KOLOKOLONI
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 2,476
- 2,371
Khaaa aaaaa khaaaa. Ukitaka kujua ulingabmnisho angalia Rais anapowatoa hao Watu kwenye Majeshi kuwapeleka Idara za Kiraia kanal anapewa Wilaya na ACP anapewa Wilaya,Major General anapewa Mkoa Kamishina wa Polisi anapewa Mkoa . Hivyo hayo macheo yanapambika tu kimajina nje ya humo majeshini kwenu hayana lolote .unawezampa hata mpa hadhi ya kamishna wa polisi,sawa tu ukitaka.
ila akijichanganya ndio haya ya kufokewa na contable wa polisi kama mtoto,maana hajui mipaka yake.
Kuna Lori juzi nimeona limeandikwa kwa nyuma 'PAKA HAWEZI KUISHI KWNY GHETTO LA MSELA'.
Askari wengi kitambo hicho walikua ni wakuryaKwanini askari wote "Haloo" wao huitamka "Aroo"[emoji1787][emoji1787]
OkSio sheria lakini imekaa kimazoea zaidi hadi imezoeleka kana kwamba ni sheria.
Kosa ni la aliye rekodi clip. Rejea shauri la watoa huduma za afya huko Uyui.Kuna video inatembea mitandaoni!
View attachment 2482273
Video ile inamuonesha mwanajeshi wa jeshi la wananchi akiwa na sare akiwa ni moja ya abiria kwenye bus (daladala) akizozana na askari wa usalama barabarani (trafiki)
Kipande hiko cha video kinaonesha kulikuwa na majibizano na lugha isiyofaa kabla!
Maneno machache yaliyosikika ni Mwanajeshi alijibu kwa kumwambia yule TRAFIKI kwamba! "Wewee huwezi kunionya Mimi wee paka tu"
Traffic alijibu kwa kuhoji "Mimi ni paka?
Mwanajeshi alijibu nae kwa kusema:
" Huwezi kunionya wewe Arooh nakucheki sana!
NANI ANA MAKOSA?
Hapo tukianza na mwanajeshi tunagundua either kwa kusahau au kwa kueleweka vibaya huenda baada ya gari alopanda (daladala) kukamatwa na kushikiliwa hakuona dalili njema za uadilifu kwa traffic ambazo zilionekana kuwachelewesha!
Hivyo kwa nia njema au mbaya huenda alimsihi yule TRAFIKI amalize kazi yake fasta wawahi!
Bahati mbaya huenda TRAFIKI aliitafsiri vibaya ile kauli ya manajeshi na kumuonya yule mwanajeshi! (Bad approach)
Kitendo cha TRAFIKI kumuonya yule mwanajeshi waziwazi kilikuwa na mlengo mbaya na mapokeo mabaya yanayoshusha hadhi ya JWTZ mbele ya RAIA (Na hapo ndipo unamuona mwanajeshi anapaniki kwamba unaweza kunionya wewe paka?)
Na baada ya TRAFIKI Polisi kugundua kwamba Kachemka, alitumia mwanya wa kuitwa PAKA kutafta kinga ya kisheria endapo mambo yataharibika!
Kimamlaka na sheria nani alikuwa sahihi?
Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani (Road traffic act) zinampa mamlaka ya kisheria askari wa usalama barabarani kukamata na kuadhibu chombo chochote cha moto kinachohisiwa kukiuka sheria za usalama barabarani pasipo kujali kimebeba nani!
Mamlaka hayo yakisheria yanamlazimisha TRAFIKI Kuongea na dreva wa chombo husika peke yake (SIYO ABIRIA)
ABIRIA anaweza kutoa maoni au taarifa ya kutokutendewa haki na dreva au chombo lakini HARUHUSIWI KUMUAMRISHA TRAFIKI kutekeleza kazi yake!
ABIRIA akifanya hivyo anakuwa katenda KOSA LA KUMZUIA ASKARI Kufanya kazi yake!
Kwa matinki hiyo TRAFIKI Anaweza kukamata CHOMBO CHOCHOTE CHA KIRAIA (siyo majeshi) hata kama chombo hicho kitakuwa kimebeba kikundi cha wanajeshi kiasi cha kuhatarisha usalama barabarani!
Hivyo kimamlaka ya usalama barabarani TRAFIKI alikuwa sahihi LAKINI ALIKOSA BUSARA!
Mwanajeshi alikuwa sahihi lakini hakutumia BUSARA kufikisha ujumbe wake!
Hapa nachoweza kusema Shamba la bwana kheri, Mbuzi wa bwana kheri!
Maelekezo ya kinidhamu yanayotolewa kila siku HAYAKUZINGATIWA na wawili hawa!
KUKOSA Kwao BUSARA Kunaweza pelekea migogoro ya mihimili miwili ya kijeshi!
Hivyo wote wawili wanastahili ADHABU kutoka wakuu wao na endapo watakuwa na makosa mengine nyuma kama hayo inashauriwa hata KUFUKUZWA KAZI!
Sasa asimamie bila kukamata? Ukikaidi maelekezo lazima ukamatwe nduguTrafiki kazi yake sio KUKAMATA ni kusimamia sheria hili neno kukamata ndio linafanya hata kosa liwe la maelekezo wanaanza usumbufu wa hela
Magereza kula yenu ipo kwa wafungwaNasisi Magereza tupo msitushau
Unadanganya watu hapaStaff sergeant wa JWTZ ana hadhi zaidi ya mrakimu wa jeshi la polisi, yaani yule afisa mwenye nembo ya bibi na bwana
MsameheUnadanganya watu hapa
Nafikiri bila ya kuangalia nani ana cheo gani, unapomkuta askari mwenzako japo ni jeshi tofauti, yuko kwenye majukumu yake, huna sababu ya kumuingilia. Ubabe wa kijinga wa jwtz daima ni tatizo kwa Tz. Wao ndio wakuendesha magari yao upande tofauti, na wanajiona ndio wako juu ya wote.Kuna video inatembea mitandaoni!
