay z 😳 😳 😳
 
Lau kama watu wangekuwa wana akili za kuzingatia mambo;
Utawala wa kiislamu ndio suluhisho la matatizo yote ya dunia hii
Mkuu mbona huko kwa wenyewe hatusikii amani kila kukicha ni vita na kulipuana,eti wanajitoa muanga.
Halafu wakishatibuana wanakimbilia kwenye nchi za watu wanaowaita makafiri.
 
Viongozi wao Mkuu wameweka mbele maslahi ya nchi yao na Wananchi wao siyo kwetu hapa hawa wanaojiita viongozi wameweka mbele matumbo yao miaka nenda miaka rudi sasa tunarudi nyuma miaka 60 iliyopita!

Watu wako na Mafuta na Gasi tu wanaishi km Paradise ,sisi tuna kila kitu ovyooo
 
Ninawaonea huruma hao wananchi bila shaka hata smartphones huko hamna coz wanafungwa kuona au kuskia ya nje
 
79f7f58663a088142e9daea071a94169.jpg



1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi yeyote (All citizens in Brunei, including expats, do not have to pay for taxes, for it is absolutely free.), Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000) huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu.

Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi na wanachi wanakula bata watakavyo.

GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA MIA....

2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).

Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.

3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali

4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NOA/NGURUWE hata mmoja nchi nzima....................

5. . Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei

6. Hii inatumia mfumo wa SHARIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk..........

7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA UCHAGUZI......Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali...ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali

8. 93% YA WATU WOTE WAMEENDA SHULE KWA KIWANGO CHA LAMI (Degree)
Hao wanajua maana ya kutumia vyema raslimali zao sio huku kwetu wizi tu
 
wakati mwingine unaweza ukafikiria hivi sisi waafrica nani katuroga?

Rathili mali zipo tena za kutosha, ila nchi zetu zinakosa viongozi wazuri wakuzisimamia na kuwaletea Maendeleo watu wake.

Tukilinganisha Tanzania na nchi tajwa Tanzania ni Mara mia ya taifa hilo.

Lakini kwa miaka zaidi ya 50 tumeshindwa kuondoa umaskini kabisa.

Mungu Atusaidie sana yumkini tumemwacha Mungu na kuviandama Vinyago.
Nchi gani ya africa iliyoondoa umaskini kabisa?
 
Natamani nilale nikiamka niwe huko maana huku hewa ni nzito sana maana ni mchanganyiko na akina Bashite
 
Back
Top Bottom