View attachment 2482273
Video ile inamuonesha mwanajeshi wa jeshi la wananchi akiwa na sare akiwa ni moja ya abiria kwenye bus (daladala) akizozana na askari wa usalama barabarani (trafiki)
Kipande hiko cha video kinaonesha kulikuwa na majibizano na lugha isiyofaa kabla!
Maneno machache yaliyosikika ni Mwanajeshi alijibu kwa kumwambia yule TRAFIKI kwamba! "Wewee huwezi kunionya Mimi wee paka tu"
Traffic alijibu kwa kuhoji "Mimi ni paka?
Mwanajeshi alijibu nae kwa kusema:
" Huwezi kunionya wewe Arooh nakucheki sana!
NANI ANA MAKOSA?
Hapo tukianza na mwanajeshi tunagundua either kwa kusahau au kwa kueleweka vibaya huenda baada ya gari alopanda (daladala) kukamatwa na kushikiliwa hakuona dalili njema za uadilifu kwa traffic ambazo zilionekana kuwachelewesha!
Hivyo kwa nia njema au mbaya huenda alimsihi yule TRAFIKI amalize kazi yake fasta wawahi!
Bahati mbaya huenda TRAFIKI aliitafsiri vibaya ile kauli ya manajeshi na kumuonya yule mwanajeshi! (Bad approach)
Kitendo cha TRAFIKI kumuonya yule mwanajeshi waziwazi kilikuwa na mlengo mbaya na mapokeo mabaya yanayoshusha hadhi ya JWTZ mbele ya RAIA (Na hapo ndipo unamuona mwanajeshi anapaniki kwamba unaweza kunionya wewe paka?)
Na baada ya TRAFIKI Polisi kugundua kwamba Kachemka, alitumia mwanya wa kuitwa PAKA kutafta kinga ya kisheria endapo mambo yataharibika!
Kimamlaka na sheria nani alikuwa sahihi?
Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani (Road traffic act) zinampa mamlaka ya kisheria askari wa usalama barabarani kukamata na kuadhibu chombo chochote cha moto kinachohisiwa kukiuka sheria za usalama barabarani pasipo kujali kimebeba nani!
Mamlaka hayo yakisheria yanamlazimisha TRAFIKI Kuongea na dreva wa chombo husika peke yake (SIYO ABIRIA)
ABIRIA anaweza kutoa maoni au taarifa ya kutokutendewa haki na dreva au chombo lakini HARUHUSIWI KUMUAMRISHA TRAFIKI kutekeleza kazi yake!
ABIRIA akifanya hivyo anakuwa katenda KOSA LA KUMZUIA ASKARI Kufanya kazi yake!
Kwa matinki hiyo TRAFIKI Anaweza kukamata CHOMBO CHOCHOTE CHA KIRAIA (siyo majeshi) hata kama chombo hicho kitakuwa kimebeba kikundi cha wanajeshi kiasi cha kuhatarisha usalama barabarani!
Hivyo kimamlaka ya usalama barabarani TRAFIKI alikuwa sahihi LAKINI ALIKOSA BUSARA!
Mwanajeshi alikuwa sahihi lakini hakutumia BUSARA kufikisha ujumbe wake!
Hapa nachoweza kusema Shamba la bwana kheri, Mbuzi wa bwana kheri!
Maelekezo ya kinidhamu yanayotolewa kila siku HAYAKUZINGATIWA na wawili hawa!
KUKOSA Kwao BUSARA Kunaweza pelekea migogoro ya mihimili miwili ya kijeshi!
Hivyo wote wawili wanastahili ADHABU kutoka wakuu wao na endapo watakuwa na makosa mengine nyuma kama hayo inashauriwa hata KUFUKUZWA KAZI!
Masuala mengi yanahitaji busara na hekima kuliko hata hizo sheria unazosema....mara ngapu hawa watu wanashikana masharti na kutwangana barabarani.....??Issue ni kuheshimiana na kusitiriana tu....maisha yaende..ukikazana na sheria kuna siku mtu atavunjwa kiuno na hakuna kitakachofanyikaWENGI Hawaijui sheria ya usalama! TRAFIKI wakiamua wanaweza kamata na kusweka lupango Mwanajeshi akivunja sheria ya usalama barabarani
Jeshi la Police lina watu Wengi ambao hawajui Sheria wala Mipaka yao wapo wapo tu, Wanataka kuburuza kila mtu wakidhani wao wana mammlaka sana tena wengine ni Seniors kabisa na hawataki Walau Kusoma au Kujua Miongozo yao
Sio hawapatani, hata raia hawawapendi paka.Kazi za jeshi ni ngumu zinahitaji morali sio kama polisi pushups kwenye Godoro sisi makamanda pushups kwenye kokoto... haiwezekani kamanda maji kupanda mlima
sasa kama me nikiwa depo naimba nyimbo za hivi... kwel polisi nitakuwa namwonaje.... hili bifu lipo tangu zamani hawapatani hawa
Hivi polis na mjeshi unaweza kusema nani yupo Juu Juu zaid kiukisema chuki unakuwa umeenda mbali,hakuna chuki ila kuna tabia ya kujiinua.hakuna anayekubali kuwa ndama.